google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 21, 2016

Malezi Mabaya Ya Familia Ni Adui Wa Mafanikio.

No comments :
Miongoni mwa sababu kubwa iliyonifanya leo kuchukua kalamu  kuweza kumwaga wino wangu juu ya karatasi ni kwamba uvumilivu umenishinda ndani ya moyo wangu. Mambo yamenifika shingoni ni lazima niyaseme leo kabla umri wangu hajaelekea jioni (uzeeni). Hata nikiangalia saa nayo bado mishale inazunguka pia hata siku nazo hazijawahi kumsaliti lady jay dee kwamba siku zinaganda.
Siku chache zilizopita tuliadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kama ambavyo  huadhimishwa kila mwaka kitu hiki ni kizuri ambacho kinafaa kiendelezwe katika jamii tunazoishi kwenu kufanya hivi ni kudumisha amani na upendo kwa watoto wetu.
Tuachane na hayo kwani hayo yamekwishapita na wala haina haja tena kuzungumzia masuala ya maadhimisho hayo.  Ila leo nimeona ni vyema tuzungumzie kwa uchache juu ya MADILI BORA YA FAMILIA.  Jamii ya leo imekosa elimu tosha juu ya malezi bora kwa familia.
Hebu jaribu kuzunguka mtaa wa kwanza utagundua kati ya watoto 9 kati ya 10 wanazungumza lugha za matusi zaidi  kama wanaimba nyimbo za injili au bongo fleva. Ukitoka mtaa wa kwanza pita mtaa wa pili huko nako utastajabu ya Musa maana huko watu wazima na akili zao wanacheza nyimbo za vigodoro, baikoko pamoja na watoto wao.
Watu wazima hao ukichungunza kwa umakini utagundua nguo ambazo wamezivaa ni fupi mithili ya mabawa ya nzi, watu hao nguo ndefu na za heshima kwao huwa ni zenye upupu. Mmmh tunakwenda wapi?

Tena toka mtaa pili ingia mtaa wa tatu huko nako utashangaa kuokota dhahabu mchangani, watoto wadogo wamekuwa ndio wanaigizwa kununua bia, madawa ya kulevya na mengineyo mengi. Ukitoka mtaa huo jaribu kuingia mtaa mwisho huko nako kweli utaamini dunia inaelekea ukiongoni maana kuna mambo ya ajabu sio kawaida ya nchi, kama Tanzania huko utakutana na watoto ambao ni omba omba wengi ambao waliletwa duniani na wazazi wenye akili timamu kabisa, wazazi hawa huwa napenda kuwaita "sura ya mzee akili ya mtoto" maana hawafai hata kidogo.
Tunasema mara kadhaa kuwa kijana ni taifa la kesho. Maneno hayo yatadhibitisha ukweli huo kwa malezi mtindo huo? Ya kuwalea watoto malezi yasikuwa na heshima wala utukufu Mbele za Mungu. Kiukweli najaribu kujiuliza kwa umakini bila hata kupata majibu sahihi tunaelekea wapi kwa maisha ya aina hiyo?
Kimsingi ni kwamba ugumu wa maisha haya tunayasababisha sisi wenyewe walezi wa familia zetu kwa namna moja ama nyingine. Mara kadhaa tumekuwa tukiwatamkia maneno mabaya sana watoto zetu hata hivyo kupelekea madili mabovu kwa jamaii hii. Mfano wa maneno hayo wapo wale wanaowambia kuwa watoto wao ni wezi au vibaka.

Kila kukicha watoto wa mitaani wanaongezeka kwa idadi kubwa, ukichunguza kwa umakini juu ya hilo utagundua ya kwamba chanzo la ongezeko hilo ni mateso na mihangano mingi ya kifamilia ambayo kila baada ya sekunde  inafanya ongozeko la watoto hao.
Wapo pia baadhi ya wazazi huwakatisha tamaa watoto wao kwa namna moja ama nyingi pindi wakiwa wadogo na kusababisha maisha magumu kwa watoto na kuwapotezea dira ya maisha. Watoto yatima wanaachwa katika mazingira magumu sana ambayo kila mwanajamii hufumba macho pindi anapo watoto wa aina hiyo na kuona mtu huyo hausiki. Tunaelekea wapi?

Ikiwa tunasema ya kuwa dalili ya mvua ni mawingu kwa methali hiyo tunaweza tukafananisha na kusema ya kwamba dalili ya umaskini wa nchi ni mateso, chuki na migogoro ya kifamilia inaandaa kizazi chenye maisha duni ambacho kinaamini katika misingi ya kuombaomba, wizi, utumiaji wa madawa ya kulevya na tabia nyingine ambazo hazipendezi machoni pa Mungu na kwa watu wenye heshima zao. Nauliza tena tunaandaa kizazi cha aina gani?
Hebu kabla sijaenda kuweka nukta tuangalie malezi ya watoto katika baadhi ya familia nyingi. Katika kufanya utafiti nimegundua ya kwamba malezi ndiye ambaye yanaandaa kwa kiasi kikubwa mafanikio ya mtu kwa namna moja ama nyingine. Wazazi wengi hawana muda wa kukaa na kuzungumza na watoto wao, ili kujua watoto wao wanahitaji nini katika maisha yao, wazazi wengi wamekuwa wanafahamu ya kuwa mtoto ni lazima aende shule, apete mahitaji mengine kama kula, malazi pamoja na chakula huku wamesahau watoto wanahitaji zaidi ya hayo.
Hebu tujiulize ya kwamba ni mara ngapi umekaa na watoto wako kuongea nao kuhusu mambo mbalimbali yatakayomjenga kwa hapo baadae? Tujiulize tena hili tatizo na ongezeko la watoto yatima chanzo chake ni nini? Halafu kwa nini kila huwa  hatujali juu ya jambo hili.
Wito wangu ni kwamba tuache kuchukulia vitu katika taswira ya kawaida, najua suluhu juu ya jambo hili lipo payana kabisa, tuache kupita na gari kwa mwendo wa kasi ili tuone mambo haya yanavyowadhuru watoto wengi katika nchi yetu. Kuna usemi unasema mtoto wa mwenzio ni wako.
Ukweli juu ya kauli hii upo wapi? Kauli hiyo ipo kwa baadhi ya vituo vya kulelea watoto yatima na mazingira magumi ila katika taasisi na watu wengi kauli hiyo imekuwa haikuhusu. Tafadhari najua ujumbe umefika mahali pake hivyo ni wakati muafaka wa kuchukua hatua mahususi kuondokana na suala hili.
Ndimi, Afisa mipango Benson chonya.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.