google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 10, 2020

Wape Watu Vitu Hivi, Utafanikiwa...

No comments :
Kanuni bora ya mafanikio ambayo unatakiwa uijue na kuitumia ni kwa wewe kuwapa watu zaidi vitu wanavyohitaji kuliko vile wasivyo vihitaji. Kama utajifunza kuwapa watu vitu vingi au yale mambo wanayoyahitaji, tambua tu pesa lazima wakupe.
Hakuna anayekwepa kukupa pesa, kama utampa anachohitaji. Na wakati mwingine inabidi ujifunze kutambua mahitaji ya watu hata kabla wenyewe hawajajua wanachohitaji na halafu wewe hakikisha unatimiza hilo na kuwapa.
Watu wenye mafanikio, kampuni zenye mafanikio, zinawapa wateja wao yale wanayoyahitaji, na hata wakati mwingine kabla hawajajua. Inawezekana hufanikiwi kwa sababu unawapa watu vitu ambavyo wewe unahitaji na sio wao.

Ukijua siri ya kuwapa watu vitu wanavyovihitaji, yaani ‘give people what they want,’ hakuna ubishi, utafanikiwa. Mafanikio yako yamejificha kwenye kuwapa watu vitu wanavyohitaji na kuacha kabisa kutowapa wasivyovihitaji, tafakari hili.
Ukitafakari utaelewa kwamba, nguvu ya mafanikio umejikita kwenye kuwapa watu vitu wanavyovihitaji. Angalia kampuni kubwa zinafanikiwa kwa kufanya kitu gani au mambo gani, utagundua zinafanikiwa kwa kuwapa watu vitu wanavyovihitaji.
Usipowapa watu vitu unavyovihitaji, utaishia kukwama au utaishia njiani na hautapata mafanikio unayoyataka. Jifunze kuwapa vitu wanavyotaka ili uweze kufanikiwa. Watu wanaofanikiwa wanawapa vitu watu wanavyovihitaji na kufikia mbali kimafanikio.

Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

Blog; dirayamafanikio.blogspot.com






No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.