google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 15, 2016

Kwanini Hutakiwi Kuwa Na Watu Hasi Kwenye Maisha Yako?

No comments :
Moja ya msisitizo mkubwa ambao mara nyingi tumekuwa tukitoa kama DIRA YA MAFANIKIO ni kwamba ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe chanya wakati wote. Hilo tumekuwa tukiliongelea sana kupitia makala mbalimbali tunazozitoa hapa.
Tumekuwa tukiongea hilo na kuendelea kusisitiza uchanya huo hautakiwi kuwa nao wewe tu bali mpaka watu wanaokuzunguka. Watu hawa wanaokuzunguka ni pamoja na marafiki, ndugu na hata jamaa zako wa karibu sana.
Kitu pengine unachotaka kujiuliza, kwa nini ni muhimu sana  kuwa na watu chanya katika maisha yako. Kama hilo ndilo swali lako majibu yake unakwenda kuyapata kwa kusoma makala haya, na utajua ukweli kwa nini hutakiwi kuwa na watu hasi kwenye maisha yako.
1. Utakuwa kama wao.
Kiuhalisia, wewe ni matokeo ya watu watano wanaokuzunguka. Kama unazungukwa na watu watano ambao ni wadanganyifu upo uwezekano mkubwa ukawa mdanganyifu pia. Kama unazungukwa na watu watano maskini ni rahisi pia na wewe kuendelea kuwa maskini.

Watu hasi ni sumu kubwa ya mafanikio yako.
Kwa kundi lolote unalozungukwa nalo upo uwezakano wa kuwa kama wao. Kama ni hivyo ni hatari sana kuwa na watu hasi, haijalishi uhusiano wenu ni wa kindugu au kirafiki. Kwa kitendo cha kuwa nao, elewa ni lazima na ni rahisi sana kufanana na wao utake au usitake.
2. Ujasiri wako unapungua.
Unapokuwa na watu hasi ni wazi lazima ujasiri wako utapungua. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu ni rahisi kusikia maneno kama hutaweza kuwa tajiri, huna bahati au una mikosi sana huwezi kufanikiwa na maneno mengine mengi yanayofanana na haya ili mradi kukukatisha tamaa.
Unapokuwa unatumia muda wako mwingi na watu hawa, kama nilivyosema watapunguza ujasiri wako. Na kwa bahati mbaya ukikosa ujasiri huwezi kufanikiwa tena. Hivyo, lazima uwe makini na watu hasi, vinginevyo kutokufanikiwa kwako kutakuwa nje nje.
3. Huwezi kujifunza kitu kwa watu hasi.
Ikiwa watu wako wa karibu unaoshirikiana nao ni watu wa kulaumu, kukaa kuongelea watu wengine na wala hawajitumi, je, unafikiri unaweza kujifunza kitu kwao cha kuweza kukusaidia kufanikiwa? Hata kwa akili ya kawaida hapo huwezi kujifunza kitu sana sana utakatishwa tamaa kila siku.
Ifahamike kwamba watu wote ambao wanafikiri hasi, hawafikiri makubwa huwa wana nguvu fulani ya kukushawishi uwaze kama wao kwa namna ya hasi hasi.  Kwa namna yoyote ile unatakiwa kuwa makini nao na ndio maana ni muhimu kukaa nao mbali, vinginevyo watakukwamisha.
4. Watakupotezea ndoto zako.
Pia sifa nyingine ya watu hasi ni rahisi sana kukupotezea ndoto na malengo yako. Kwa jinsi utakavyozidi kukaa nao utagundua kwamba mara kwa mara ni watu wa kutokuongelea malengo ya kimaisha zaidi ya porojo za hapa na pale.
Sasa unapokuwa na watu hawa si rahisi kufanikiwa. Ikiwa unazipenda ndoto zako na kuziona zikitimia, acha mara moja kuendelea kuwa na watu hasi. Watu hawa watakupotezea mengi sana katika maisha yako wakati mwingine hata bila wewe kujijua.
Kumbuka ni muhimu sana kuwakwepa watu hasi katika maisha yako kwa sababu unapokuwa nao ni rahisi kuwa kama wao, watakufanya ushindwe kujiamini, hutaweza kujifunza kitu kutoka kwao na zaidi watakupotezea ndoto zako za maisha.
Chukua hatua sitahiki za kubadili maisha yako na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.