Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, September 15, 2016

Mambo Ya Msingi Ya Kuzingatia Katika Kufanya Uchunguzi Wa Kibiashara.

No comments :
Moja ya changamoto kubwa inayowakabili wafanyabiashara wengi ni kutokujua kwa undani jinsi ya kufanya utafiti wa kimasoko katika biashara ambayo anaifanya au anataraji kuifanya, na kutokana na changamoto hiyo,  imepelekea biashara nyingi kushindwa kukua na hata kupelekea baadhi ya biashara nyingine kufa kabisa.

Hivyo ni jambo jema ukayafahamu mambo ya msingi yahusuyo masuala ya masoko katika kibiashara ili kuweza kukuza biashara yako na hatimaye kupata faida.

Yafuatayo ndiyo mambo ya msingi ya kuzingatia katika kufachanya uchunguzi wa masoko.

1. Nani atakuwa ni mteja wako?

Hili ni swali la msingi la kujiuliza. Kwa mfanyabiara yeyote ni lazima aweze kutafakari kwa makini zaidi ni nani ambaye atanunua bidhaa au huduma ambayo unaitoa. Katika kujiuliza swali hili ni lazima uweze kumchanganua mteja wako kwa kuangalia mambo yafutayo;

Uwezo  wa kiuchumi kwa wahitaji wa bidhaa au huduma.

Kwa kutazama uwezo wake wa kifedha ni vyema ukajiuliza je kwa bidhaa au huduma ambayo ninaiuza mteja wangu ana uwezo wa kununua?. Kwa mfano, huwezi ukafungua biashara ya ‘supermarket’ maeneo ya vijijini kwani hali ya maeneo mengi ya vijinini hawana uwezo Wa kuweza kununua bidhaa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na mjini.

Angalia ukubwa wa soko lako katika kuchunguza biashara.
Umri na jinsia.

Ni vyema ukajiuliza kuhusu watumiaji wa bidhaa au huduma yako kwa kuangalia uhitaji wa bidhaa yako kwa kujiuliza je, ni umri gani ambao watatumia zaidi bidhaa yako? Na ni lazima ujiulize ni jinsia gani watapendelea zaidi kutumia bidhaa yako? Ukipata majibu sahihi ndipo utakapojua ni biashara gani utaifanya katika eneo husika.

2. Upi ukubwa wa kisoko?

Hili pia ni suala la msingi la kuweza kuzingatia hususani suala zima la kufanya biashara yenye ubora na yenye kukua. Watu wengi huwa hawalizingatii hili na hivyo kupelekea biashara kufa, lakini kujua ukubwa wa soko huusisha masuala ya uhitaji wa bidhaa au huduma, kufanya hivi kutakusaidia kwa kiwango kikubwa kujua uwezo wa kuzalisha kwa kiwango gani kulingana na uhitaji wa wateja wako.

Soma; Mawazo Muhimu Unayotakiwa Kuwa Nayo Ili Kukuza Biashara Yako.

3. Bei itakuwa ni kiasi gani?

Kwa mjasiriamali yeyote ni vyema ukajua namna ya kupanga bei katika biashara yeyote ambayo unaifanya au unataka kufanya, kama utakuwa ni mdau mzuri wa mtandao huu nilieleza namna ya kuweza kupanga bei katika biashara yako.

Kwa harakaharaka nikukumbushe ya kwamba katika upangaji wa bei ni lazima uangalie uhitaji wa bidhaa, gharama za uzalishaji na uendeshaji na pia ni lazima uwatazame washindani wenzako wanafanyaje katika biashara hususani suala zima la kupanga bei.

Soma; Mbinu Bora Za Kupanga Bei Katika Biashara.

4. Namna ya kufikisha huduma/bidhaa kwa walengwa.

Hili ni jambo muhimu kuweza kulifahamu. Katika biashara yeyote ile kuna njia mbili za kufikisha huduma au bidhaa kwa wateja. Jambo la kwanza ni kuweza kufikisha bidhaa moja kwa moja kwa mteja, njia hii humkutanisha mzalishaji na mteja.

Na jambo la pili kuweza kufikisha bidhaa kupitia ununuzi rejareja au kwa jumla, njia hii haimkutanishi mzalishaji na mteja. Mfano mzuri kama tufanyavyo kununua vitu kwa madukani kwa mangi. Hivyo katika kufanya utafiti wa kimasoko ni lazima ujue namna na mbinu ambazo zitakufanikisha kufanya biashara kwa ufanisi hatimaye kupata faida.

Endelea kutembelea mtandao huu kila Mara ili kujifunza vitu vitakavyobadili Maisha yako kwa namna moja ama nyingine.

Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.

Ndimi; Benson Chonya
0757909942


No comments :

Post a Comment