google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 2, 2017

Mafanikio Makubwa Yanajengwa Sana Na Mambo Haya.

No comments :
Watu wengi wenye mafanikio makubwa kiuchumi  huwa ni watu wa kufanya mambo fulani ambayo yanawasaidia sana kujenga mafanikio yao kila siku. Kwa kufanya mambo hayo huweza kuwaongoza moja kwa moja kufikia mafanikio makubwa katika maisha yao.
Na mara nyingi watu hawa wenye mafanikio makubwa, kwao inakuwa ni vigumu kuweza kuacha kufanya mambo hayo. Huwa ni watu wa kufanya mambo hayo karibu kila siku na kila mara.
Katika makala haya tutaangalia mambo muhimu yanayojenga mafanikio. kama nilivyosema haya ni mambo ambayo yanatumiwa karibu na watu wote wenye mafanikio makubwa. Hata wewe unaweza ukajifunza mambo haya leo na kujenga mafanikio makubwa.
Fuatana nasi katika makala hii kuyajua mambo hayo zaidi:-
1. Kujifunza.
Hili ndilo jambo la kwanza linajenga mafanikio yoyote yale. Maisha ya watu wote wenye mafanikio makubwa kwa sehemu kubwa yametawaliwa na kujifunza sana.
Leo hii kama umeamua kujenga mafanikio yako makubwa ni lazima ujifunze tena sana na kila siku. Hii ni tabia ambayo itakupelekea kukufikisha kwenye mafanikio makubwa sana.

2. Kuweka vipaumbele.
Siri nyingine ya kujenga mafanikio makubwa ipo kwenye kuweka vipaumbele. Ili kufanikiwa ni lazima uwe mwekaji mzuri wa mipango yako kwa kuzingatia vipaumbele zaidi. Tambua bila kuweka vipaumbele itakuwa ngumu sana kwako kuweza kufanikiwa.
3. Kujitoa mhanga.
Mafanikio yote mara nyingi yanategemea pia kujengwa na tabia ya kujitoa mhanga ambayo unatakiwa kuwa nayo. Unapojitioa mhanga inakusaidia kufanya maamuzi magumu ambayo kwa mtu wa kawaida ni lazima ataogopa.
4. Nidhamu binafsi.
Hauwezi kufanikiwa kama kwenye maisha yako huna nidhamu binafsi. Mafanikio makubwa yanajengwa sana na nidhamu ambayo inatakiwa ikuongeze kila siku hadi kufikia kilele cha mafanikio yako.
5. Kufanya kazi kwa bidii sana.
Hakuna mbadala wa hili kama una lengo la kutoka kwenye umaskini. Ili ufanikiwe unatakiwa kufanya kazi haswa tena sio kazi ya kitoto. Unapojituma kila siku mafanikio yatake yasitake ni lazima yatakuja upande wako.
6. Ung’ang’anizi.
Kwenye maisha zipo changamoto nyingi sana. Sasa ili uweze kujenga mafanikio yako kwa uhakika ni lazima unatakiwa kuwa mbishi wa mafanikio yako. usikubali kushindwa kirahisi, hiyo itakuwa ni hasara kubwa sana na utashindwa kufanikiwa.
7. Kuuliza.
Kujenga mafanikio makubwa ni lazima kila wakati ujiulize maswali yatakayokusaidia kukutoa hapo walipo na kwenda ngazi nyingine kimafanikio. Usiwe msikilizaji au mpokeaji wa moja kwa moja bila kupata muda wa kudadisi na kuuliza. Uliza upate msaada na kujenga mafanikio yako.
8. Maliza kile unachokianza.
Watu wenye mafanikio si waanzaji tu wa mambo mapya mengi, bali pia ni watu wa kumaliza kile walichokianza. Wanapopanga mipango yao ni lazima mwisho wa kumaliza wauone na ndicho kitu ambacho kinakuwa kinafanyiika mpaka kufikia ndoto zao.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.