Aug 11, 2015
Kama Unaendekeza Tabia Hizi, Umaskini Kwako Utakuwa Ni lazima.
Tabia
tulizonazo mara nyingi ndizo zinajenga maisha yetu na kuweza kukutambulisha au
kutupa ishara halisi ya kuwa sisi tunaweza tukawa akina nani baada ya muda
fulani. Zipo tabia ambazo tukiwa nazo zinatupa uhakika wa sisi kuwa na
mafanikio na zingine tukiwa nazo zinaturudisha nyuma kabisa hadi kwenye
umaskini.
Je,
umeshawahi kujiuliza kwa nini mara kwa mara huwa inatokea unajikuta huna pesa
na hata pia ‘account’ yako nayo inakuwa haina kitu? Pengine umekuwa ukiuumiza
kichwa na kujiuliza ni wapi ulipokosea hasa? Kitu ambacho umekuwa hujui unakuwa
katika hali hiyo wakati mwingine kutokana na tabia ulizonazo.
Tabia
ulizonazo zina nguvu ya kuweza kubadili au kutengeneza maisha yako kwa kadri
jinsi unavyozitumia. Katika makala hii tutaaangalia tabia mbaya ambazo nyingi
ya hizo ukiwa nazo uwe na uhakikia huwezi kufanikiwa katika lolote zaidi ya
kuwa maskini. Ni tabia ambazo zimewaathiri wengi bila kujijua.
Fuatana
nasi katika makala hii kuzijua zaidi:-
1. Tabia ya kutumia pesa zaidi ya kipato
ulichonacho.
Kama
unatumia pesa hizo kwa kuwekeza upo sawa. Lakini kama unafanya matumizi makubwa
zaidi ya kipato chako, tambua na elewa kabisa upo kwenye mstari mwekundu wa
kuelekea kwenye umaskini tena wakujitakia. Wengi wenye tabia hii huwa ni watu
wa kuishi kwa madeni kila wakati na hali zao kifedha daima huwa ni mbaya siku
zote na maisha yao huishia pabaya.
Nini cha kufanya?
Ili
uweze kuondokana na hali hiyo jiwekee kiapo cha kutotumia pesa zaidi ya zile unazopata.
Kaa chini kisha tafakari, na amua kuwa na matumizi tu ya kawaida ambayo hayataweza
kukugharimu na kukuharibia maisha yako kwa ujumla.
SOMA; Tabia 8 Muhimu Unazotakiwa Kuwa Nazo, Ili Kujenga Maisha Ya Mafanikio Makubwa.
2. Tabia ya kushidwa kujiwekea akiba.
Kinaweza
kuwa ni kitu cha kawaida kwako lakini ni hatari kwa afya ya mafanikio yako.
Kama utaendelea kuwa na maisha ya kuwa unapokea tu pesa halafu unashindwa
kujiwekea angalau kiasi kidogo ambacho kinaweza kukusaidia kwa baadae uwe na
uhakika pia kufanikiwa kwako itakuwa kugumu kidogo hata kama hutaki kukubali
ukweli huu.
Nini unachotakiwa kufanya sasa?
Anza
kujiwekea utaratibu wa kujiwekea pesa zako wewe mwenyewe. Kiasi chochote cha pesa
unachopata tenga asilimia fulani ambayo utaiweka. Inaweza ikawa asilimia kumi
ambayo itakusaidia katika shughuli nzima ya kuwekeza kwa hapo baadae pesa hizo
zitakapokuwa nyingi tayari.
3. Tabia ya kutokujiwekea kumbukumbu.
Wengi
wetu mara nyingi huwa tunatabia ya kutokuweka kumbukumbu hususani kwa pesa
tunazozitumia. Huwa ni watu makini kwa baadhi ya matumizi lakini ukweli unakuja
palepale kuwa matumizi mengine ya pesa hasa yale madogo madogo huwa hatupo
makini nayo hali ambayo huweza kutupelekea kupoteza pesa nyingi bila sababu.
Nini cha kufanya?
Ili
kuweza kuondokana na tabia ya kupoteza pesa hovyo ni vizuri tukajiwekea
utaratibu ambao utakuwa unaweka kumbukumbu kwa kila shilingi unayoitumia. Kwa
kuweka kumbukumbu hizo itakusaidia kuweza kuepuka matumizi yasiyoyalazima
kwako.
SOMA; Ili uweze Kufanikiwa, Una Haja Ya Kujifunza Zaidi Juu Ya Kitu Hiki Katika Maisha Yako.
4. Tabia ya kutokujiwekea bajeti.
Pesa
yoyote ambayo inatumika bila kuwa na bajeti maalumu siku zote huwa inatumika
hovyo tu. Watu ambao wanaishi maisha ya kutojiwekea bajeti huwa ni watu wa
kutumia pesa kiasi cha kwamba huwa inafika mahali hawaelewi hizo pesa zao
zimekwenda wapi. Kutokana na hali hiyo huwa ni sababu tosha ya kuwapeleka
kwenye njia ya kuelekea kwenye umaskini bila hata wao kujitambua.
Kitu gani cha kufanya?
Kitu
pekee cha kufanya hapa ni kuhakikisha unatengeneza utaratibu wa kujiwekea bajeti
na kuhakikisha ni lazima unaifata. Kwa kufuata bajeti hiyo ni lazima
utafanikiwa na utaondokana na matumizi ya hovyo ambayo ni rahisi kwako kuweza
kukurudsha kwenye umaskini.
SOMA; Kama Unataka Kufanikiwa Na Kuwa Tajiri, Acha tabia Hizi.
5. Tabia ya kutokujali sana mambo ya
leo.
Ili
uweze kujihakikishia mafanikio yako ya kesho unahitaji kufanya mambo yako kwa
ubora zaidi kila siku. Kama leo utafanya vizuri zaidi ya jana na kesho ukafanya
vizuri zaidi ya leo uwe na uhakika hakuna mtu wala kitu kitakachoweza kukuzuia
kwenye njia kuelekea ya mafanikio. Wengi huwa wanashindwa kufanikiwa kutokana
na kutokujali hilo.
Wengi
ni watu wakijikuta ni wa kusema kuwa nitafanya hiki na kile kesho ama siku
nyingine na kujisahau kabisa kuwa leo ni siku muhimu kwa mafanikio yao kuliko
wanavyofikiri. Kwa kutokujali leo hivyo hujikuta ni watu wasio na mafanikio
katika maisha yao kwa sehemu kubwa sana.
Kitu cha kufanya ni nini?
Ni
muhimu kutambua kuwa leo ni msingi wa mafanikio yako makubwa ya kesho. Kwa
kulitambua hilo fanya kazi kwa bidii zote kama leo ndiyo siku yako ya mwisho.
Acha kukata tamaa na wala usichoke, ongeza na kuchochea bidii zote. Kwa
kutekeleza hayo uwe na uhakika ni alazima utafanikiwa.
Tunakutakia
kila la kheri katika safari ya mafanikio, endelea kuwashirikisha wengine
kutembelea mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku kwa kujifunza na
kuhamasika zaidi.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
§ 0713
04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.