Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, June 7, 2016

Mambo Matatu (3) Yatakayofanya Kuboresha Kujiamini Kwako.

No comments :
Kujiamini ndiko kunakomfanya mtu aweze kufanikiwa zaidi. Watu wengi hawadumu katika mambo wanayofanya hii yote inatokana na kufanya vitu kwa kutojiamini. Tupo baadhi yetu tuna mawazo mazuri ila changamoto inakuja pale ambapo tunapotaka kuzitimiza. Changamoto yenyewe inakuja kwa kuwa haujiamini unajiona ni bora umshirikishe mtu mwingine, na kwa kuwa mtu huyo hana upeo wowote juu ya jambo hilo atakwambia usifanye na kwa kuwa ni mtu wako Wa karibu unaacha kufanya jambo hilo.

Mara kadhaa nimekuwa nikishika kalamu yangu kuandika ya kwamba moja ya changamoto kubwa ya watu waliofeli ni kwamba waliomba ushauri kwa watu ambao sio sahihi juu ya ushauri walioomba. Na kwa kitendo hicho kimefanya watu wengi kufa na Ndoto zao. Hivyo siku ya Leo ili kuokoa watu wengi wanaokufa na ndoto zao nimeona nilete makala hii uisomayo ili iweze kukupa  nguvu na hamasa ya kuongeza kujiamini kwako.
Yafuatayo ndiyo mambo muhimu ya kuzingatia ili kuongezea kujiamini kwako;
1) Tazama ni mambo mangapi umeyatimiza.
Hii ndio njia sahihi ya kuongeza kujiamini kwa jambo ambalo unalifanya. Kuna wakati umekuwa umepanga mipango mingi lakini mingi ikekuwa haikamilika hii ni kutokana haujiamini kwa mambo ambayo unayafanya. Kwa mfano mtu unaingia kwenye biashara ila huna imani kama itakuwa au laaah!Ili kujenga mahusiano kati yako na kujiamini ni vyema ukajua ni mambo mangapi ili yapanga na leo yemetimia na mangapi hayajatimia. Ukiona mambo mengi ambayo umeyapanga ukiona hayatimia ujue ya kwamba bado haujiamini kwa mambo yako. Ili kujenga uiamara wa kujiamini hakikisha ya kwamba kila unalopanga linatimia kwa wakati muafaka.


Tambua kilichomo ndani yako, kisha jiamini.
2) Tambua kilichomo ndani yako.

Moja za gumzo ya kujua kilichomo ndani yako kinakufanya uweze kujiamini na kufanikiwa zaidi. Kuna baadhi ya watu hawajui vitu vilivyomo ndani yao. Unakuta mtu anafanya biashara lakini kumbe kilichomo ndani yake ni ualimu, hata hivyo kwa kuwa anafanya kitu ambacho hakipo nafsini mwake, mwisho wa siku unakuta biashara hiyo inakufa mapema hata kabla ya muda wake kufika.

Kama ndivyo hivyo basi ni wakati wako muafaka wa kuhakikisha ya kwamba unatenga muda wako siku ya leo ili uweze kujua ni nini kilichomo ndani yako. Huenda huko ndiko mafanikio yako yapo upande wako, kama kilichomo ndani yako ni kufanyabiashara! basi ifanye kwa uhakika wa kutosha ila kama unahisi wewe ni muigizaji kaa katika misingi.

Na moja ya umuhimu wa kujua kilichomo ndani yako ni kwamba utakuwa mtaalamu kwenye kitu hicho. Kufanya yote hayo kutakufanya uweze kujiamini kwani huko ndiko ugali wa watoto wako ulipo.
3. Panga malengo ya muda mfupi.
Ukitaka kufanikiwa unachotakiwa kupanga ni kupanga mipango ya muda mfupi, hata yawe malengo makubwa kiasi gani, kumbuka kufanya hivi kutafanya uweze kujua mbinu mbalimbali za utekezaji wa malengo hayo. Moja ya kuweza kufanikiwa zaidi pindi upangapo malengo ni lazima ujue muda maalum wa kutekeleza malengo hayo.
Mfano kama unataka kununua gari nzuri andika lengo lako ni lini utanunua gari hiyo hii itakutia hasira za kufanya kazi kwa bidii ili uweze kufanikisha lengo hilo. Kufanya hivi Kutakujengea imani ya kujiamini ya kwamba unaweza kutimiza ndoto yako kwa wakati mfupi.
Ansante kwa kuwa pamoja nami na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Mwandishi; Benson Chonya
Simu: 0757-909942
Email 
bensonchonya23@gmail.com
Facebook; Benson Chonya

No comments :

Post a Comment