google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 12, 2016

Njia Huru Za Kimafanikio.

No comments :
Miongoni mwa kauli ambazo nilikuwa nasikia wakati nakua nilikuwa nasikia wanasema maisha ni kama kioo ukicheka na yenyewe yanacheka. Kwa kipindi hicho sikuwahi kujua wanamaana gani watu waliyokuwa wanasema hivyo. Ila kwa bahati nzuri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ninavyoelewa walikuwa wanamaanisha nini.
Kwa utafiti wangu nimegundua ya kwamba katika maisha ya kusaka mafanikio ni lazima ujishughulishe kwa kutumia nguvu, kipaji, juhudi na maarifa ili uweze kupata mafanikio hayo. Na endapo utafanya kinyume chache utazidi kulaumu na kuishia kusema ndoto zangu ni kuwa mtu fulani na vitu kama hivyo.
Mwandishi mmoja anayeitwa Charles Nduku aliwahi kuandika katika kitabu chake cha ‘my plan, my life’ kwa kusema acha Kuota ndoto bali anza kufanya.

Kwa kipindi kirefu umekuwa unasema nataka kuwa hivi na vile. Kumbuka ya kwamba huu sio mda wa kusema maneno hayo. Ila muda wakuanza kutekeleza malengo yako. Watu wengi wapo vizuri zaidi kwa kusema kuliko kutenda, na ukichunguza vizuri watu hao hufa na ndoto zao. Badili mtazamo wako na kuwa ni mtu wa vitendo dhidi ya maneno.
Utaweza kubadili mtazamo wako na kuwa mtu wa vitendo ikiwa lakini utajifunza kutumia njia huru za kimafanikio. Kwa kusoma makala haya utajifunza njia hizo huru za mafanikio ambazo zitakufanya ufanikiwe. Naamini una hamu ya kutaka kuelewa ni njia zipi huru za mafanikio ambazo unaweza kuzitumia. Karibu na twende pamoja kujifunza njia hizo.

1. Tafuta nafasi.
Kwa kile ambacho unataka kuwa tafuta nafasi ya kutenda jambo hilo. Watu wengi kama niliposema hapo awali ni wazuri wa kusema kuliko kutenda. Kwa mfano kuna watu wanasema nataka kuwa muigizaji utamsikia akisema tu nataka kuwa muigizaji ila hatafuti nafasi ya kuwa muigizaji. Halikadharika hata wewe mwenye kitu cha tofauti, fanya kitu hicho na usiishie kusema tu haitakusaidia. Endapo utaishia kusema tu jiandae kufa na malengo yako.

Katika kutafuta nafasi ni lazima ujiulize nafasi hiyo ninayo au sina , kama sina naipata wapi? Ni nini kitu ambacho kinahitajika katika nafasi hiyo ninacho au sina kama sina nina kipata wapi? Ukipata majibu ya maswali hayo  lazima uweze kufanikiwa.

Tengeneza nafasi.
2. Tengeneza jina.
Katika jambo ambalo unalifanya ni lazima utengeneze jina ambalo watu wataweza kukufahamu kwa kile ambacho unakifanya. Utengezaji wa jina hutokana na kutengeneza huduma bora kwa watu wengine. Kwa mfano kuna siku nilikuwa katika harakati zangu za hapa na pale nikawa akapita mtoto mdogo ni kamuuliza yule mtoto et nitapata wapi chipsi mtoto yule akanijibu nenda kwa mpemba, wakati najiuliza ni kitu gani kinamfanya huyo mpemba mpaka watoto wadogo wamfahamu, nilipofika hapo kwa huyo mpemba ndipo nilipopata jibu. Ya kuwa ubora na usafi wake ndio uliomfanya atengeneze jina. Jina hilo ndilo linalomtengenezea wataja wengi.


Nadhani pia utakuwa  unawafahamu watu wenye majina makubwa ambao wanazalisha vitu vyenye ubora kwa hapa nchini. Kama ndivyo hivyo ni wakati wako na wewe kuweza kutengeneza jina kwa jambo ambalo unalifanya. Ifike wakati mtu akitaka kitu fulani hata ukimuuliza mtu yeyote hata awe mtoto mdogo awe anakufahamu kutoka na kile unachokifanya. Kama ilivyo leo kwa watu wengi maarufu unaowafahamu..
Ukiyafanya hayo hapo ndipo pesa zitapokuja kwa kasi zaidi. Mbinu hizo huru za kimafanikio wengi waliofanikwa ndizo ambazo walizozitumia. Zitumie leo uwe tajiri mkubwa.

Mwandishi: Afisa Mipango Benson chonya .
Simu; 0757-909942
E-mail;
 bensonchojya23@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.