google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 6, 2020

Njia Sahihi Itakayokufanya Wewe Kufikia Mafanikio Makubwa.

No comments :
Moja ya njia sahihi itakayokufanya wewe kufikia mafanikio makubwa ni kwa wewe kukubali kutumika kwa nguvu zote/ be more useful. Usikubali utumike kidogo kidogo, kama kuna kazi unaifanya kubali kutumika kwa asilimia zote.
Unaweza kutumika kwa mwajiri wako au unaweza kutumika kwa kazi zako binafsi, lakini lililo kubwa ni kwa wewe kukubali kutumika kwa nguvu zote ili ujenge mafanikio. Usipokubali kutumika, ukipata mafanikio kidogo usishangae.
Ninapozungumzia kutumika nina maana ya wewe kujituma. Unatakiwa kujituma sana na bila kukwama au kuishia kati.  Watu wote wanaojituma na kuuamua kutumia uwezo wao wote wa kufikiri na daima watu huwa ni watu kufanikiwa.

Jitume sasa na amua kutumika ili kuweza kufanikiwa. Mafanikio utayasikia kwa wengine kama wewe hujitumi kwa nguvu zote. Jenga mafanikio yako kwa kukubali kujituma haswa na kutumika vilivyo, na hapo utafanikiwa.
Kuna msemo maarufu wa ‘mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe’. Ni kweli ili uweze kutoka hapo ulipo na kuboresha maisha yako unatakiwa kutumika kwa kufanya kazi. Kazi ndio itakayokutoa kwenye maisha magumu na sio kitu kingine.
Acha kulalamika eti huna mtaji, acha kulalamika huku wakati umelala, amua kutoka hapo ulipo na amua kutumika kikamilifu ili kuhakikisha ndoto zako zinatimia. Ukiendelea kulala na huchukui hatua, ujue tayari umekwama.
Hapo ulipo una kila kitu, akili unazo, afya unayo, sasa unalalamika nini. Kama huna mambo hayo mawili, labda hapo inaweza ikawa changamoto kidogo kwako. Kitu kikubwa ninachotaka kukwambia, ni wewe ukubali kutumika ili kufanikiwa.
Watu wenye mafanikio wanajua vizuri kanuni hii na ndio maana ni watu wa kujituma na ratiba zao wanazipangilia vizuri sana kwa kukubali kutumika kwa kila namna. Wewe hutaki kutumika, halafu unataka mafanikio, kweli utapayapata?
Unatakiwa ujiulize mara mbili mbili, kwa nini unakwepa kutumika, ukiona hivyo uje ndani yako kuna ka uvivu na unatakiwa ubadilike mara moja. Kumbuka njia sahihi ya kukutoa hapo ulipo ni kwa wewe kukubali kutimika. Jitume rafiki na UTAFANIKIWA.

Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.

Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

Blog; dirayamafanikio.blogspot.com



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.