google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 4, 2020

Mambo Ya Kufanya Ili Kuwa Mshindi Katika Safari Yako Ya Ujasiriamali.

No comments :
Zipo hadithi nyingi sana za watu, ambazo zinaeleza ili kufanikiwa katika  safari ya ujasiriamali unatakiwa kufanya hili au lile. Na kwa bahati  nzuri au mbaya hadithi hizi ziko tofauti baina ya mtu na mtu.
Pasipo kujali ni nini kinachozungumzwa sana katika safari ya kuelekea kwenye ujasiriamali, hapa kupitia makala haya nataka nikushurikishe, mambo ya msingi ya kufanya ili kuwa mshindi katika safari ya mafanikio.
Ni mambo yapi ambayo unatakiwa uyafanye ili uweze kuwa mshindi katika safari yako ya mafanikio? Sasa karibu ili uweze kujifunza mambo hayo;-
1. Tengeneza fursa.
Inaweza kuwa ni kosa kubwa kwako kama kila wakati unasubiri fursa ikufate pale na badala ya kuitengeneza. Kama unafanya hivyo yaani kusubiri fursa, nakuhakikishia utakuwa unachelewa sana kufikia mafanikio yako.
Kama kuna kitu unatakiwa kukifanya, hebu kifanye na acha kusubiri subiri hadi mambo yawe sawa sana. Ukizidi kusubiri unaweza ukajikuta umechelewa kabisa. Kama ipo fursa ya kazi ambayo hata hailipi sana, hebu anza kuifanya hiyo kazi, itakulipa baadae.

2. Endelea kujifunza.
Wajasiriamali wa kweli ni watu wa kujifunza kila siku, nawe pia kama unahitaji kuwa mshindi katika safari ya ujasiriamali, unatakiwa tu kwa wewe kuamua kujifunza haswa na tena kila siku bila hata ya kupoteza muda.
Kwa chochote kile unachokifanya, kitafutie maarifa zaidi na hakikisha unakijua vizuri ili kuweza kutimiza ndoto zako za kufika kwenye ujasiriamali wenye mafanikio. Jifunze, jifunze, na acha kusimama kujifunza kila siku jifunze na utafika mbali kimafanikio.
3. Rekebisha makosa yako mara kwa mara.
Lipo eneo ambalo unatakiwa kufika kimafanikio, sasa ili kufika eneo hilo kimafanikio, inabidi ukubali ukikosea kurekebisha makosa yako. Acha kujiachia tu na kusahau kurekesbisha makosa yako, kwani ukishindwa hivyo utakwama.
Watu wote ambao wanarekesbisha makosa yao, ni watu ambao wanaweza kufanikiwa na kufika mbali sana kimafanikio. Unaweza ukawa ni miongoni mwa watu hao, kubali kurekebisaha makosa yako ili uwe mshindi.
4. Jifunze kutokana na mazingira.
Ni muhimu na na ni msingi kujifunza kutona na mazingira yanayo kuzunguka. Jaribu kuchunguza eneo ulilopo lina fursa gani na watu wa eneo hilo wanahitaji nini, kwa kujua hivyo itakuwa ni nia sahihi kwako ya kujifunza kutokana na mazingira.
Kama ikitokea utashindwa kujifunza kutokana na mazingira basi elewa utakwama sana na utashindwa kufanikiwa. Magfanikio ya kweli yanakuja na kujengwa kama utajua namna ya wewe kujifunza kutoka na na mazingira yako na kuchukua hatua.
5. Kuwa na mwendelezo wa kufanya.
Ikiwa unataka kuwa mshindi katika safari yako ya ujasiriamli, hakikisha una mwendelezo wa kufanya. Usiwe mtu wa kuishia kati. Kama kuna kitu umeamua kukifanya, fanya ufanyavyo ila mwendelezo huo unatakiwa kuwa nao.
Wengi si wazuri sana katika kuwa na mwendelezo ni watu ambao akianza jambo hilo leo, ni rahisi tu kumkuta mtu huyo jambo hilo kesha achana nalo na hana habari. Ukijijengea nidhamu ya kuwa na mwendelezo, sio siri utafanikiwa.
Ukizingatia na kuyafatilia mambo hayo na ukayachukulia hatua, yatakusaidia wewe kuweza kuwa mshindi katika safari yako ya ujasiriamali.

 Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.