google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 12, 2020

Kitu Unachosahau Sana Unapokuwa Kwenye Wakati Mgumu.

No comments :
Kipo kipindi ambacho unaweza ukajikuta upo kwenye wakati mgumu sana kwenye maisha yako, nikiwa na maana mambo yako kila ukiangalia hayaendi na unaona ni kama kila kitu kimesimama na unakuwa umeyumba.
Hiki ni kipindi kinachochanganya, ni kipindi ambacho kinakatisha tamaa, ni kipindi ambacho wengi huwa wanafikiri ni wao wanakipitia tu, kumbe kuna watu tayari walishapitia na kuvuka katika kipindi kama hicho.
Naamini, unaelewa mpaka hapa ninachoongea na pengine una uzoefu wa kupitia nyakati ngumu kama hizi ninazozizungumza hapa. Je, ni mawazo gani ambayo huwa yanakuja unapokuwa kwenye nyakati ngumu kama hizi.?


Najua huwa kuna mawazo mengi, lakini hata hivyo huwa kuna kitu ambacho wengi wanasahau sana wanapokuwa kwenye nyakati hizo ngumu. Kwa kusahau huku hupelekea kuingia zaidi kwenye tatizo badala ya kutoka.
Je, huwa unasahau nini unapokuwa kwenye wakati mgumu? Kitu ambacho huwa unasahau sana unapokuwa kwenye wakati mgumu ni kwamba unasubiri mambo yakawe sawa yenyewe na kusahau kuchukua hatua.
Kama upo kwenye wakati mgumu na unaendelea kusubiri mambo yakawe sawa yenyewe unajidanganya na kujipoteza. Unatakiwa kuchukua hatua, unatakuwa kutafuta njia na si kusubiri kusubiri hapo ulipo.
Unatakiwa kukumbuka, njia ya mafanikio yako haitafutwi kwa kusubiri, inatafutwa kwa wewe kuendelea kusonga mbele na si kusubiri subiri. Ukiendelea kusubiri hujishughulishi, nakwambia utaishia kukwama hapo ulipo.
Kama umekuwa ni mtu wa kufanya kosa hilo nikwambie, amka upesi kutoka hapo ulipo kwenye usingizi na kisha nenda kaipiganie ndoto yako na ili mambo yaweze kusonga mbele na kufika mbali kimafanikio.
Kusubiri subiri, kunaumiza matumbo, amka, nenda ukachukue hatua, tafuta njia ya mafanikio yako mwenyewe. Hakuna njia ya mafanikio itakayopatikana kwa wewe kuendelea kukaa hapo na kusema ipo siku mambo yatakuwa sawa.
Maisha ya mafanikio yanapatikana kwa kuchukua hatua ndogo ndogo za kila siku. Chukua hatua hizi ndogo kila siku, ili ufike utengeneze maisha yako. Kama huchukui hatua hizi ndogo, nikwambie unakwama na itakuwa ngumu kwako kufanikiwa.
Kumbuka, kitu unachosahau sana unapokuwa kwenye wakati mgumu unasubiri mambo yakawe sawa yenyewe na kusahau kuchukua hatua na kusahau kutafuta njia ya mafanikio yako. Jikumbushe jambo hili kila wakati, na uchukue hatua.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 

Nikutakie kila la kheri,

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.