google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 17, 2020

Haya Ndiyo Mahitaji Muhimu Kwako Yatakayokupa Maisha Ya Mafanikio.

No comments :

Yapo mahitaji matatu ambayo ni ya lazima kwako ili kuishi vizuri na kukujengea msingi mkubwa wa mafanikio. Haya ni mahitaji ambayo kwa namna yoyote ile huwezi kuyakwepa, ni lazima uwe nayo na uyatawa
Kwanza, mahitaji ya mwili, hapa ni lazima mwili wako unahitaji kuvishwa nguo nzuri na kula chakula kizuri ili kujenga afya. Kama huli vizuri ni rahisi sana na mambo mengine pia kwenda hovyo.

Pili, mahitaji ya akili, ili akili yako ifanye kazi vizuri ni lazima pia kuizoesha kuilisha vizuri kwa kujifunza. Hata kama sio utamaduni wako kujifunza, hebu anza kidogo kidogo. Jifunze kusoma vitabu vya kukujenga na sio kukubomoa.

Tatu, mahitaji ya kiroho, ni lazima sana pia kukua kiroho ili kuleta usawa katika maeneo yote matatu. Unahitaji kujifunza neno la Mungu na kutambua misingi ya kiroho. Kumbuka sisi sio miili tu ni zaidi ya hapo.

Maisha yako yanakuwa sawa na maana ikiwa maeneo yote hayo matatu yatakuwa na uwiano ulio sawa. Hakuna mwenye mafanikio makubwa na akawa na furaha kama eneo moja hapo likawa lina upungufu mkubwa.

Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.

Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.