google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 11, 2020

Kitu Hiki Kitaboresha Maisha Yako Sana, Ikiwa Utakizingatia.

No comments :
Kati ya kitu ambacho kinaweza kikaboresha maisha yako na kuyafanya yakawa bora ni mawazo yanayoboreshwa/ ideas for improvement. Kila wakati na kila siku unatakiwa kujifunza kuboresha chochote kile unachokifanya ili kikupe mafanikio zaidi mengine.
Kitu chochote kile kinaweza kikaboreshwa, na kuleleta matokeo au mafanikio makubwa. Unaweza ukaboresha bidhaa yako, unaweza ukaboresha huduma na unaweza ukaboresha kitu chochote ambacho utakichagua.
Mawazo yaliyoboreshwa, yana uwezo wa kukufanya ukawa tajiri na ukafanikiwa kwa viwango vya juu. Mawazo yaliyoboreshwa ni moja ya bidhaa muhimu sana, ambayo wewe unatakiwa uitoe kila siku kwenye maisha yako.

Kumbuka mawazo ya kuboresha kitu chochote kwenye kampuni kubwa, huwa yanatoka kwa watu wa kawaida na ambao wako kama wewe. Hivyo boresha kile ambacho unakiona ni cha muhimu kwako ili kikupe mafanikio.
Kama usipoboresha kile unachokifanya na uelewe hutapata mafanikio makubwa na utaishia kupata mafanikio ya kati au ya kawaida kabisa. Jitahidi sana kuboresha kile unachokifanya ili uweze kufanikiwa.
Kila siku waza, ni nini ufanye ili uweze kuboresha kitu hicho. Ukimudu kuboresha kitu hicho utafanikiwa. Mawazo yaliyoboreshwa ni faida kubwa sana ya mafanikio yako leo na hata kwa baadae. Anza leo kuboresha hicho unachokifanya ili ufanikiwe.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.

Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 

Nikutakie kila la kheri,

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.