google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 14, 2020

Usikubali Hali Hii, Ikakuzuia Kufanikiwa.

No comments :
Kwa hali yoyote ile ambayo inatokea nje ya wewe haina mchango mkubwa sana wa kuweza kukukwamisha au kukufanya ushindwe kufikia mafanikio yako. Kitu ambacho kitakufanya ushindwe kufanikiwa ni ile hali inayotokea ndani mwako tu.
Hali hiyo inayotokea ndani mwako, ndiyo ina nguvu kubwa sana ya kubadillisha maisha yako na kuwa ya mafanikio kabisa. Hebu jiulize kila unapowaza mafanikio, ndani mwako unajionaje? Unajiona ni kwamba utafanikiwa au utashindwa?
Nikuulize ni kipi unachokiona ndani mwako kila unapofikiria mafanikio? Kama unaona kuna kushindwa, nakwambia utashindwa tu, na kama unaona kuna ushindi mbele yako, pia nakwambia ni lazima utafanikiwa.
Haijalishi watu wanasemaje au watasema nini juu yako, hata watu dunia nzima waseme kwamba utafanikiwa, lakini kama ndani yako huoni hivyo ni wazi huwezi kufanikiwa, kwa sababu mafanikio hayo huyaoni ndani mwako.

Pia hata itokee dunia nzima iseme kwamba wewe ni wa kushindwa, lakini ikiwa ndani yako unajiona wewe ni mtu wa mafanikio, utafanikiwa. Hali yoyote inayotokea ndani mwako ndio inayokufanya ufanikiwe au ushindwe.
Kitu kikubwa hapa, jifunze kutokulaumu hali yoyote ile, inayotokea nje katika maisha yako kwamba ndio imekukwamisha. Anayejizuia na kujikwamisha sio mwingine bali ni wewe mwenyewe na hali hasi nyingi ulizozibeba.
Kuanzia leo amua kujenga hali bora ndani mwako itakayokupa mafanikio makubwa. Amua kujijengea mitazamo sahihi, amua kuona hali halisi ya mafanikio inatokea ndani yako na kukupa mwanga wa mafanikio.
Ukiwa na hali nzuri yenye mtazamo sahihi, ni wazi nakwambia hiyo ni lazima ufanikiwe. Unatakiwa ujue hali yoyote ya nje, haina uwezo wa kukuzuia wewe kuweza kufanikiwa bali ni hali ya ndani peke yake ndio ina uwezo wa kukuzuia kufanikiwa.
Ni wapi unapokwama, ni kwa nini hufanikiwi? Acha kulaumu hali au mazingira yoyote ya nje, unatakiwa ujilaumu wewe mwenyewe kwamba ndio umeshindwa kufanikiwa. Ukiuona ukweli huo nakwambia utafanikiwa kweli.
Kumbuka, hali yoyote ya nje, haina uwezo wa kukuzuia wewe kufanikiwa, zaidi hali ya ndani mwako ndio ina uwezo wa kukufanya wewe ukashindwa kufanikiwa au kufikia ndoto zako unazozitaka. Usikubali kukwamishwa na hali yoyote ile ya nje kwako.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
 Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.