Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, June 20, 2016

Mambo 8 Ambayo Watu Wenye Mafanikio Hawapotezi Muda Kuyafanya.

No comments :
Katika harakati za kutafuta maisha si ajabu sana kukutana na watu walio kata tamaa au watu wenye msongo wa mawazo inayotokana hasa na kuona ndoto na malengo yao hayatimii. Ni jambo ambalo huwa linatokea sana miongonii mwetu na kufikia mahali kuona maisha kama hayafai.
Lakini kitu nilichokuja kugundua, kipo chanzo kikubwa kimoja tu ambacho hupelekea kuona ndoto au malengo ya wengi kutokutumia na kusababisha msongo wa mawazo au kukata tamaa. Chanzo hiki si kingine bali ni kupoteza muda kwa mambo madogo madogo.
Ukiwa kama mjasiriamali ni muhimu sana kujua thamani ya kila sekunde unayoitumia. Sasa wengi hawalijui hili, wanapoteza muda hovyo na kujifanya wanatafuta mafanikio. Wajasiriamali waliofanikiwa hawapotezi muda wao kwa mambo yasiyowasadia.
Ni wakati umefika wa kujua kila thamani ya muda wako unaoutumia kuanzia dakika, saa mpaka siku nzima. Usipoteze muda kufanya mambo yanayokurudisha nyuma. Anza sasa kuishi kwa mafanikio, kwa kujifunza mambo ambayo wajasiriamali wenye mafanikio hawapotezi muda kabisa kuyafanya:-
1. Hawapotezi muda kwenye mitandao ya kijamii.
Kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama face book, twitter au instagram kuangalia taarifa za hapa na pale ni moja ya sehemu ya maisha yetu ya sasa. Lakini ikiwa utashindwa kutawala muda wako na kujikuta wewe ni mtu wa kuperuzi utapoteza muda mwingi sana ambao ungekusaidia kwa mambo mengine.
Watu wenye mafanikio wana nidhamu kubwa sana juu ya hili, na wakati wote huwa makini na mitandao hii ili isiwapotezee muda. Kama wewe ni mlevi wa mitandao ya kijamii, jiwekee muda wa kuingia huko na kuangalia mambo yako. Usiingie tu kwa kuwa unao muda. Yapo mambo mengi ya kufanya na muda ikiwa pamoja na kujisomea.

2. Hawapotezi muda kufikiria makosa yaliyopita.
Kila mtu anafanya makosa kwenye maisha yake, halikadhalika hata watu wenye mafanikio wanafanya makosa pia. Siri kubwa ya mafanikio ni pale unapokosea jifunze juu ya makosa hayo na ya kusaidie kuweza songa mbele zaidi ya pale ulipokuwa.
Inapotokea unafanya kosa, huhitaji kulia sana zaidi ya kujifunza na kuchukua hatua za kukusaidia kufanikiwa. Hata watu wenye mafanikio katika maisha yao wanapokosea, huwa hawapotezi muda kufikiria makosa yao na kikubwa wanachokifanya ni kuhakikisha wanajifunza na kuendelea mbele.
3. Hawapotezi muda kuanza siku yako bila kuipangilia.
Watu wenye mfanikio wana mipango ya kuwaongoza kufanikiwa kila siku. Ni watu wa kuandika mipango yao ya kesho siku moja kabla. Hivyo, wanapoianza siku wanakuwa wanajua ni wapi wanapotakiwa kuanzia na wapi wanapotakiwa kuishia kwa siku inayofuata.
Kimsingi, hakuna kitu kizuri kama kuianza siku yako kwa kuipangilia kwanza kabla hujaifikia. Ni utaratibu mzuri sana ambao haukupotezei muda na unakufanya uishi kwa ushindi. Watu wenye mafanikio hawapotezi muda kuainza siku yao bila kuipangilia, nawe pia unatakiwa kujifunza juu ya hilo.
4. Hawapotezi muda kufikiria mambo yanayofanywa na wengine.
Watu wenye mafanikio ni mara nyingi hawapotezi muda wao wa thamani kujilinganisha na watu wengine. Kwa kifupi, ni watu ambao hawaangalii sana wengine wanafanya nini ili nao wafanye. Ni watu ambao wana misimamo yao wenyewe na kuamini kile wanachokifanya kwamba kitawasaidia kufanikiwa hata kama ni kidogo.
Hata hivyo kumbuka si vibaya kuangalia au kushindana na yale ambayo wengine wanayafanya. Mtu pekee ambaye unaweza kushindana naye kwa yale unayoyafanya ni wewe mwenyewe. Kila siku unatakiwa kuwa bora zaidi ya jana ili kuyaweka maisha yako katika nafasi nzuri ya kufanikiwa.
5. Hawapotezi muda kuwa na watu hasi.
Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya mafanikio wanatuambia kwamba, tabia na mienendo yako kwa ujumla inaathiriwa sana na watu wanaokuzunguka. Watu wanaokuzunguka wana athari kubwa sana juu ya maisha yako, haijalishi athari hizo ni chanya au hasi.
Kwa kulijua hilo watu wenye mafanikio, huwa ni watu ambao hawapotezi muda wao kabisa kuwa na watu hasi. Kwa sababu wanajua watu hao watawakatisha tamaa na kuwafanya washindwe kufikia malengo yao waliyojiwekea. Hivyo hicho ni kitu amabacho huwasaidia sana kufanikiwa.
6. Hawapotezi muda kwa mambo wasiyoyaweza kuyatawala.
Katika maisha ya binadamu huwa yapo mambo na matukio ambayo katika hali ya kawaida huwa si rahisi kuyatawala. Matukio haya yanaweza yakawa kama ajali, ugonjwa, kufikiwa au hali mabaya ya uchumi. Haya ni baadhi ya matukio ambayo binadamu huweza kukutana nayo na sio rahisi kwake kuyatawala.
Kwa watu wenye mafanikio, wanapokutana na matukio ya aina hii, kwao huwa si rahisi sana kupoteza muda na kuendelea kuyafikiria. Kitu wanachokifanya yanapowakuta matukio kama hayo ni kuyapokea kama yalivyo, kisha baada ya kuyatatua basi huachana nayo na si kuendelea tena kuyafikiria kila wakati.
Kwa kuhitimisha makala haya, naamini umejifunza kitu kuhusiana na mambo amabayo watu wenye mafanikio ambayo hawapotezi muda wao kuyafikiria sana. Kitu cha kufanya chukua hatua za kuelekea kubadilisha maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri katika safari ya maisha yako. Kitu kikubwa ambacho kama DIRA YAMAFANIKIO tunakuomba ni kwamba endelea kuwashirikisha wengine ili waweze kujifunza kama wewe unavyofanya sasa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

No comments :

Post a Comment