google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 14, 2016

Sababu Zinazofanya Wafanyabiashara Wadogo Kushindwa Kufanikiwa.

No comments :
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamimiko mengi iwe kwenye vyombo vya habari au mtaani hasa kwa wafanyabiashara wadogo. Malalamiko hayo yamekuwa yakihusisha mambo mengi, lakini mojawapo likiwa la wafanyabiashara hawa wadogo kushindwa kufanya vizuri au kufanikiwa sana kwenye biashara zao.
Hoja zao mara nyingi wamekuwa wakizielekeza kwenye lawama kulaumu pengine Serikali au kundi fulani la watu ambalo wao wanaona kama linawabana katika utendaji na hadi wao kushindwa kufanikiwa. Hoja hizi kwa siku ya leo sitaki kuzijadili hapa kama ni za kweli au la!
Badala yake makala haya itakuonyesha mambo mengine kadhaa ya msingi yanayopelekea wafanyabishara wadogo kushindwa kufanikiwa. Mambo haya kwa sehemu yamekuwa kikwazo na sababu kubwa inayopelekea wafanyabishara wengi wadogo kushindwa kupiga hatua na kujikuta wapo palepale.
Hebu kwa pamoja tuangazie nukta kadhaa zitakazotusaidia kujua ni kwa nini wafanyabishara wengi wadogo wanashindwa kufanikiwa kwa viwango vya juu.
1. Ukosefu wa mitaji ya kutosha.
Wafanyabishara walio wengi wadogo, wakati mwingine wanashindwa kufanikiwa sana kwa sababu ya mitaji midogo waliyonayo. Mitaji hiyo midogo inakuwa kikwazo cha mafanikio kutokana na sababu mbalimbali kama tutakavyokwenda kuziona.
Kwanza, kwa sababu ya mitaji midogo  biashara inakua inashindwa kwenda kwa kasi kama inavyotakiwa iwe, ili kukabiliana na ushindani mkubwa uliopo sokoni. Hivyo kwa sababu hiyo hupelekea mafanikio kutokuonekana kwa wafanyabiashara hawa wadogo kwa haraka.

Tengeneza usimamizi mzuri kwenye biashara yako, utafanikiwa.
Pili, kwa sababu ya mitaji midogo biashara nyingi za wafanyabiashara wadogo zinakuwa zinakabiliwa na changamoto mbali kama kodi ya pango, kodi ya mapato na hata matumizi binafsi.
Kwa changamoto kama hizi kwa wafanyabiashara wengi walio wadogo huwa si rahisi sana kukabiliana nazo kwa uhakika, hivyo kupelekea wao kushindwa kufanikiwa kwa viwango vya juu. 
Naamini katika suala zima la ukosefu wa mitaji umeshawahi kulisikia sana likilalamikiwa na wafanyabiashara wadogo  walio wengi. Na hii ni moja ya sababu inayowazuia kufanikiwa kwa viwango vya juu.
Nini kifanyanyike?
Yapo mengi yanaweza kufanyika ili kukuza mitaji kwa wafanyabiasha wadogo. Mojawapo ni kujiwekea akiba hata kwa muda mrefu ambayo baadae itatumika kama mtaji wa kuanzia biashara kubwa.
Pia wafanyabiashara hawa wanaweza kuungana na kuanzisha mfuko wa pamoja kama mfumo wa SACCOS au VICOBA ambao utawasaidia kwa urahisi kuweza kukopa pesa zitakazowasaidia katika suala zima la mitaji.
Hiyo haitoshi kitu kingine kinachoweza kufanyika ni kwa wao wafanyabiashara kuwa waangalifu na makini na kodi wanazolipa pamoja na suala zima la matumizi ili kukuza biashara.
2. Usimamizi mbovu.
Pia biashara nyingi ndogo zinashindwa kufanya vizuri kwa sababu ya kuwa na usimamizi mbovu. Mara nyingi wafanyabiashara wadogo huwa wanakuwa na usimamizi mbovu katika maeneo mengi kama mauzo, manunuzi, uzalishaji wa bidhaa duni na hata jinsi ya kuwajali wateja.
Kama hujanielewa vizuri katika hili nitakupa mfano. Utakuta mtu ana biashara yake ya aina fulani, lakini biashara hiyo kamuachia mtu mwingine  anayeiendesha karibu muda wote na wala hakuna ufatiliaji ule wa karibu. Kwa usimamizi kama huo inakuwa si rahisi sana kuweza kufanikiwa.
Hali kama hizi za usimamizi mbovu kwa maeneo niliyoyataja zipo sana kwenye biashara nyingi mtaani. Jaribu kutembelea mtaani au sokoni chunguza kile wanachokifanya baadhi ya wafanyabishara wadogo, kuna wakati unaweza usiamini kile wanachokifanya lakini ndio ukweli.
Kutokufanikiwa kwa biashara zao naweza sema ni kama kifo cha kujitakia. Mambo mengi yanafanywa kimazoea sana hasa jambo kama kumuchukulia mteja mtu wa kawaida kabisa na kushindwa kumjali.
Kama unafikiri natania katika hili, tembelea baadhi ya maeneo hapa nchini na chunguza juu ya hilo, utashangaa jinsi wateja wanavyochuliwa na baadhi ya wafanyabiashara. Hii ni hali halisi iliyopo katika jamii yetu na ndio chanzo kikubwa kimojawapo kinachopelekea baadhi ya wafanyabiashara wadogo kushindwa kufanikiwa kwa viwango vya juu.
Nini kifanyike?
Kitu cha kufanya hapa, ni lazima kwa mfanyabiashara yoyote kuwa makini na eneo la usimamizi wa biashara, hiyo itasaidia sana kukuza biashara yako wakati wote na kujenga mafanikio makubwa. Bila kufanya hivyo itasumbua sana biashara yako kukua.
Kwa leo niishie hapa naomba tukutane tena wiki ijayo na siku kama ya leo katika sehemu ya pili ya makala haya, kuangalia sababu zingine zinazopelekea wafanyabiashara wadogo kushindwa kufanikiwa.
Nikutakie siku njema na mafanikio mema, ila endelea kujifunza na kuwekeza maarifa kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki,

Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,




No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.