google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 22, 2020

Kama Utatumia Nguvu Hizi, Ni Lazima Ufanikiwe.

No comments :
Binadamu tumeumbiwa nguvu za aina nne ambazo tunatakiwa kuzitumia kwa ufasaha ili tuweze kupata mafanikio makubwa. Kama utaweza kumudu kuzitumia nguvu hizo vizuri, ni wazi utafanikiwa na hakuna ubishi.
Watu wengi hawafanikiwi kwa sababu, kwa namna moja au nyingine hawatumii nguvu hizo kiufasaha au kuna baadhi ya nguvu hawazitumii kabisa. Katika Makala haya nataka kukuonyesha nguvu hizo, ikiwa utazitumia, utafanikiwa.
1. Nguvu ya mwili (Physical energy).
Ili kufanikiwa, unahitaji mwili wenye afya, unahitaji mwili wenye nguvu ili ukusaidie kufanya kazi zako. Kama utakuwa una mwili ambao hauna afya, sahau mafanikio. Ndio maana tunasema, afya ndio kitu cha kwanza kwenye maisha yako.
Kwa hiyo kila siku, kabla hujafanya kazi zako, angalia kazi ambazo zinahitaji matumizi makubwa ya nguvu za mwili kabla hujachoka. Kisha, anza na kazi hizo ili ukichoka utafanya kazi laini, lakini ukumbuke nguvu ya mwili ni muhimu sana.



2. Nguvu ya ubora (Emotional energy).
Hapo ulipo ndani mwako una nguvu fulani ya ubora ambayo imejificha. Ili ubora huo uweze kuonekana kwa nje unatakiwa kutumia kwa namna moja au nyingine. Kama utaulalia ubora wako basi tu elewa utakwama.
Unatakiwa kuujua na kuutumia ubora wako kwa namna yoyote ile. Usijadanye kwamba wewe si bora, hapana, ndani yako una ubora wa aina fulani ambao unatakiwa kutumia kila siku ili ukuletee mafanikio na maajabu makubwa.
3. Nguvu ya  akili (Mental energy).
Pia akili ni nguvu mojawapo ambayo umeumbiwa ili tuweze kufanikiwa. Kama umeweza kusoma hapa, basi akili zako ziko sawa na unatakiwa ujue jinsi ya kutumia nguvu hiyo ya akili ili kujenga mafanikio makubwa.
Watu unawaona wana mafanikio, wanatumia akili zao ili kuweza kufanikiwa. Na wewe unaweza ukatumia akili zako kuweza kufanikiwa kwa viwango vya juu sana. Sugua akili yako na ujue ni nini cha kufanya, na nini ambacho hutakiwi kufanya.
 4. Nguvu ya kiroho (Spritual energy).
Hii ni pia ni nguvu muhimu kwa sababu, inasaidia kutuongoza kujua ni lipi jema na lipi ambalo sio jema. Kwa kujua hivyo inasaidia sana kututengenezea mafanikio makubwa maisha mwetu kila wakati.
Hivyo kwa kufika hapo, bila shaka umezijua nguvu nne, ambazo nguvu hizo kila binadamu anatakiwa kuzitumia ili kufanikiwa. Kwa kumudu kutumia nguvu hizo mafanikio kwako yatakuwa jambo la lazima na si kuuliza tena.

Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.