google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 26, 2015

Mambo 6 Ya Kukusaidia Kutengeneza Biashara Itakayokupa Faida Kubwa.

1 comment :
Ili uweze kufanikiwa vizuri katika biashara yako, kwenye kipindi hiki chenye ushindani wa kila namna,  unahitaji kuwa mipango imara na utaratibu mzuri utakaoweza kufanya biashara yako ikasimama kwa muda mrefu bila kuteteleka. Watu wengi huwa wana mawazo ya kufikiri kuwa wana uwezo wa kutengeneza pesa na faida kubwa mara moja katika biashara zao  kwa kuwa wana mtaji na uwezo wa kufungua biashara wanao.

Kwa mawazo hayo, huwa yakiwapoteza wengi kutokana na ukweli kwamba mambo mengi yamebadilika kwenye biashara kwa sasa tofauti na siku za nyuma. Kitendo cha wewe kuwa na mtaji mkubwa siyo kipimo cha mwisho cha kukuhakikishia ni lazima biashara yako itatoa faida kubwa kama unavyofikiri. Yapo mabadiliko na mambo ya lazima ambayo unatakiwa uyafanye ili kuweza kutengeneza pesa za kutosha na si mtaji pekee tu.

Wapo watu ambao walianza na mitaji mikubwa katika biashara zao lakini hawakuweza kuona matokeo makubwa kama walivyofikiri. Na pia wapo watu walianza na mitaji midogo waliweza kufanya vizuri na kupata faida kubwa sana. Ninachotaka kukuonyesha hapa ni ujue  kuwa yapo mambo ya ziada unayotakiwa uyajue mbali na mataji ili ufanikiwe.  Lakini, sio nia yangu kukuonyesha uzuri ama ubaya wa mtaji mdogo au mkubwa katika biashara yako.

Kwa kuweza kujua mambo hayo itakusaidia hatua kwa hatua, kujenga biashara itakayoweza kukupa faida. Watu wenye mafanikio makubwa kibiashara,  moja ya siri kubwa wanayoitumia katika biasha zao ni kufanyia kazi mambo hayo kila siku. Hiki ndicho kitu tunachotaka ujue leo hapa kupitia makala hii. Ni mambo gani yatakayoweza kukusaidia kutengeneza biashara itakayokupa faida kubwa na endelevu?

Haya Ndiyo Mambo 6 Ya Kukusaidia Kutengeneza Biashara Itakayokupa Faida Kubwa.

1. Kuwa mbunifu.
Ipo nguvu kubwa sana ya kimafanikio ikiwa utakuwa mbunifu katika biashara yako. Bila kuwa na ubunifu wowote ule muhimu katika bishara yako, elewa utaachwa nyuma sana. Kwa kuwa mbunifu itakusaidia kujua ni wapi ulipo na uboreshe biashara yako eneo lipi ili uweze kushinda nguvu ya ushindani.

Kwa kadri unavyozidi kuwa mbinifu ndivyo mafanikio makubwa yanazidi kuwa upande wako. Biashara yoyote ile yenye mafanikio makubwa, ndani yake huwa ina ubunifu. Hili ni jambo mojawapo muhimu sana litakalokuwezesha kukusaidia kutengeneza biashara itakayokupa faida kubwa, ikiwa utalizingatia.



2. Kuwa tayari kwa ushindani.
Hiki ndicho kitu ambacho hutakiwi kukiogopa hasa linapokuja suala ushindani katika biashara. Kikubwa unachotakiwa kujua hapa ni hao washindani wako wanafanya nini cha ziada tofauti na wewe, ili nawe uweze kujifunza na ikiwezekana ufanye kama wao na pengine kuzidi zaidi ya hapo walipo. Kwa kufanya hivyo itakusidia kukabiliana na ushindani na kufikia malengo yako.

3. Kuwa na utaratibu wa kuweka kumbukumbu.
Karibu wafanyabishara wote wenye mafanikio makubwa huwa wana utaratibu wa kuweka kumbukumbu katika biashara zao. Kwa kuweka kumbukumbu muhimu itakusaidia sana kujua ni wapi ambapo unakumbana na changamoto na pia kujua ni eneo lipi unalopaswa kuliboresha zaidi. Hii ndiyo siri mojawapo unayoweza kuitumia kutengeneza faida katika biashara yako.


4. Kuwa tayari kujitoa mhanga.
Katika kipindi ambacho ndio kwanza biashara yako inaanza, ili kufanya biashara yako ikue kwa kasi unalazimika kujitoa mhanga ama kuchua ‘Risk’. Hii ndio njia muhimu itakayoweza kukuza biashara yako. Kuna wakati utalazimika kufanya kazi zaidi kuweza kujifunza hata kwa wengine ili kuona matokeo unayoyataka yawe kwako. Bila kujitoa mhanga juu ya biashara yako utachelewa kufika kule unakotaka kufika.

5. Kuwa mvumilivu.
Kuna wakati  mambo yanaweza yakawa mabaya na yakakuendea kinyume na ulivyotarajia, lakini kuwa mvumilivu. Hii ni nguzo muhimu kwako ambayo unatakiwa kujishikilia bila kuachia mpaka ufanikiwe. Matatizo yoyote yatakayo kupata kwenye biashara yako siyo mwisho wa mafanikio. Jifunze juu ya changamoto hizo na kisha chukua hatua ya kuendelea mbele zaidi. Vinginevyo, ukikata tamaa, utakuwa umejikwamisha wewe mwenyewe.

6. Kuwa tayari kutoa huduma bora.
Hii naweza kusema ndio funga kazi. Ukiweza kutoa huduma bora itakayoweza kukidhi matakwa ya mteja ujue tayari umefanikiwa katika biashara yako. Nasema hivyo kwa sababu, suala la kutoa huduma bora kwa wengi ni tatizo kubwa sana. Unaweza ukafanya uchunguzi mdogo tu, utaelewa ukweli zaidi wa hili ninalosema. Acha kufanya biashara ilimradi ufanye tu, jifunze kutoa huduma nzuri itakayomvuta mteja aje tena kwako kesho.


Tambua  kuwa, kuanzisha na kuendesha biashara itakayokupa mafanikio makubwa unahitaji kujua mambo hayo muhimu, lakini zaidi kuwa na nidhamu binafsi na king’ang’azi mpaka upate matokeo chanya. Kinyume cha hapo, hakuna mafanikio yanayokuja kama ndoto ni muhimu na lazima sana kujitoa.

Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza zaidi kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

1 comment :

  1. Thanks much!!!!!your opening mind of many blinded mind people!

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.