google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 10, 2015

Ili uweze Kufanikiwa, Una Haja Ya Kujifunza Zaidi Juu Ya Kitu Hiki Katika Maisha Yako.

No comments :
Je, unaweza kuandika orodha ya tabia zako zote? Kama unaweza kuziandika zitenge katika makundi mawili. Kundi moja liwe la zile ambazo zinakusaidia na zenye manufaa kwako  hata kwa wengine na kundi la pili ni zile ambazo hazina maana na hata zinawauzi na kuwakera  watu  wengine sana.

Kama utafanya zoezi hili kwa uaminifu huku ukiamini hakuna atakayeiona orodha yako , kuna mambo mawili huenda ambayo utafikiria kuyafanya. Kwanza, utasikitika kugundua kuwa baadhi ya tabia zako mbaya ni zile ambazo ungependelea kuziacha haraka ili kuboresha utu wako. Jambo la pili ambalo litakujia katika fikra zako ni kuongeza orodha ya tabia zako nzuri.

Unapoongeza tabia nzuri ni lazima utambue haziwezi kuwa kuwa tabia zako kwa kuziandika tu katika orodha. Katika zoezi hili watu wengi wenye akili timamu hupendelea kuwa na tabia nzuri nyingi zaidi. Ni watu wachache tu ambao huweza kufikiria kuongeza tabia zisizofaa.

Katika makala hii tutajadili jinsi mtu anavyoweza kujifunza tabia mpya na namna anavyoweza kuziacha tabia zisizo nzuri. Hata hivyo, tunapozungumzia tabia huna budi kukumbuka kuwa zinajumuisha tabia zinazojengeka katika akili ya mtu. Wala hatukusudii zile tabia zinazoingia katika kundi la vitendo hisia kama vile mtu kusikia njaa anapokaa muda mrefu bila kula chakula.


Lakini unapopata mawazo ya kuongeza tabia nzuri ina maana unatambua umuhimu wa tabia katika maisha yako ya kila siku. Hebu fikiria baadhi ya tabia ulizonazo. Asubuhi unaamka mapema, unaoga na kupiga mswaki na kuvaa nguo na viatu. Pengine kabla ya kutoka kitandani unaweza kufungua redio au televisheni ili kupata taarifa za habari. Baada ya kujitayarisha unajipatia kifungua kinywa na kuondoka nyumbani kuelekea kazini. Hizi ni baadhi ya tabia ulizojizoeza tangu ulipokuwa mtoto.


Mtu una tabia hizi tulizozitaja na nyingine nyingi ambazo zote kwa pamoja hufanya maisha yako kuwa mazuri nay a furaha. Kwa kawaida mtu hujikuta ana tabia nyingi na utaratibu wa maisha ambazo zimemwingia na kumvaa zenyewe na pengine bila kufanya juhudi ya kuzipata ama kuzifikiria.

Tabia zote hizo zinaweza kuwa kama vile ucheshi na kuzungumza vyema na watu, kuheshimu wanaokuzidi umri na kustahi wadogo, ukarimu na huruma kwa watu, uadilifu, staha, uaminifu na nyingine nyingi.jambo muhimu katika maisha ni kuzidumisha na kuboresha zaidi.

Kudhibiti mfumo wa kupata tabia tukumbuke kuwa kwa kufanya mazoea fulani tunaweza kusitukia tumebadili baadhi ya tabia. Inabidi tuwe makini kuepuka kujifunza tabia mbaya. Hii ni kwa sababu tabia mbaya hutupotezea wakati na kutufanya tushindwe kupata mafanikio katika maisha. Aidha ni dhahiri kuwa zipo tabia zinazoboresha mienendo yetu na kutufanye tupate mafanikio makubwa katika maisha.


Kumbuka kuwa kwa vile umeshakwisha kuwa mtu mzima juhudi za kuunda tabia mpya ambazo zitafanya maisha yako yawe mepesi  zinakutegemea wewe mwenyewe. Ulipokuwa ungali mdogo misuli na mfumo wako wa neva za hisia ulikuwa haujakomaa kiasi cha kukuwezesha kukabiliana na mazingira na kujenga tabia zote ambazo ni muhimu kwa maisha yako.

Wakati ule kila hatua ya maendeleo ya kupata tabia mpya ilitegemea mafunzo kutoka kwa wazazi, walimu na watu wengine waliokuzidi umri. Maadhali sasa umekua, wewe mwenyewe unaweza kufahamu sababu za kujenga tabia mpya. Ili kuunda tabia mpya unahitaji kuwa na dhamira na utashi wa dhati.

Licha ya utashi mkubwa jambo la pili ni kuandaa utaratibu thabiti utakaokufanya uitende tabia hiyo mara kwa mara ili uweze kujenga  mazoea ya kujiridhisha kuwa una chokifanya kitasaidia kuimarisha hiyo tabia.

Kanuni za kujifunza tabia mpya, kujenga tabia mpya na kujifunza kitu kipya ni kitu muhimu san asana kwako. Maana ya kujifunza ni nini? Kujifunza ni kujipatia mwelekeo fulani kikamilifu katika mfumo wa neva ya ufahamu. Hivyo kujipatia tabia mpya ni kujifunza kwa kufuata kwa kanuni kuu mbili zifuatazo

  • Kwanza kuwa na matakwa thabiti ya kujifunza.
  • Pili kuandaa mpango au utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ya kutenda tabia hiyo mpaka uimudu kuitekeleza kwa usahihi.
Hebu tutumie mfano ufuatao ili kuelewa jinsi ya kutumia kanuni hizi:-
Kulikuwa na mtu aliyekuwa akifanya kazi katika mji na akiishi katika kijiji cha mbali. Hivyo kila siku asubuhi alikuwa akiondoka nyumbani na kutembea kuelekea kazini. Na jioni hivyohivyo akipata taabu kwa kutembea kurudi nyumbani. Alikuwa amechelewa kufika kazini asubuhi na jioni pia alichelewa kurudi nyumbani.

Wakati huohuo kulikuwa na jirani yake aliyekuwa akitumia baiskeli kwenda kazini na kurudi nyumbani. Jambo hili lilimfanya Yule jirani yake ajiulize afanye nini kwa kuwa alikuwa hajui kuendesha baiskeli. Hata hivyo alikiri moyoni kuwa ingekuwa vyema kiasi gani kama angeweza kwenda na kurudi kazini kwa baiskeli kama wenzake.


Kama ungekuwa wewe ungefanya nini?  Hapana shaka ungeamua kufanya kama jirani yake kutumia baiskeli. Hivyo utakuwa na hunabudi kujifunza kuendesha baiskeli. Hii ni hatua ya kujifunza tabia mpya ya kuendesha baiskeli, hatua ya kwanza katika dhamira ya kujifunza tabia hii mpya itakuwa  ni kujizatiti katika utashi wako.

Hatua ya pili utaanza kujifunza jinsi ya kukaa juu ya baiskeli kwa uwiano ulio uzito sawa ili usiegemee upande moja na kukufanya ukaangika. Kisha utaanza kujifunzakuendesha baiskeli. Hatua ya tatu itakuwa ni kuweza kutambua kuwa ili uweze kuendesha baiskeli huna budi kufanya mazoezi.

Hivyo, utalazimika kupanga muda na kufanya mazoezi ili kuuzoesha mfumo wako wa neva uwe umejifunza na kukuwezesha kuimudu tabia hii mpya.hata katika mafanikio, ili uweze kufanikiwa ni lazima ujifunza juu ya tabia bora za mafanikio zitakazoweza kukufanikisha. Utaweza pia kujifunza tabia mbaya kwa kufuata pia hatua kama hizi.

Kanuni za kuacha tabia mbaya kama vile mtu anavyoweza kujifunza tabia mpya pia kuna njia ya kupangua na kutuplia mbali tabia usiyoipenda. Hapana shaka unaelewa jinsi mtu anavyosahau haraka jambo analolijua anapoliacha kabisa kulitenda kwa muda. Hii ndiyo njia unayoweza kuituumia ili kuacha tabia ambayo hupendi kuendelea nayo.

Tunaposema tabia mbaya tuna maana ule mwenendo ulionao unaowaudhi watu wengine na kuwafanya wapoteze imani na upendo kwako au ile tabia ambayo inaweza kukuathiri afya yako. Unapokusudia kuiacha taba mbaya unaweza kufuata tabia zifuatazo:-

Kwanza, uwe na nia au utashi thabiti wa kuiacha kabisa tabia hiyo. Pili, jiaminishe katika nafsi yako na ujidhihirise kikamilifu na uamuzi wako kwa nini uumeamua kuiacha hiyo  tabia na tatu, fanya mazoezi ya kuacha kuifanya hiyo utabia na hakikisha imetoka kabisa katika mfumo wako wa neva.

Hitimisho.
Tabia ndiyo inayomtofautisha binadamu na mnyama. Hivyo, kadri mtu aavyokuwa na tabia njema ndivyo kadri anvyouimarisha ubinadamu wake na mafanikio kwa ujumla. Kila mtu anawajibika kuhakikisha anaimarisha utu wake kwa kuongeza tabia bora na kuacha tabia mbaya kama makala hii ilivyotufunza.

Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YAMAFANIKIO kujifunza zaidi.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,


MAKALA HII IMEANDIKWA NA ABEID SAKARA, DAR ES SALAAM.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.