google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 6, 2016

Sababu Zinazokufanya Ushindwe Kwa Kile Unachokifanya.

No comments :
Kuna wakati katika maisha yetu hali ya kushindwa, huwa inajitokeza kwa namna moja au nyingine katika mambo tunayoyafanya. Kimsingi, kushindwa huko mara nyingi pia huwa hakutokei kwa bahati mbaya.
Kiuhalisia, huwa yapo mambo mengi yanayochangia kushindwa huko. Je, binafsi ulishawahi kujiuliza kwa nini kushindwa kunakuwa kunajitokeza katika maisha yako kwa wakati fulani?
Hebu kwa pamoja tuangazie nukta kadhaa zitakazotusaidia kukumbusha kwa nini kushindwa wakati mwingine kunajitokeza katika maisha yetu.
1. Mitazamo tuliyonayo.
Mara nyingi mitazamo tuliyonayo ina uwezo wa kukufanya ukafanikiwa au ukashindwa kwa kile unachokifanya. Mitazamo tuliyonayo ina nguvu kubwa ya kubadili maisha yetu. Na mitazamo hii kuna wakati ina waangusha wengi kwenye safari ya mafanikio bila kujua.
Kwa mfano utakuta mtu ana karibu kila kitu, lakini unashangaa ameshindwa kwenye jambo fulani. Ukichunguza chanzo ni mitazamo aliyobeba. Unapokuwa unajibebesha mitazamo hasi, mitazamo ya kuona huwezi kwa kile unachokifanya ni lazima utashindwa.

Mitazamo uliyonayo inauwezo wa kukufanya ukashindwa.
2. Kukosa uvumilivu.
Wengi wanashindwa katika maisha na kwa yale mambo wanayofanya kwa sababu tu ya kukosa uvumilivu. Watu hawa hawashindwi si kwa sababu hawana maarifa au uwezo bali ni kwa sababu ya kukosa uvumulivu wa kuwasaidia kuendelea mbele.
Kwa mfano watu hawa wanaoshindwa, wanapokutana na changamoto hata kama ni ndogo inakuwa ni rahisi sana kwao kukata tamaa na kuona kila kitu kimekwisha. Hivyo, unapokuwa unakosa uvumilivu kwa kile unachokifanya ni rahisi na lazima utashindwa.
3. Kutokuwa tayari kujifunza.
Tatizo kubwa walilonalo watanzania walio wengi ni kule kutopenda kujifunza. Kutokana na tatizo hilo hupelekea wengi sana kushindwa kwa yale mambo wanayoyafanya. Inawezekana hata wewe unashindwa kufanikiwa kwa viwango vya juu kwa sababu hauko tayari kujifunza.
Kama unafikiri nakuonea hebu jiulize, mwaka huu umesoma vitabu vingapi? Utaona idadi ya vitabu ulivyosoma ni vichache au hakuna kabisa. Kwa sababu hiyo, huwezi kufanikiwa kama huko tayari kujifunza. Ni lazima uwe na maarifa ya kutosha kukusaidia kufanikiwa.
4. Kurudia makosa yale yale.
Kuna wakati unaweza ukajikuta unashindwa kwenye malengo yako, kwa sababu tu ya kurudia makosa yale yale unayofanya kila wakati. Inapotokea umefanya kosa, halafu kosa hilo ukalirudia tena na tena ni wazi kushindwa kwako itakuwa ni rahisi sana.
Kitu cha kutambua moja ya kitu kikubwa cha kuepuka ili usiendeleze kushindwa, acha kurudia makosa yako mara kwa mara. Ukichunguza wengi makosa wanayoyafanya na kuyarudia tena yamewagharimu na kupelekea wao kushindwa.
5. Kukosa nidhamu binafsi.
Nidhamu binafsi ni nguzo kubwa ya mafanikio makubwa. Unapokosa nidhamu hii kwa kawaida kushindwa kwa kile unachokifanya hautaweza kukwepa. Unajua ni kwa nini? Ni kwa sababu utafanya mambo mengi hovyo hovyo na kukuharibia ndoto zako.
Unapokuwa na nidhamu binafsi inakujengea uwezo wa kujituma na kujitoa kweli kweli. Lakini unapoikosa ni rahisi kwako kutumia pesa hovyo, au kufanya mambo yasiyokusaidia kufikia ndoto hizo ulizonazo. Kwa namna yoyote ile ukiona huna nidhamu binafsi, elewa hutaweza kufanikiwa.
Nimalizie makala haya kwa kusema, mitazamo uliyonayo, ukosefu wa nidhamu, kukosa kujifunza mara kwa mara na kushindwa kuvumilia, ni moja ya mambo yanayoweza kukufanya ukashindwa kufanikiwa kwa jambo unalolifanya.
Chukua hatua za kujifunza zaidi, lakini usiishie hapo tu endelea kuwashirikisha wengine waweze kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika kusaka mafanikio ya kweli,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.