Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, November 5, 2015

Huu Ndiyo Ufunguo Wa Lazima Unaotakiwa Kuwa Nao Ili Kufanikiwa.

No comments :
Moja ya changamoto kubwa inayopelekea malengo ya wengi kutokutumia, ni ile hali ya kukosa hamasa yakuendelea kwenye hayo malengo. Hamasa hii inapokosekana kwa malengo yoyote yale iwe kuamka asubuhi na mapema, kubadili tabia fulani au kubadili tabia ya matumizi mabaya ya pesa ni dhahiri malengo hayo hayawezi kutimia.
Hamasa ni kitu kikubwa sana kinachofanya wengi kushindwa kuendelea na malengo hayo hasa pale wanapoikosa. Hiyo yote inatuonyesha kwamba hamasa ni ufunguo mmojawapo wa mafanikio muhimu, ambao kila mtu mwenye nia ya mafanikio hatakiwi kuukosa. Kama utakosa jambo hili kila wakati, ni wazi hutaweza kufanikiwa.
Uzoefu unaonyesha hakuna kitu kitu chochote ambacho mtu anaweza kukifanisha ikiwa atakosa hamasa. Kwa hiyo kama unataka kujua kama uko kwenye njia sahihi ya kufanikisha malengo yako, angalia hamasa uliyo ndani yako. Una hamasa kubwa kiasi gani ya kukusukuma kwenye mafanikio?
Unaweza ukawa unaanza kujiuliza kazi kubwa ya hamasa nini na inafanya kazi vipi? Sikiliza, siku zote hamasa inasimama kwetu kama msukumo, au kitu cha kutusukuma kila siku kwenye kufanya malengo yetu tuliyojiwekea. Na hamasa hizi huwa zipo za aina mbili yaani hamasa hasi na hamasa chanya.
Unapokuwa una hamasa chanya hapa unakuwa unajisukuma mwenyewe, hakuna anayekwambia fanya hivi au vile kwa sababu unakuwa unajua faida ya jambo unalolifanya. Lakini unapokuwa na hamasa hasi, hii tunasema ni hamasa kama ya kusukumwa, unakuwa unafanya jambo pengine kwa sababu unaogopa kufukuzwa kazi. Tuchukulie upo kazini na bosi wako anataka mambo yaende vizuri ni lazima ufanye kazi kwa bidii na kwa hamasa, maana ukifanya kinyume na hapo utafukuzwa kazi.
Hivyo, hamasa yoyote ile iwe chanya au hasi ni muhimu sana kwetu lakini ingawa ile chanya ndiyo unayotakiwa kuwa nayo kwa sababu utafanya kazi zako bila kuchukia. Wengi wanaofanya kazi zao kwa hamasa hasi, mara nyingi hujikuta wakichukia kazi zao na kuziona mbaya. Mpaka hapo unaweza ukaona hamasa ni kama kipimo cha kujua tupo wapi na tuna hali gani kuelekea kwenye malengo yetu.
Kwa hiyo, hamasa ni kitu cha lazima kukuwezesha wewe kufanya jambo lolote bila kuchoka. Inapotokea umekata tamaa unaona huwezi kubadili tena tabia zako mbaya zinazokuzuia kwenye mafanikio kitu pekee kitakacho kunyaua hapo ni hamasa uliyonayo. Msukumo huu ni muhimu sana kwa wewe kuwa nao kwa jambo lolote hasa pale mambo yanapokuwa magumu.
Kama ni hivyo, ni lazima kila siku na kila wakati katika safari yako ya mafanikio hakikisha unayohamasa ya kutosha kukuwezesha kuendelea  mbele. Ni lazima uwe na hamasa hii itakayokufanya ufanye mambo hata yale unayohisi wakati mingine huwezi kuyafanya. Hilo ni lazima. Hamasa hiyo unaipataje kila siku? Ni rahisi tu:-
Kwanza, anza kwa kidogo.
Utajenga hamasa kubwa sana ikiwa utakuwa utaanza malengo yako kwa kidogo. Acha kutaka kubadili mambo makubwa kwa pamoja utakuwa unakosea. Kama umejiwekea malengo ya kukimbia anza kwa kidogo tu. Kama umejiwekea malengo ya kujisomea sana anza pia kwa kidogo.
Kumbuka katika kila eneo anza kwa kidogo hiyo itakupa nguvu ya kuendelea mbele na utajikuta umejenga hamasa ya kutosha kila siku. Wengi wanaofanikiwa kujijengea hamasa kubwa kila siku, kila kitu wanachokifaya huwa wanaanza nacho kwa kidogo na kisha huchukua uzoefu na kusonga mbele zaidi ya pale walipo.

DIRA YA MAFANIKIO
HAMASA NI LAZIMA KWA MAFANIKIO YAKO.
Pili, jiwekee malengo machache.
Siri ya mafanikio ipo kwenye kutekeleza malengo machache kwanza. Ikiwezekana jiwekee lengo moja tu kwanza ambalo utaamua kulifatilia usiku na mchana mpaka litimie. Lakini kitendo cha kuwa na malengo mengi inaweza ikawa ni sababu mojawapo ya kukatisha tamaa na kukosa hamasa.
Unapokuwa na malengo machache hiyo inakuwa inakupa nguvu na hamasa ya kutaka kuendelea kufanya siku hadi siku kwa sababu unakuwa unaona mendeleo ya malengo yako mapema. Hivi ndivyo hamasa kubwa inavyopotikana kila siku.
Tatu, jifunze kwa wengine.
Ni muhimu kujifunza kwa wengine kwa kile unachokifanya. Unaweza ukaangalia waliofanikiwa zaidi yako. Ama unaweza ukajifunza kupitia vitabu. Ikiwezekana unaweza ukakaa nao ili wakueleze nini kilichowasukuma na kufika hapo walipo.
Watu hawa utakaojifunza kwao ni lazima watakupa nguvu fulani ya kukuchochoa kuweza kusonga mbele na kukupa hamasa ya ajabu kwa kile unachokifanya.  Hamasa hiyo utakayoipata itakusadia kusimama katika nyakati zote za maisha iwe za kawaida au kukatisha tamaa.
Nne, weka wazi jambo unalolifanya.
Ili uweze kufanikiwa ni vyema ukaweka wazi jambo unalolitaka kulifanya. Kama umeamua kukimbia basi, unaweza ukaliweka lengo lako hilo kwenye mandishi au picha na likaonekana kwa uzuri kabisa. Kwa kufanya hivyo litakupa hamasa ya kufatilia malengo yako hayo mara kwa mara.
Kwa kufanya mambo hayo manne yatakusaidia sana kukupa hamasa ambayo utakuwa nayo karibu kila siku. Na kumbuka huu ndio ufunguo muhimu unaotakiwa kuwa nao kwa ajili ya mafanikio yako ya leo na kesho.
Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio iwe ya ushindi na endelea kuwashirikisha wengine kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,


No comments :

Post a Comment