google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 30, 2016

Usipokuwa Makini Na Mambo Haya, Yatakuzuia Sana Kufanikiwa.

No comments :
Ni matumaini ya tulio wengi ni kupata mafanikio kwa kila mambo ambayo tunayafanya, na ukichunguza kwa umakini  mara nyingi huwa hutapati kile ambacho tukitamani huku changamoto zikiwa nyingi kuliko mafanikio yenyewe. Huku wengine wakiamua hata kutumia njia zisizo rasmi katika kusaka mafanikio hayo na yote hufanyika kwa sababu ya tamaa iliyoko ndani ya mtu katika kutekeleza malengo yake. Na ukiendelea kufanya uchunguzi huo utakuja kugundua kuwa idadi kubwa ya watu hao huenda wasipate mafanikio hayo na kupoteza fedha nyingi zaidi ya kile wanachokitafuta.
Kwa kuwa mimi huwa naamini sana katika kufanya utafiti. Niliendelea kufanya utafiti ili kujua sababu zingine na vikwazo ambavyo mara kadhaa vimekuwa chanzo cha watu wengi kutokufanikiwa zaidi. Nakusihi ufuatane nami kwa kujifunza kupitia Makala haya mwanzo hadi mwisho.
Vifuatavyo ndivyo vikazo ambavyo vinasababisha watu wengi kutokufanikiwa.
1. Kutokujua pesa inafanya matumizi yapi.
Mara nyingi nimekuwa nikieleza kuhusu pesa, Pesa kwa sababu ndizo tunazozitafuta ili kupata mafanikio. Ila mambo yetu huwa hayawi kama tunavyotaka hii ni kutokana na kutokujua jinsi ya matumizi sahihi ya pesa kwa maneno mengine naweza sema kuwa hatuna nidhamu ya pesa. Kwa kuwa na maana hatujui pesa tunazopita zinatakiwa kutumika kwa utaratibu, ukitaka kubaini juu ya ukweli huu tofauti na daftari za kumbumbuku za biashara yako je una daftari inayohusu mapato na matumizi yanayohusu maisha yako binafsi na familia kwa ujumla?
Kama haupo katika misingi hiyo anza sasa kuwa na daftari ambalo utajaza kila kitu kinachohusiana na matumizi yako ya kifedha   na familia kwa ujumla. Pia kama una amini katika kujifunza kama mimi soma kitabu cha "rich dad, poor dad" kilichoandikwa na Robert Kayosaki ambacho kitakupa mwangaza zaidi juu matumizi sahihi ya kifedha.

Ipe thamani elmu yako itakufanikisha.
2. Kutoipa thamani elimu yako.
Hapa ndipo ambapo kunatufanya tuwe maskini zaidi. Mara nyingi mtu anashindwa kufanya kitu fulani kwa sababu hana elimu. Siwezi kulaumu sana maana tumeshakuta mifumo ambayo inatuambia msomi ni yule mwenye elimu ya chuo kikuu kwa maana shahada( degree) . Na kwa kuwa mifumo hiyo ndiyo ambayo tumeikuta na tumekuwa tukiamini hivyo. Na kwa kuwa imani ina nguvu basi tunajikuta wengi tunaamini hivyo. Na wale ambao kwa namna moja au nyingine hawana elimu hiyo ya chuo kikuu hujikuta wanafanya mambo ambayo siyo rasmi kama vile wizi, ukahaba na mengineyo mengi hii ni kwa sababu waliaminishwa ya kwamba elimu ni ufunguo wa maisha na kwa kuwa wao hawana elimu hiyo hujikuta wanafanya mambo ambayo sio ya kisomi.
Tatizo kubwa ambalo linasabisha yote hayo ni kutoipa thamani elimu iliyo nayo kwamba unaweza kufanya mapinduzi makubwa ya kimafanikio. Mtu anashindwa kufanya jambo fulani eti kwa kisingizio cha elimu aliyonayo. Mtu utamsikia si unajua niliishia darasa la saba au sikubahatika kumaliza elimu ya sekondari. Maneno hayo ni sumu kuliko ilivyo sumu ya panya katika swala zima la kimafanikio.
Hebu tuangalie watu wawili ambao ni uhakika unawafahamu sana. Yule tajiri ambaye ameamua kuilisha Tanzania kwa vyakula na vinywaji na kuuza ving'amuzi je elimu yake ni ipi?  Haya yule msanii anayetuwakilisha vizuri hasa katika kuitambulisha vizuri nchi yetu kimataifa je na yeye elimu yake ni kiasi gani? Usinipe majibu ila nikuombe uweze kufuatilia kwa umakini juu ya elimu zao ili kujua kwa undani ili kuipa thamani ya elimu uliyo nayo uone ni jinsi gani elimu hiyo uliyonayo inaweza kufanya mabadiliko makubwa ya kimafanikio binafsi na jamii kwa ujumla.
Niweke nukta kwa kusema mafanikio makubwa yanakuja kama utaamini kile ulichonacho.
Nikutakie siku njema na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza.

Imeandikwa na afisa mipango; Benson chonya.
 E-mail; 
bensonchonya23@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.