Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, November 2, 2015

Kama Ulikuwa Hujui, Huu Ndiyo Ukweli Halisi Wa Maisha Yako.

No comments :
Kama ulikuwa hujui, unazo siku za kuishi ambazo hazizidi elfu 30,000 kuanzia sasa, hiyo ikiwa ni sawa na miaka 82. Nikiwa na maana kuwa baada ya siku hizo kuisha karibu kila mtu aliyepo hapa duniani atakuwa ameshakufa ikiwemo hata na mtoto anayezaliwa leo. Kama itatokea binadamu atakuwa hai baada ya siku hizo basi huo utakuwa ni moja ya muujiza.
Kama ni hivyo umejipangaje kuishi kwenye siku hizo ambazo naweza nikasema ni chache. Lengo langu siyo kukukatisha tamaa ya maisha, ila nikukufikirisha na kujua namna utakavyoweza kujipanga na kuishi maisha yenye hamasa ya kukufanya ufanikiwe na siyo kujikalia na kubweteka.
Kitu cha kukumbuka hapa ambacho hutakiwi kusahau ni kwamba unazo siku chache sana za kuishi duniani. Je, unazitumiaje siku hizo katika maisha yako ya sasa. Je, umekuwa ukizitumia kwa manufaa au hasara? Kama umekuwa ukizitumia kwa hasara pole sana, utapoteza mengi na ni lazima utajuta.
Elewa, maisha yako ni kama dharura. Kama ni hivyo hutakiwi kuishi kiholela kama vile umenunua muda wote duniani. Inatakiwa tuishi kwa mipango ambayo unaamini ni  lazima ilete matokeo chanya na ya haraka kwa kipindi cha muda mfupi ulionao. Kama kuna mtu anakupotezea muda, achana naye. Ishi kwa kulinda muda ulionao.

FURAHIA MAISHA YAKO YA SASA.
Wakati ulionao ni sasa rafiki yangu. Fikiri jambo hili vizuri, mambo yaliyopita yamepita na hakuna kesho katika maisha yako hata ufanyaje. Kama ni hivyo, nafasi pekee uliyonayo kwenye maisha yako ni sasa. Mara nyingi umekuwa ukipanga sana kwamba nitafanya hiki siku nyingine au mwaka fulani yote hayo ni sawa, lakini hakuna kesho wakati ulionao ni sasa wa kufanya mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.
Acha kuendelea kujidanga kila siku kwa kujipa ahadi nyingi ambazo huzifikiki. Uhalisia wa maisha yako upo sasa. Kama kuna kitu unataka kukifanya kifanye leo, na wala usingoje kesho. Ikiwa utaendelea kungoja kesho hakuna ambacho utaweza kufanikisha kwenye maisha yako, sana sana utapoteza muda.
Zaidi kumbuka kifo, hakikusubiri wewe ukamilishe mipango au mambo yako fulani ili ufe, kifo kinakuja kwako muda na wakati wowote. Hivyo, hutakiwi kupoteza muda wako kwa lolote lile. Jipange kuishi maisha yako kwa furaha, amani na mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi ulionao.
Lakini hata hivyo hiyo haitoshi ni vyema kuishi maisha mazuri na wengine yatakayokupa furaha wewe na wao kwa siku ulizonazo. Utawazaje kuishi hivyo?
1. Tengeneza orodha yako.
Ni vyema ukajitengenezea orodha ya mambo yako unayotaka kuyatimza kabla hujafa. Iandike orodha hiyo vizuri na hakikisha unaifatilia kwa makini kuona kama uliyoandika unayafatilia na kuyatimiza.
2. Ishi sasa.
Hakuna kujidanganya ishi maisha yako sasa, usiwaze  sana juu ya kesho, halafu ukajikuta ni mtu wa kuahirisha tu. Kama ni kuboresha maisha yako, yaboreshe maisha yako sasa. Baada ya muda utakuwa mtu mwingine wa mafanikio makubwa tofauti na unavyofikiri.
3. Furahia mafaniko unayoyapata.
Kama kuna kitu umekifanisha ni vyema ukajifunza kukifurahia leo. Acha kusubiri hadi ufikie mafinikio makubwa ndio uanze kufurahia maisha yako. Kwa kadri utakavyozidi kufurahia mafanikio haya madogo, utajikuta ndivyo unapiga hatua kubwa ya mafanikio.
4. Weka alama za maisha yako.
Ni kitu gani ambacho ikiwa utakufa leo utakiacha kama kumbukumbu kubwa kwa kizazi cha leo na kesho. Kama kitu hicho kipo ni vyema ukaanza kukifanya kwa juhudi zote. Weka alama ili kizazi kijacho kijue wewe ulikuwa ni nani. Na uliacha kitu gani cha faida kwao.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kujifunza kila siku bila kuchoka.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,No comments :

Post a Comment