Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, September 6, 2016

Magonjwa Sugu Yanayotibiwa Na Kitunguu.

No comments :
Kazi kubwa sana ya mbogamboga pamoja na viungo mbalimbali  na matunda tunayokula ni kuilinda na kuirekebisha mifumo mbalimbali ya ufanyaji kazi iliyoharibika mwilini.
Kuharibika kwa mifumo hii kunasababishwa na uharibifu wa mazingira, uchovu wa mwili, kuingia kwa vijidudu visivyotakiwa mwilini kama vile virusi au bacteria, na wakati mwingine mifumo hii huharibiwa na sumu kutoka kwenye madawa ya kuulia wadudu wa majumbani.
Nikisema wadudu wa majumbani, nina maana inzi, mbu, mende, komba mwiko na wengine.
Hivyo basi ni vyema tukawa waangalifu kwenye kilimo tusitumie mbolea kali sana au zenye kemikali kwa wingi, vilevile tusitumie madawa makali kwenye kuua wadudu waharibifu wa mazao kwa kuwa sumu hizi huchukua muda mrefu kuisha nguvu yake.
Mboga mboga au matunda ili yalete afya iliyokusudiwa ni muhimu kutilia maanani usafi kabla ya kutumia.
Kama tunatumia mbogamboga na matunda kama dawa au  kinga kwa matatizo fulani, ni lazima mtumiaji aweke nia ya kufanya hivyo na kufuata taratibu zake, kwani miaka mingi vitu hivyo vinatumika kwa namna hiyo. Kumbuka kuwa pia mwili una namna yake ya asili ya kujikinga na kijitibu.

Hebu tutazame kitunguu. Kitunguu ni kiungo kinachotumika kama dawa ya asili, kwa kuwekwa kwenye chakula au mboga wakati wa kupika, vilevile huwekwa kwenye kachumbari.
Kuna aina kama tatu hivi za vitungu maji. Kuna vile vyeupe, vyekundu na vya njano.
Aina nzuri sana na yenye manufaa kwa afya zetu ni vitunguu vyeupe. Inaaminika kuwa asili ya vitunguu hivi ni Asia ya kati, inawezekana kuwa ni Iran au Pakstani.
Kitunguu kimekuwa kikitumika kama dawa na kinga nzuri kwa muda mrefu bila wengi kujua. Kwa mfano, kitunguu kina protini kiasi, kimejaa madini ya calcium na riboflavin kwa wingi sana.
Kwa kila gram 100 kuna majimaji asilimia 86. 6, protini asilimia 1.2, mafuta asilimia 0.1, nyuzinyuzi asiimia 0.6, wanga asilimia 11.1, madini mengine yaliyomo ni pamoja na phosphorus, chuma, carotene, thiamine, nicin na vitamin C.
Kwa hiyo tunapokuja katika suala la tiba, kitunguu kinaweza kutibu matatizo kama; kifua kikuu. Juisi ya kitunguu ikitumika kijiko cha chai asubuhi na jioni inaondoa tatizo hili. Unaweza ukachanganya na asali au sukari guru.
Pia matatizo kwenye njia ya hewa (upumuaji). Kitunguu kinayeyusha mgando kwenye mishipa ya damu na kuzuia isikae kwenye njia ya hewa, hivyo hutibu kikohozi, mafua na matatizo ya mapafu.
Vijiko vidogo vitatu vya juice yake, vilivyochanganywa sawasawa na asali mara mbili kwa wiki ni dawa tosha.
Vitunguu vina madini ya chuma yanayoyeyuka kirahisi sana mwilini na hiyo ni vizuri sana kutibu ukosefu wa damu.
Magonjwa ya moyo. Kwa kuwa kitunguu kina mafuta asili, madini mabalimbali pamoja na vitamin kadhaa, kinasaidia kuondoa sumu zinazoweza kuudhuru moyo na hivyo kuondoa mchafuko kwenye mishipa ya damu.
Ni vyema kutumia gram 100 za kitunguu kwa siku.
Kindupindu; chukua gramu 30 za vitunguu na pilipili manga 7. Pondaponda kwa pamoja, mpe mgonjwa. Unaweza kuongeza asali au sukari kidogo.
Huleta kiu, kuchoka na kuzuia au kupunguza kutapika.
Matatizo ya meno; pia matataizo haya huweza kutibika kwa kutafuna ganda moja la kitunguu kwa siku, huuwa vijidudu vibaya kinywani na kwenye meno.
Matatizo ya ngozi; kitunguu kinachachatika kwenye ngozi na kinaamsha mzunguko wa damu. Tatizo la kwenye ngozi lilosababishwa na virusi, chukua kitunguu kikate katikati, halafu sugua kwenye ngozi iliyoliwa.
Kitunguu kinafaa kwa mambo mengi sana, tukitumie hasa kikiwa kibichi, kwani kikipikwa kinakuwa kigumu kusagwa mwilini.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
No comments :

Post a Comment