Nov 13, 2015
Kama Unaona Maisha Ni Magumu Utawezaje Kushinda?
Hebu
kaa chini na jaribu kujiuliza maswali haya kwa muda kidogo? Maisha yako ni
nini? Una mtazamo gani unapofikiria juu ya maisha yako? Je, maisha yako
yanakupa kile unachokihitaji? Haya ni maswali ambayo unapaswa kujiuliza ili
yakupe dira,mwelekeo na picha ya maisha yako unavyotaka yawe.
Namna
unavyoyaona maisha yako ndivyo unavyoyatengeneza. Namna ambavyo unaishi na
malengo ndiyo yanaeleza maana ya maisha yako. Watu husema vitu tofauti kuhusu
maisha kama vile maisha ni safari, maisha ni kitendawili kigumu, maisha ni kama
duara, maisha ni kama foleni au maisha ni mchezo mchafu.
Lakini
kila unapojiuliza wewe mwenyewe maisha ni nini! Unapata picha gani? Watu wengi
wanaelewa maisha kupitia mavazi, vitu vya thamani, magari, mtindo na pesa au
kwa namna nyingine kwa kadri jinsi wanavyoyatafsiri.
Picha
uliyonayo juu ya maisha inakuhamasisha kwa hayo uliyonayo. Kama una picha ya
maisha ni kama riadha utafanya mambo yako harakaharaka na kukazana. Kama una
picha ya maisha ni mapambano utafanya chochote kupigania maisha yako. Ila kila
siku upo katika mtihani au mchezo unaopaswa kushinda wala si kushindwa. Maisha ni
jaribio la muda mfupi. Kwenda ngazi nyingine unahitaji kushinda mtihani kila siku.
WEWE NI MSHINDI WA MAISHA YAKO. |
Maisha
yamegawanyika katika ngazi tunazopaswa kuzivuka na kushinda. Huu ni ushindi wa
lazima kwako, ambao ni lazima uushinde kama vile ulivyo mchezo wa mpira wa
miguu. Sote tunapaswa kushinda maisha katika ngazi mbalimbali kama vile, ngazi
ya makundi(Utoto), Robo fainali( Kijana),Nusu fainali(Mtu mzima) na fainali(
Uzee).
Ili
ushinde lazima uwe na kanuni, mbinu na mipango madhubuti ya kushinda. Kama vile
kilivyo kikosi cha mpira wa miguu, tumia kikosi cha mambo yafuatayo kushinda
katika maisha yako.
Kikosi
cha kwanza cha mambo yako kitakachokupeleka kwenye mafanikio kiwe hiki:-
1.
Kweli.
2.
Utu wema.
3.
Uvumilivu.
4.
Uwajibikaji.
5.
Imani.
6.
Msamaha.
7.
Elimu.
8.
Furaha.
9.
Umoja.
10.
Kiasi
11.
Upendo.
UKIWEKA JITIHADA NA KUVUMILIA UTASHINDA. |
Kikosi
cha ziada weka au fanya mambo haya:-
1.
Uadilifu.
2.
Haki na heshima.
3.
Uaminifu.
4.
Ndoto.
5.
Fadhili.
6.
Upole.
7.
Uelewa.
Tambua
wewe ndiye kiongozi na kocha wa maisha yako unatakiwa kuyasimamia na
kuhakikisha unafanya mambo hayo ili kufanikiwa.
Unapokuwa
na kikosi imara kama hicho ni rahisi kupambana na kikosi angamizi cha maisha
yako kama magonjwa, umaskini, kufeli, marafiki wabaya, tamaa na kujidharau. TAMBUA
USHINDI KWAKO NI LAZIMA kama utayaona maisha yako kwa mtazamo chanya.
Nikutakie
siku njema, yafanyie kazi mambo hayo na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamsika.
Makala hii imeandikwa na Noel Ngowi
wa Moshi- Tanzania. Kama una maoni au ushauri wasiliana na mwandishi wa makala
hii kwa email truesuccess89@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.