google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 18, 2016

Jinsi Ya Kutoka Katika Kifungo Cha Umaskini.

No comments :
Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra.
Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani  maana ya kifungo hicho.
''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo.
Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya.
Mara kadhaa maisha yetu yamekuwa ni yale yale kwa asilimia kubwa hii ni kutokana na uongo ambao kila mmoja aweka ndani ya nafsi yake, na uongo huo huo bila kujali kama una madhara makubwa katika maisha yetu ndio tumekuwa tukiusujudu kwa namna moja ama nyingine.

Unajua binadamu huongozwa kwa asilimia kubwa na mtazamo, mtazamo huo huo umegawanyika katika makundi mawili hapa nina maanisha mtazamo chanya na mtazamo hasi.
Na pia kama unaamini katika kujifunza kama mimi utagundua ya kwamba watu wengi ambao wamefanikiwa, watu hao kwa kiwango kikubwa huwa na mtazamo chanya sana. Lakini ni kwanini watu wengi ambao hatupo katika mtazamo chanya maisha yetu daima yapo vilevile ?
Hii ni kutokana tumezoea kufanya vitu kawaida  kwa njia ile moja huku tukiamini mafanikio yanakuja kwakufanya hivyo. Kufanya hivyo ni kuendelea kujidanganya.

Wito wangu kwako kama nilivyoanza hapo juu tuache kujidanganya wenyewe kama kweli tunataka mafanikio . Huenda tangu hapo juu hadi nilipofikia hujanielewa mtu huwa anajidanganyaje? Shusha pumzi kidogo huku na mimi nikizidi kutumia halmashauri yangu ya kichwa na mamlaka ya mkono kukujuza zaidi kama ifuatavyo.
Binadamu ni kiumbe wa kujifajiri sana hata sehemu isiyo farijika unashangaa wala usishange afisa mipango nakandamiza kwa kupaka wino mweusi kwa kusema huo ndio ukweli.

Tujikite japo kwa sekunde chache japo ni nyingi kimaana katika kuuleza yafuatayo, tuangalie wafanyabiashara wangapi ambao hutumia vinywa vyao katika kuzidanganya nafsi zao ambazo huwa zinaathiri mafanikio yao kwa ujumla?
Ukijaribu kumuuliza mtu ambaye anafanya biashara kwamba biashara yake inaendeleaje? Hata kama biashara hiyo haiendi vizuri kiasi gani atakwambia biashara ni nzuri, mmh huku ndiko kujifariji kwenyewe, kwanini tusiwe wakweli wa nafsi zetu.

Hebu taangalie wale ambao ni wasomi ambao bado wanatumia kalamu zao katika kupata ujuzi zaidi, na hao hao ukiwauliza unaendeleaje na masomo hata kama anafeli kwa kiasi gani katika masomo yake utamsikia msomi huyo huyo atakwambia naendelea vizuri, aah tunakwenda wapi kwa kujifajiri kwa vitu ambavyo vimekuwa havitusaidii hata chembe zaidi kuendelea kufeli?
Siku zote tuache kujifariji kwa kuwadandanya wengine ya kwamba tunaendelea vizuri wakati uhalisia wake hauko hivo. Kuendelea kujidanganya wenyewe. binafsi ni sawa na kutumia muwa kama fimbo ya kutembea kwani utafika mahali utautafuna tu.

Inawezekana pia licha kuendelea kuidanganya nafsi yako kwa namna moja ama nyingine, umekuwa ukiitumia fimbo hiyo hiyo kuwafariji wengine na huku kufanya hivyo unahisi kutamsaidia mtu huyo kumbe ukweli na uhalisia wake haupo hivyo hata chembe.
Kuna usemi fulani ulikuja kwa ndege unaseme ''the only truth shall set you free" kwa kibantu ukiwa na maana "ukweli pekee ndio utaokuweka huru" haina haja ya  kuinua macho angani kutafakari katika kujua msemo huo maana unajieleza kabisa na upo wazi kwa maana unaeleweka kabisa.

Kuanzia sasa badili mtazamo wako kwa kuwa na fikra chanya ambayo itakufanya ujisemee ukweli, wewe binafsi na watu wengine kwani kufanya hivi kutakupa uhuru mkubwa kwa jambo ambalo unalifanya na huku matokeo ya kimafanikio yakija kwa upande wako kwa asilimia kubwa zaidi. Pia tuwakumbuke wahenga ambao wazidi kutupa hamasa kwa kusema hatma ya maisha yako unayo wewe mwenyewe.

Ni matumaini yangu makubwa unakwenda kubadilikia kuanzia sasa na mafanikio makubwa yatakwenda kuwa ukweli endapo utakwenda kuchukua hatua madhubuti zenye matokeo chanya.

Ndimi Mjenzi wa  Taifa kupitia Uandishi (MTU); Afisa mipango Benson Chonya.

Blogu; 
www.dirayamafanikio.blogspot.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.