google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 21, 2020

Ikiwa Unapata Matokeo Usiyoyataka, Acha Kujiona Hivi.

No comments :
Ikiwa unapata matokeo usiyoyataka hasa kwa kile kitu unachokifanya, acha kujiona mnyonge na kukata tamaa, endelea kuweka juhudi. Kwa kuendelea kuweka juhudi huko, matokeo unayoyataka utayapata.
Ikiwa unapitia kwenye changamoto nyingi za kimaisha pia acha kukata tamaa, endelea kuweka juhudi upo wakati ambapo utazivuka hizo changamoto hizo na kuwa huru, huwezi kubaki kwenye changamoto hizo milele.
Ikiwa huridhiki kabisa na mwenendo wa maisha yako na kujiona kila wakati kama mtu ambaye umepoteza, pia usikate tamaa, endelea kuweka juhudi. Kwa kuendelea kuweka juhudi, itafika wakati utaona mwelekeo wa maisha yako.
Kwa kila hatua unayochukua kwenye maisha yako hata ikiwa ndogo sana, inaleta mabadiliko kwenye maisha yako. Usijadanganye eti hatua hii ni ndogo haiwezi kuleta mabadiliko, kila hatua inaleta mabadiliko kwenye maisha yako hata kama huyaoni.



Angalia ulikotoka kwenye maisha, sasa kwa nini ukate tamaa na wakati sasa hivi upo mbali sana? Dawa si kukata tamaa ni kuweka juhudi tena. Usikubali ukakatishwa tamaa na chochote, weka juhudi utafanikiwa.
Hata upate matokeo mabaya vipi ambayo unaona hayakuridhishi kabisa endelea kuweka juhudi, kwani lazima juhudi zako zitaleta matunda. Matokeo mabaya unayoyaona, ni ya muda tu, lakini una uwezo wa kuyabadili sana.
Hakuna mtu katika dunia hii ambaye ameweka juhudi endelevu, halafu zikaja kumwangusha, mtu huyo hayupo. Kila anayeweka juhudi endelevu, mwisho wake unakuwa mzuri na anavuna anachokitaka.
Hivyo, hata ushindwe mara nyingi vipi, endelea kufanya mabadiliko kwenye maisha yako, kwani upo wakati mabadiliko hayo utayaona kwa wazi kabisa, hata kama kwa sasa  huyaoni mabadiliko hayo kwa nje.
Kila hatua unayoichukua, kumbuka inakusogeza karibu kabisa na mafanikio yako. Hakuna hatua utakayochukua na kuifanyia kazi halafu ikaja kukuangusha, hata ukianguka chukua kama fundisho. Chukua hatua sahihi, ili ufikie mafanikio yako.

Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.