Aug 13, 2015
Hii Ndiyo Sababu Kubwa Inayokufanya Uahirishe Mambo Yako.
Kuna
wakati ambapo Professa mmoja kutoka chuo kikuu cha Havard, Marekani aliwahi
kufanya utafiti ambapo alitaka kujua ni kwa nini hasa watu wengi huwa wana
tabia ya kuahirisha mambo yao mara kwa mara. Aliamua kufanya utafiti huo mara
baada ya kutambua kuwa kuahirisha mambo ni moja kati ya tabia inayokwamisha
wengi katika safari yao ya mafanikio.
Bila
shaka hata wewe unaweza ukawa shahidi katika hili ni mara ngapi hasa umekuwa
ukiona watu ama wewe mwenyewe binafsi ukiahirisha mambo yako mengi zaidi,
ambayo yangeweza kukusaidia kusonga mbele? Najua ni mara nyingi umekuwa ukifanya
hivyo na pengine bila kujiuliza kwa nini
iko hivyo.
Katika
utafiti wake huo ilikuja kubainika kuwa binadamu kama binadamu huwa anatabia ya
kuahirisha mambo inayotokana na kitu kimoja tu. Kitu hicho ni kupenda kuwa huru
na kufurahia maisha ya sasa na kuweza kusahau mambo ya baadae. Kufurahia maisha
ya sasa inaweza ikawa ni kupenda kulala sana, kuongea, kutembea, kuangalia tv au
mpira na mengineyo. Lakini hii ndiyo
sababu inayofanya wengi wawe wanaahirisha mambo yao.
SOMA; Huyu Ndiye Mtu Pekee Anayekufanya Ushindwe Katika Maisha Yako.
Unaweza
ukawa bado hujanielewa vizuri lakini iko hivi, kwa mfano unaweza kuwa una kazi
ambayo unataka kuifanya sasa hivi lakini wakati huohuo unakuwa unapenda kuongea
na rafiki yako kwenye simu au unataka kuperuzi kwenye mtandao. Kwa namna yoyote
ile unaweza ukajikuta unaahirisha hiyo kazi unayotaka kufanya ambayo ni muhimu
kwako na kuamua kuongea na huyo rafiki yako.
Kwa
kufanya hivyo utakuwa moja kwa moja umependa kufurahia maisha ya sasa na kuweza
kusahau kazi yako ambayo pengine ni muhimu sana kwa faida ya baadae katika
maisha yako. Hivi ndivyo inavyotokea na wengi ndivyo huwa wanajikuta wanaarisha
mipango na malengo yao mazuri waliojiwekea siku hadi siku.
Unaweza
ukatambua ambavyo mtu kwake inaweza kuwa rahisi kuweza kutumia pesa zake hovyo
kwa sababu ya starehe za leo na za muda mfupi na kusahau kujikita katika suala
zima la uwekezaji. Hiyo yote inakuja kwa sababu ya kupenda kufurahia maisha ya
sasa na kusahau kabisa maisha ya kesho
ambayo yanaweza kuwa ni msaada mkubwa kwake.
Hivyo,
mtu kwa hali hiyo hujikuta akisema nitafanya hili kesho ama kesho kutwa na
kupelekea siku nyingi kuweza kusonga mbele bila kufanya ama kubadili chochote
katika maisha yake. Jaribu kuchunguza hili kwa makini utagundua ninachosema
hapa, mara nyingi unapenda kuahirisha mambo kwa sababu ya starehe fulani fulani
za leo au uvivu, huu ndiyo ukweli.
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kukabiliana Na Changamoto Katika Maisha Yako.
Ili
uweze kuondokana na hali hiyo unatakiwa utambue kuwa uhuru unaotaka sasa au starehe, pengine
unazozifanya na ambazo zinakupelekea wewe kuacha majukumu haziwezi kukufikisha
popote. Elewa kabisa maisha yako unatakiwa kuyajenga wewe mwenyewe na siyo mtu
mwingine. Jifunze kutokuharisha mambo yako kwa gharama yoyote ile.
Kama
si hivyo jifunze kuangalia faida ya jambo hilo ikiwa hutaweza kuariahirisha.
Angalia matokeo chanya ambayo utayapata kwa kutokuahirisha kitu unachokifanya.
Kama utaendelea kuahirisha mambo yako utakuwa unajiwekea vikwazo wewe mwenyewe
vya kufikia mafanikio yako.
Ansante
kwa kwa kuwa msomaji mzuri wa DIRA YA MAFANIKIO, endelea kuwashirikisha wengine
kuweza kujifunza zaidi.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.