google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 16, 2015

Mambo 4 Ya Kujifunza Pale Unaposhindwa Kufanikiwa Kwa Kile Unachokifanya.

No comments :
Kwa kila safari yoyote ya mafanikio duniani ni lazima iwe na changamoto zake. Hakuna mafanikio ambayo yanakuwa yanakuja moja kwa moja bila kukutana na changamoto. Mara nyingi changamoto hizi zinapotokea kwa wengine hupelekea kushindwa kufanikiwa kwa kile kitu ambacho wanakifanya.
Inapotokea ukashindwa kufanikiwa kwa kile unachokifanya kutokana na changamoto yoyote, ni nini ambacho huwa unafanya? Hapa ndipo ule umuhimu wa kujifunza kutokana na makosa huwa unakuja. Najua umewahi kusikia sana juu ya kujifunza kutokana na makosa pale unapokosea. Lakini je, umeshawahi kujiuliza ni mambo gani unayotakiwa kujifunza?
Yafuatayo Ni  Mambo 4 Ya Kujifunza Pale Unaposhindwa Kufanikiwa Kwa Kile Unachokifanya.
 1. Mafanikio hayaji mara moja.
Kwa lugha rahisi naweza nikasema kwamba mafanikio yote yanakuja hatua kwa hatua. Hakuna mafanikio yanayokuja mara moja. Kwa hiyo kushindwa kwa lile jambo unalolifanya ni ishara inayo onyesha kwamba ili kufanikiwa ni lazima kujaribu tena na tena mpaka kufanikiwa, ikiwa lakini umefanya kwa mara ya kwanza na kushindwa.
Itakuwa haina maana kwako na utakuwa hupo makini na mafanikio ikiwa utaka tamaa mara moja baada ya kushindwa. Ukishindwa jambo tambua huo siyo mwisho wako, bali ndio mwanzo wa mafanikio kwa sababu mafanikio hayaji mara moja. Ukijua hivyo mafanikio hayaji mara moja hutakaa ukisikitika pale unaposhindwa, zaidi utaongeza juhudi na uzoefu.

JIFUNZE KITU KUTOKANA NA MAKOSA YAKO.
2. Kujenga mafanikio inahitaji muda.
Pia unaposhindwa kufanikiwa katika jambo unalolifanya kwa mara ya kwanza, hiyo inatuonyesha kwamba mafanikio yanahitaji muda kuyajenga. Mafanikio sio kitu cha kutokea tu mara moja kama wengi wanavyofikiri. Unatakiwa ujipe muda wa kujaribu tena na tena mpaka matokeo chanya yatokee.
Watu wote wenye mafanikio, walitumia muda mwingi kuwekeza kwenye mafanikio yao. Hakuna mkato juu ya hilo, inabidi ujitume na kuwekeza muda wako vya kutosha ili ufanikiwe. Kama kuna jambo unalifanya usihisi kama vile unapoteza muda kama hupati matokeo ya haraka. Kumbuka siku zote kujenga mafanikio inahitaji muda.
3. Siyo rahisi kufanikiwa kama jambo unalolifanya hulipendi.
Kama kuna jambo unalifanya halafu ukawa hulipendi sana, elewa ukishindwa huo ndio utakuwa mwisho wako. Kanuni au sheria za mafanikio zinatufundisha kwamba ili uweze kufanikiwa ni lazima ulipende lile jambo unalolifanya kwa moyo wote.
Unapofanya jambo unalolipenda hata unapokosea inakupa nguvu ya kusonga mbele kwa kuweza kujaribu tena na tena. Hili ni jambo ambalo unatakiwa kulielewa kuwa utajifunza kutokana na makosa yako kama jambo hilo unalipenda kweli kutoka moyoni. Kinyume cha hapo haitawezekana kwako.
4. Kushindwa kwako ni ishara ya kwamba umechukua hatua.
Ni sawa umeshindwa kwa kile unachokifanya, lakini yote hiyo inakuonyesha kwamba umechukua hatua. Kama usingechukua hatua ya kufikia mafanikio yako, basi ni wazi ungebaki kama ulivyo. Kwa kuwa umelijua hilo endelea kuchukua hatua kwa kusonga mbele. Usihofie kukosea kwako, huo pia ni msingi wa mafanikio yako.
Ansante kwa kusoma makala hii, kumbuka kushindwa kwa kile unachokifanya ni njia mojawapo ya kukupeleka kwenye mafanikio ikiwa utajifunza. Usifanye kushindwa kwako kukakurudisha nyuma.
Ni kipi unachojifunza wewe pale unaposhindwa kwa mara ya kwanza kwa jambo unalolifanya? Unaweza ukanishirikisha machache hapo chini kwenye maoni, tukajifunza kwa pamoja.
Nikutakie ushindi katika safari yako ya mafanikio, kumbuka endelea kuwashirikisha wengine waweze kutembelea mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamasika.
Tupo pamoja katika safari ya kuyafikia mafanikio makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.