google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 26, 2016

Tunaposhindwa Kulinda Tunachokipenda Huvuna Maumivu.

No comments :
Wazazi wana nafasi gani kwenye kutuamulia maisha yetu ya uhusiano? Jibu la swali hilo linategemea mambo mengi. Mojawapo ya mambo hayo ni malezi yetu, na namna tulivyopata nafasi ya kukua kiufahamu nje ya malezi. Lakini ukweli ni kwamba, wazazi wana nafasi ya ushauri tu, kuhusu maisha yetu ya uhusiano. Lakini kwa bahati mbaya, wazazi wengi hujipa nafasi kubwa na mamlaka zaidi na watoto wengi huwaruhusu wazazi wao kuchukua nafasi hiyo.
Hebu tuchukulie kwa mfano mzazi ambaye anamkatalia mtoto wake wa kiume asimuoe binti aliye nyumba ya tatu kwa sababu ya kuona tu binti yule ni mfanyakazi wa ndani. Kwa tafsiri ya haraka haraka mzazi huyu anakuwa amemwona binti yule kama nusu mtu na asiyefaa kitu. Naye mtoto wa kiume pengine kwa kusikiliza ushauri wa mzazi anaweza kukubali lakini baadae inaweza ikawa majuto kwake ikiwa ataoa mwanamke ambaye atamtesa ingawa kiuhalisia anakuwa ametoka familia tajiri.
Lakini pia huwa inatokea sana kwa wazazi wanapoona mtoto wao awe wa kike au kiume akiwa amependana na mtu ‘choka mbaya kimaisha’ kwa wengi huwa sio rahisi kukubali mahusiano hayo na kujikuta kuweka vizuizi vingi sana kwa watoto ili wasiweze kuoana. Hapa watoto wasipokuwa makini hujikuta wamekubali walichoelezwa na wazazi wao na matokeo yake hujikuta kwa pande zote mbili kujuta kutokana na kujiingiza kwenye mahusiano yasiyo sahihi.

Linda unachokipenda, kisipotee.
Hali kama hizi zipo sana katika jamii zetu. Kuna wengi ambao ndoa zao zinaingiliwa sana na wazazi au hata ndugu zetu na pengine tu hata marafiki zetu na kujikuta hata kukosa uhuru. Hali kama hii inapokutokea na ukajikuta umekosa uhuru wa kuonyesha ukakamavu wa kuonyesha kile unachotaka kwenye mahusiano au ndoa yako utaumia sana. Utahisi dunia sio sehemu salama kwako kwa sababu ya kuhisi kama ndugu wanakuonea kila wakati. Kama hili limewahi kukutokea pole sana.
Naamini umeshawahi kusikia mikasa kama hii ya kuingiliwa kwenye mahusiano. Wengi wetu mara nyingi tunafundishwa namna ya kuishi na wake au waume zetu, kama tuendelee kuwa nao au tuwaache. Huwa tunawasikiliza wazazi, ndugu au marafiki na kuvunja uhusiano. Baadaye, kwa maumivu makubwa tunakuja kubaini makosa tuliyoyafanya. Tunajaribu kuunga palipokatika. Huwa inawezekana, ingawa mara nyingi haiwezekani tena.
Unaweza ukasambaratishwa kwenye mahusiano au ndoa yako na ndugu zako pasipo kujua na matokeo yake kuleta majuto makubwa sana. Na majuto hayo unaweza ukaendelea kuamini pengine ungedumu kwenye uhusiano wako wa mwanzo ungekuwa upo salama kimafanikio na kindoa pia. Lakini ulipo ‘moto’ umewaka kutokana na kwamba upo sehemu ambayo siyo sahihi. Ni kitu ambacho kina uwezo wa kukuuma sana siku zote na ukajikuta umeharibu kila kitu ikiwa pamoja na mafanikio sababu ya uhusiano.
Kumbuka kwamba, wewe ndiye unayetakiwa kusema na kuamini kwamba, umempenda fulani. Wewe ndiye unayetakiwa kulinda uhusiano wako kwa msimamo wa hali ya juu. Wengine wanakuwa wana uhuru wa kutoa maoni kuhusu penzi au mpenzi wako, lakini hawana ruhusa au nafasi ya kuamua kuhusu hatma ya penzi lako. Ikiwa kwa namna moja au nyingine utashindwa kulinda kikamilifu kile unachokipenda, elewa utavuna maumivu tena makubwa sana.
Tunakutakia mafanikio mema katika ndoa na maisha. Pia endelea kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.