Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, May 2, 2016

Mambo Matatu Ya Kufanya Pale Unapohisi Umefanya Makosa Kwa Kile Unachokifanya.

No comments :
Hakuna mafanikio ambayo unaweza kuyapata bila kukosea. Na hakuna ambaye amewahi kufanikiwa bila kukosea.  Siku zote mafanikio yanakuja kutokana na makosa madogo madaogo yanayojitokeza iwe tunayataka au hatuyataki. Makosa haya ndio hutujengea uwezo wa kutusaidia kufikia kwenye mafanikio makubwa. Kama kuna sehemu umekosea, huna haja ya kulaumu, zaidi jifunze kutokana na makosa yako na kisha songa mbele.
Kwa hiyo kama makosa ni muhimu kutufikisha kwenye mafanikio? Kwa nini ulie, uhuzunike au kusonononeka sana kutokana na makosa yako? Kama ndicho umekuwa ukikifanya amka kutoka usingizini si wakati wa kukatishwa tamaa na makosa yako. Kitu cha ziada unachotakiwa kufanya ni kuyatumia makosa haya kukusaidia kufanikiwa. Kivipi? Twende pamoja kujifunza nini cha kufanya pale unapokosea.
1. Yaone makosa hayo kama ngazi ya mafanikio.
Kama umefanya kosa, usije ukafanya kosa tena lingine kwa kuruhusu makosa yako yakakukatisha tamaa. Ikiwa utaruhusu makosa ya kukatishe tamaa naweza sema kwa lugha rahisi huo ndio utakuwa mwisho wako. Siku zote, jaribu kuyaona makosa yako kama ngazi ya kukusaidia kufanikiwa. Unapokosea kitu, jifunze na kisha endelea mbele. Kama utayaona makosa kwako ni ngazi ya kukusaidia, ni wazi pia utafanikiwa kweli.

Jifunze kutokana na makosa yako.
2. Kubali kwamba umekosea.
Mara nyingi kwa wengi huwa sio rahisi kukubali eti kwamba wamekosea. Sasa ili uweze kufanikiwa inatakiwa uwe mwepesi wa kukubali kwamba chanzo cha makosa yote hayo kimetokana na wewe, hata kama sio. Kwa kukubali hivyo hiyo itakusaidia sana kuweza kujirekebisha na kuchukua hatua nyingine za kukusaidia kufanikiwa. Wengi wanaokubali makosa yao mapema na kukubali kujifunza siku zote huwa ni watu wa kufanikiwa.
3. Usikubali tena kurudia makosa hayo.
Jambo lingine la kufanya mbali na hayo mawili tuliyojifunza hasa pale unapokosea, usikubali tena kurudia kosa hilo. Kama usipokubali kurudia makosa yako itakusaidia sana kufanikiwa. Kitendo cha kurudia makosa yale yale siku hadi ni dalili nzuri mojawapo inayoweza kutuonyesha kwamba huwezi kufanikiwa. Muda wote kuwa makini sana, usirudie makosa ambayo umeshawahi kuyafanya kipindi cha nyuma. Ikiwa utarudia utakwama sana.
Kwa kujua na kuyanyia kazi mambo hayo matatu, yatakusaidia kuyatumia makosa yako vizuri na hatimaye kuweza kufanikiwa.
Tunakutakia mafanikio mema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu;- 0713 048035,


No comments :

Post a Comment