google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 7, 2017

Sababu Ya Bidhaa/ Huduma Kushindwa Kufanya Vizuri Katika Mzunguko Wa Kibiashara.

No comments :
Bidhaa ndiyo alama ambayo inayomtambulisha mfanyabiashara fulani katika biashara. Kwa mfano leo ukiona bidhaa fulani unajua kabisa ni nani ambaye ametengeneza bidhaa hiyo. Lakini siku zote ni kwamba ili tuweze kukua kibiashara ni lazima tutafute upekee wetu katika biashara husika.

Watu wengi tunafanya biashara lakini hatutafuti utofauti wetu na wafanyabiashara wengine, na kufanya hivyo kumesababisha biashara nyingi kufa kabla ya wakati. 

Na hizi baadhi ya sababu ya kufa kwa bidhaa au huduma katika mzunguko wake;-.
Ubora hafifu wa bidhaa.

Kuwepo kwa ubora hafifu katika bidhaa au huduma yeyote ambayo unaitoa hiyo ndo chanzo cha kufa kwa biashara nyingi.  Hivyo kwa kuwa unasoma hapa kwa lengo la kupata mawazo chanya ya kukuza biashara Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha inazalisha bidhaa zenye ubora kila wakati. 

Kuzalisha bidhaa bora kila wakati ndo chanzo cha kukuza biashara yako na hatimaye kupata faida kubwa. Hivyo ikumbukwe ya kwamba ukitaka kujitofautisha na wafanyabiashara wengine hakikisha ya kwamba unazalisha bidhaa bora.



Uhaba wa njia mathubuti za usambazaji.

Hii ni  sababu nyingine ambayo inachangia bidhaa nyingi kushindwa kukua katika soko ni kuwepo kwa uhaba wa njia mathubuti za usambazaji wa njia za kutosha wa bidhaa kutoka kwa mfanyabiashara kwenda kwa mteja. 

Hivyo kama kweli unataka mafanikio ya kibiashara Unachotakiwa kufanya ni hakakikisha unafanya vizuri katika suala zima la usambazaji wa bidhaa yako kutoka kwako kwenda kwa mteja.  Kama una uwezo pia wa kusambaza bidhaa kwa kumpelekea mteja wako huduma mahali ulipo. 

Kupanda kwa bei kiholela . 

Sababu nyingine ambayo husababisha  bidhaa kufa kabla ya wakati ikiwa sokoni ni pamoja na kupanda na kushuka kwa bei ya huduma au bidhaa. Kufanya hivyo ni dalili tosha ya kuwayumbisha wateja wako. 

Hivyo ili kuweza kushinda vikwazo ambavyo vitasabaibisha kufa kwa biashara yako hakikisha unakuwa na utaratibu maalumu. Ikiwezekana wajuze wateja wako juu ya upandaji wa bei mwezi mmoja kabla ya bei ya bidhaa yako kupanda. 

Na kufanya hivyo kuyafanya mteja wako ajisikie huru kama ni sehemu ya ufalme, maana kuna usemi husema mteja ni mfalme. 

Kutoa huduma au bidhaa isiyohitajika kwa watu. 

Mara nyingine umekuwa ukilalamika ya kwamba inawezekana ukawa umelogwa katika biashara yako,  hii ni kutokana umekuwa huoni faida. Lakini ukweli ni kwamba hakuna ambaye amekuloga zaidi ya kujiloga mwenyewe. 

Hivyo ili uweze kukua katika biashara yako kama nilivyoeleza katika makala haya unatakiwa kufanya uchunguzi wa kile ambacho wateja wako wanaohitaji kwa wakati sahihi. 

Ukifanya uchunguzi wa kile ambacho wateja wako ambacho wanaohitaji utasababisha kufanya ongezeko la mauzo na wateja kwa ujumla. Hivyo hakikisha unatoa huduma sahihi kwa wakati sahihi ama hakika biashara yako itafanikiwa. 

Ndimi afisa Mipango : Benson Chonya,
bensonchonya23@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.