Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, June 23, 2016

Je, Unahitaji Mafanikio Ndani Ya Muda Mfupi?

No comments :
Kuna wakati inakupasa uweze kuondokana kwenye jopo la watu ambao wanalalamika na kuingia kwenye kundi la watu ambao ni watu wasaka mafanikio daima na sio walalamikaji. Kuna baadhi ya watu huelekeza mawazo yao hasi katika kulaumu watu wengine kuliko kuwaza ni kwa jinsi gani wataweza kuyasaka mafanikio kiurahisi kabisa.

Mara nyingi sana tunatumia muda mwingi katika kufanya mambo ambayo hayana manufaa katika maisha yetu. Kwa mfano, tumekuwa tukipoteza muda kwenye mitandao au kupenda mazungumzo yasiyo na msaada kwetu. Kwa kuwa tunapoteza muda huo mwingi katika mambo yasikuwa na tija inafika mahali tunakuwa ni watu maisha ya kawaida kila siku.

Na ili kutoka hapo kwenye kuishi maisha ya kawaida, hakuna dawa nyingine zaidi ya kuacha kufanya mambo yasiyo na manufaa kwetu. Ukiweza kufanya hivyo, mafanikio utayapata tena kwa muda mfupi. Siri kubwa ya kupata mafanikio kwa muda mfupi ipo kwenye kufanya mambo yenye manufaa kwako kila siku na si kinyume cha hapo.


Najua unakuna kichwa unawaza “daaaah! sasa Afisa mipango kama nikitaka mafanikio kwa muda mfupi nafanyaje tena?” Kama ni hivyo na unataka kusikia jibu kutoka kwa afisa Benson nisikilize. Ili kupata mafanikio kwa muda mfupi, mbali na kutokufanya mambo ambayo hayana manufaa kwako pia zingatia sana yafuatayo:-

1. Amini nguvu iliyopo ndani yako kwamba unaweza.
Watu wengi hawaamini nguvu ambazo zipo ndani yao. Wengi huamini ya kwamba mafanikio huja kwa watu mafisadi peke yao. La hasha mafanikio yapo kwa kila mtu ambaye anamini ya kwamba yeye ni mshindi katika maisha yake, bila kuangalia ni changamoto ngapi ambazo amezipitia.

Unapokuwa unaamini uwezo na nguvu kubwa uliyonayo ndani mwako, inakusaidia sana kufikia mafanikio yako kwa muda mfupi. Kwa kadri utakavyozidi kuamini na kutumia vipawa na nguvu zilizopo ndani yako, utajikuta mambo mengi yanaenda vizuri tofauti na ulivyokuwa ukiwaza.

Tumia muda sahihi, kufikia mafanikio yako.
2. Kuwa na kusudi maalamu kwa chochote anachotaka kufanya.

Moja ya changamoto ya watu wengi ambao walifeli kimaisha ni kwamba watu hao walifanya vitu bila kujua ni nini kusudio lao maalumu, hata hivyo ikawapelekea watu hao kuweza kuwa na malengo ambayo hayana tija. Unakuta mtu anafanya biashara ukimuuliza kusudio la kufanya biashara hiyo utakushanga ya kwamba hata mfanyabiashara huyo huenda ukawa hajui pia.

Unahitaji kuwa na picha kamili ya jambo ambalo unalifanya kwa miaka ya mbeleni. Picha hii ndiyo ambayo itakuonesha utaweza kufanikiwa kwa kiasi gani? Au utashindwa kwa kiasi gani. Kama ni biashara ni lazima uwe na mlolongo mzima wa biashara yako jinsi itakavyokuwa kwa siku za mbeleni.

3. Usichukue ushauri wa kila mtu.

Kimsingi maneno ya watu yapo ambayo yanajenga kwa namna moja ama nyingine. Ila maneno ambayo hajajengi ndiyo yapo mengi zaidi, kwa mfano leo hii utaka kufanya biashara utakwenda kumshirikisha mtu ambaye yupo karibu yako unakwenda kuomba ushauri, mtu huyo atakwambia biashara hiyo hafai.

Utakapoambiwa biashara hiyo haifai mwishowe unajikuta unawabadilisha mawazo na kufanya jambo jingine na kwa kuwe wewe haujia amini unajikuta huna hata jambo hata moja ambalo unalifanya kwa uhakika. Mwishowe unakosa hata jambo moja ambalo lina manufaa kwako.


4. Fanya jambo la kwako.

Ili kufanikiwa kwa muda mfupi ni lazima kujua u wewe wako ndio siri ya mafanikio kwani moja ya watu wengi walioshindwa katika maisha ni kwamba waling'ang'ana kufanya vitu visivyokuwa vya kwao. Nikuache na swali la kujiuliza je jambo ambalo unalifanya ni lako?

Pia kumbuka maisha ya mwanadamu yanafanana na miiba ya michongoma kwa maana ya kwamba kila wakati uwe tayari katika kupambana na changamoto ambazo zinajitokeza kama ilivyo kwa miiba ya michongoma, maana miiba hii kila wakati upo  tayari kwa ajiri ya upambanaji tu.

Mwisho Afisa nimalizie kwa kusema akili ikiamua kufanya jambo inawezekana hivyo inahitajika nguvu ya mwili katika kuisaidia akili katika utekelezaji. Naamini ukifanya mambo hayo yatakusaidaia kufikia mafanikio yako kwa muda sahihi  unaohitajika.

Tunakutakia siku njema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati. Karibu sana na tupo pamoja.


ANGALIZO; Lengo la makala hii ni kukuhamasisha kufikia mafanikio yako kwa muda sahihi kama inavyotakiwa iwe. Lakini usije ukafikiri makala hii inakutaka utumie njia za mkato ili ufikie mafanikio yako kwa muda mfupi. Makala hii inahitaji uachanae na mambo yote yatakayokupelekea uchelewe sana kufanikiwa. 

Imeandikwa na afisa mipango: Benson Chonya.

No comments :

Post a Comment