google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 15, 2020

Ili Kujenga Mafanikio Makubwa, Achana Na tabia Hii…

No comments :



Tabia moja ambayo itakukwamisha sana na haitakusaidia kufanikiwa kama utakuwa nayo na kuiendeleza ni ile tabia ya kuamua kuwa mtu wa kushangaa katika maisha. Wapo watu ambao tabia zao ni kushangaa tu karibu kitu.
Kwa mfano, Utakuta wao ni watu wa kushangaa na kuhamasika sana na miradi wanayofanya watu wengine, ukija upande wao hakuna hata kitu kimoja wanachofanya au hawachukui hatua kabisa.
Pia utakuta ni watu wa kuingia kundi moja, wanashangaa kinachoendelea humo na kutoka na kuingia tena kundi lingine wanashangaa wee na kutoka tena, pia bila kuchukua hatua.
Dunia ya sasa hivi ni ya mwendo kasi, watoto wa mtaani wanakwambia ‘hutakiwi kuuza sura’, fanya kazi. Kama kuna fursa hata kama ni ndogo, itumie ikusaidie kufanikiwa na acha kubaki tu kuwa mtu wa kushangaa.  Kama ni kujifunza, jifunze kweli.
Uzuri au ubaya wa maisha hakuna ubabaishaji, ukileta ubabaishaji wa aina yoyote ile, utaumbuka tu na ni lazima utajibiwa na maisha kama vile wewe unavyobabaisha. Badilika rafiki na achana na biashara ya kushangaa, kuwa mtendaji na aamua kufanya kazi.

Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.