Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, February 1, 2017

Amua Kuwa Hivi Katika Kuyasaka Mafanikio.

No comments :
Mwandishi fulani wa masuala ya mafanikio jina tunalihifadhi kwa sababu za kiufundi aliwahi kuandika ya kwamba "awezavyo mtu akilini mwake ndivyo alivyo". Ukifikiria kwa umakini bila kuiruhusu akili mgando katika kuwaza utajua ya kwamba usemi huo ni ukweli kabisa.

Unajua ni kwanini ukweli huo ni ukweli? ipo hivi miongoni mwa na sababu ya sisi kuendelea kuwa katika hali ya umaskini kila wakati, inatokana na vile ambavyo tunaweza na kuamini katika akili zetu.  Wengi wetu tumekuwa na mawazo mgando ambayo yamekuwa hayana msaada wowote katika kupiga hatua za kimaendeleo na kimafanikio.


Mawazo hayo mgando yamekuwa yakitendeka na mwisho wa siku tumejikuta tukiwalamu watu wengi ambao wanatuzunguka ikiwemo serikali, ndugu jamaa na marafiki. Licha ya kuendelea kulaumu mawazo hayo mgando yamekuwa ni kizuizi katika safari ya mafanikio.

Hivi hajawahi kukutana na mtu anasema ya kwamba  hawezi kufanikiwa milele? Hii ni kutokana na mtu huyo amekwishakata tamaa?  Bila shaka umewahi kukutana na aina hii ya watu,  kama hajawahi kukutana na watu wa aina hii huenda ukawa ni wewe.

Amua kuwa wa tofauti katika kuyasaka mafanikio yako.
Lakini ukweli ni kwamba hatma ya maisha yako inatokana na wewe mwenyewe vile ambavyo ameamua kuwaza na kuchukua hatua ya kile ambacho unawaza.  Vilevile maisha ya kimafanikio yatakuwa na nafasi kwa upande wako endapo "utaaamua kuwa wewe"

Kuwa wewe ni ndo siri kubwa ya mafanikio yako,  hata siku moja usiruhusu mtu awaze juu yako,  au uamue kuwaza vitu vingine ambavyo watu wengine wanawaza. Tunashindwa kufanikiwa kwa sababu vitu ambavyo tunavifanya kuna mtu alisema tufanye kwa sababu vinalipa.


Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanalalamika ya kwamba biashara ngumu kwa sababu waliona mtu fulani amefanya na wao wakaamua kufanya, lakini leo hii wanalalamika ya kwamba biashara ni ngumu.  Sababu ya kutokea kwa hali hiyo ni kwamba hawajafanya kuwa wao ila wameamua kufanya mawazo ya watu wengine.

Lakini ikumbukwe ya kwamba masuala ya kimafanikio kwa upande wako yatakuja kama utaamua kuwa wewe kwa kufanya kitu ambacho kitatoka nafsi mwako.  Kwani kufanya hivi utakifanya kwa moyo wako wote na    si vinginevyo.

Nimalize kwa kusema acha mawazo mgando amua kuwa wewe ama hakika utafanikiwa. Mwisho nikutakie maisha mema yenye mafanikio tele.

Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.

Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.

TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya


No comments :

Post a Comment