google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 31, 2016

Misingi Mitano (5) Unayotakiwa Kuifahamu, Ili Kujihakikishia Kipato Cha Kudumu.

No comments :
Kati ya kitu ambacho kinatafutwa sana na wengi katika hii dunia ni pesa. pesa hiyo imeanza kutafutwa toka enzi za mababu na mababu mpaka leo. Juhudi za kutafuta pesa hadi kuipata zimekuwa ni kubwa sana kila kukicha. Kutokana na matokeo ya juhudi hizo, hiyo yote imekuwa ikitudhirishia au kutuonyesha kwamba kumbe pesa ni sehemu ya maisha yetu, tena maisha ya kila siku.
Lakini pamoja na juhudi kubwa za kuitafuta pesa hiyo bado lipo kundi kubwa la watu ambao wamejikuta wakiikosa pesa hiyo. Harakati zote za kuamka asubuhi na mapema na hata kuchelewa kulala kwa sababu ya pesa zimekuwa ni kama kazi bure kwa sababu hawaipati. Watu hawa wamekuwa  wakipishana na pesa karibu kila siku,utafikiri wao wanalaana na pesa hiyo hadi washindwe kuipata.
Hebu jaribu kuangalia kwenye eneo unaloishi jinsi pilika pilika za kutafuta pesa zilivyo nyingi. Lakini cha kushangaza pamoja na juhudi na pilika pilika hizo bado ni wachache wanaoipata pesa na kuwahakikishia kipato cha kudumu. Wengi wamekuwa wakitafuta sana pesa na kuishia maumivu na mateso ya kutokuipata. Sina shaka hali hii unaijua vizuri ya wengi kuendelea kukosa pesa ingawa wanaitafuta sana.
Kutokana na mazingira haya wapo ambao huanza kuamini wamelogwa. Na wengine pia huanza kuamini wana mikosi au laana. Je, kitu cha kujiuliza hizo ndizo huwa sababu halisi za wao kukosa pesa? Ukifatilia kimsingi, hizo sio sababu halisi za wao kukosa pesa, bali sababu hizo hutumika kama kisingizio. Watu hao kitu wasichokijua mara nyingi hushindwa kuwa na kipato cha kudumu kwa sababu ya kukosa misingi ya kuwaongoza.
Ndio. Naona unashangaa, inawezekana hata wewe ukawa kwenye wimbi la kutokuwa na kipato cha kudumu kwa sabau ya kukosa misingi ya kukuwezesha kuwa na kipato hicho. Kama unafikiria natania, kwa nini huna kipato cha uhakika na kudumu mpaka sasa? Nafikiri sasa, utakubaliana nami kwa kile ninachosema. Je, unajua misingi hiyo ni ipi unayotakiwa kuwa nyo ili kujihakikishia kipato cha kudumu?
1. Bajeti.
Hatua ya kwanza itayokuhakikishia wewe uwe na kupata cha kudumu ni kujijengea utaratibu wa kuwa na bajeti yako. Bajeti hiyo itakuongoza kujua pesa yako inatoka wapi na pesa yako inaenda wapi. Lakini  si hivyo tu, unapokuwa na bajeti inakusaidia pia kujua ni lini na wapi uweze kuwekeza pesa yako. Hivyo ni njia mojawapo muhimu sana ya kukuhakishia kipato cha kudumu kwenye biashara na maisha yako kwa ujumla.

Pesa unayopata hata kama ni kidogo, wekeza.
2. Kuwekeza.
Njia nyingine bora ya kukupa kipato cha kudumu ni kuifanya pesa yako ikuzalishie. Hakuna namna nyingine ya kuweza kuifanya pesa yako ikuzalishie zaidi ya kuweza. Kama una kitega uchumi kimoja, ongeza na kingine cha pili, cha tatu na kuendelea. Watu wenye mafanikio wana vipato vya kudumu kwa sababu wamewekeza katika maeneo mengi. Halikadhlika, nawe unatakiwa kufanya hivyo ili kuwa na kipato cha kudumu.
3. Kuweka akiba.
Kati ya kitu cha msingi katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa ni kujiwekea akiba. Kwa kiasi chochote cha pesa unachokipata, jifunze kuweka akiba. Akiba hiyo itakusaidia katika kuwekeza kwenye miradi mingine mingi baadae, lakini si hivyo tu pia ni njia mojawapo ya kukutengenezea kipato cha kudumu. Kama inatokea umeishiwa ni rahisi kuweza kuchukua pesa kwenye akiba yako kuliko kukopa kopa hovyo.
4. Kulipa madeni mapema.
Ni vyema ukajua mapema ili kujiweka salama katika safari yako ya mafanikio, jifunze kulipa madeni mapema. Unapokuwa unalipa madeni mapema inakusaidia sana kutokukuvurugia mambo yako mengi. Kama una mkopo benk au sehemu nyingine, lipa mapema ili uanze kuwa huru kutafuta pesa zako mwenyewe ambazo zitakupa uhuru mkubwa  wa kimafanikio. Kama unadaiwa kila wakati si rahisi sana kuendelea na kuwa na kipato cha uhakika.
5. Kuwa mjasiriamali mpambanaji.
Hautaweza kuwa huru kipesa na kujijengea kipato cha kudumu, kama leo hii hutaweza kuamua kuwa mjasiriamali mpambanaji. Amua kuwa mjasiriamali mpambanji unayetaka kutengeneza matokeo na sio mjasiriamali wa kulalamika kila siku. Hakuna mafanikio yanayoweza kuja au kupatikaa kwa kulalamika. Kama kuna changamoto zitatue na utafika mbali kimafanikio kipesa.
Kabla ya kuweka kalamu yangu chini, naomba utambue kwamba kama hutojiwekea misingi hiyo imara ya kipesa, suala la kupata pesa na kuwa na kipato cha kudumu litakusumbua sana. Usishangae ukawa mtu wa kufukuza pesa siku zote za maisha yako bila mafanikio. Zingatia hili sana na chukua hatua.
Ansante kwa kunifatilia na pia washirikishe wengine waweze kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.