google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 20, 2020

Jenga Utaratibu Wa Kujiuliza Maswali Haya, Utafanikiwa.

No comments :
Katika maisha yako, anza kujenga utaratibu mpya wa kujiuliza maswali kwa mambo unayoyataka yawe katika maisha yako. Kwa mfano, unaweza ukawa unajiuliza nina fanyaje ili niingize kipato kikubwa zaidi au ninafanyaje ili niweze kutoka hapa nilipo.
Akili kama akili imeumbwa ili ikusaidie kutafuta majibu kwa yale mambo magumu. Sasa kama upo upo huisumbui akili yako ikusaidie kutatua changamoto zako, aisee uwe na uhakika utabaki sana hapo ulipo.
Kumbuka kila wakati akili ya binadamu, inafanya kazi kwa kuuliza maswali na kujijibu. Chochote ambacho unajiuliza sana kwenye akili yako haijalishi ni kibaya au kizuri, ni lazima kitu hicho utaweza kukipata.
Acha kukukosea katika hili, jiulize maswali magumu yatakayosaidia kuboresha maisha yako. Ukiisumbua akili yako, utapata hicho unachokihitaji na utajenga msingi wa maisha bora sana kwako na kizazi chako cha baadae.



Ukiilaza akili yako, na ujue pia kuna mambo mengi sana utayalaza na hutafika mbali kimafanikio. Kwa hiyo jukumu lako ni kila siku kuisumbua akili yako ikupe majibu ya kitu gani unachokitaka maishani.
Kwa kadri unavyoisumbua akili yako, utakuta majibu na yale mambo unayoyataka unayapata. Acha kulaza damu waza, tumia kichwa chako kufikiri na sio kutumia kichwa chako kukiburudisha tu na kutulia.
Nikwambie, hutaweza kufa eti kwa sababu ya kuwaza, sumbua akili yako, waza tena na tena mpaka upate majibu sahihi ya nini unachokitaka kwenye maisha yako. Waliofanikiwa elewa, wanasumbua akili zao na sio watu wa kulala tu.
Akili inayojishughulisha na kutafuta majibu ya changamoto ndio inayofanikiwa. Ikiwa wewe unajidanganya kwamba mafanikio yako yatakuja yenyewe, nakwambia unajidanganya na hautaweza kufika popote kwa sababu unajidanganya.
Usikubali kushindwa kwa kujiambia ‘oooh mimi siwezi,’ nani aliyekwambia huwezi? Akili yako umepewa ina nguvu na majibu mengi ya changamoto zako. Ikiwa kweli umewaza na umefika mwisho, nikwambie Mungu ataonyesha njia kwako.
Kama haujishughulishi na kuwaza, kutafuta suluhu ya changamoto zako na ukaamua kutafuta msaada wa Mungu, kwako ni lazima utakwama. Umiza akili yako, jenga uataratibu wa kujiuliza maswali kwa yale unayotaka na utafanikiwa.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.