Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, May 13, 2016

Usiruhusu Magumu, Kukuzuia Kufanikiwa.

No comments :
Ni vigumu sana kusikia kile ambacho wengine wanakukosoa ikiwa kweli umejitoa kufanya kazi kwa bidii zote bila kuangalia mtu. Kukosoa huko hakutasaidia kitu, kwa sababu utajali na kuangalia matokeo yako yaliyo mbele yako.
Ni vigumu sana kujenga tabia ya kuamka asubuhi na mapema ikiwa unachelewa kila wakati kulala na kulala kidogo. Kama nia yako ni kujenga tabia ya kuamka asubuhi hutaweza kama umejijengea tabia hii.
Ni vigumu kutabasamu na kufurahia maisha yako ikiwa ndani mwako tayari umejitengenezea huzuni ya kutosha.
Ni vigumu pia kufikia mafanikio makubwa ikiwa ndani yako, unaona huwezi kufikia mafanikio hayo.
Ni vigumu kuwaongoza wengine kama hata wewe mwenyewe unashindwa kujiongoza.

Ng'ang'ania mafanikio.
Ni vigumu kuwa king’ang’anizi na nidhamu ya kufikia mafanikio makubwa ikiwa kile unachokifanya hakikupi matokeo unayoyataka.
Sio rahisi pia kuanza upya kwa haraka kwenye jambo ulilokuwa ukilifanya ikiwa umeanguka, hiyo itakuwa ni ngumu kidogo.
Ni vigumu kwenda mbele zaidi ikiwa ndani yako unaona umefika mbali kimafanikio.
Kwa kawaida njia ya mafanikio ina mambo na vizuizi vingi sana ambavyo kila mtu anatakiwa kukabiliana navyo ili kushinda. Hakuna urahisi katika kutafuta mafanikio. Wenyewe wanakwambia ‘No easy road’.
Magumu yanajitokeza wakati unatafuta mafanikio yapo na hayakwepeki. Hakuna ujanja wa kuyakwepa , jambo la muhimu ni kukabiliana nayo mpaka kuyashinda.
Acha kuogopa kukosea, kumbuka bila kukosea huwezi kufanikiwa sana na kufika mbali kimafanikio.
Kwa chochote unachofanya hata kama kuna magumu vipi hakikisha unasonga mbele. Acha kutoa visingizio havitakusaidia kitu zaidi, vitakukwamisha. Usiruhusu magumu yakakuzuia kufanikiwa hata kidogo. Chukua hatua na utabadili maisha yako.
Nakutakia siku njema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu;0713 04 80 35,

No comments :

Post a Comment