Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, October 18, 2016

Aina Tano Za Mafanikio Ambazo Ni Muhimu Kuzifahamu Na Kuziishi-2

No comments :
Wiki iliyopita tuliangalia aina mbili kati ya tano za mafanikio ambazo ni vyema ukazifahamu na kuziishi, nitumie fursa hii kukushukuru wewe ambaye ulichukua hatua kwa kuanza kuzitekeleza aina mbili hizo za mafanikio ambazo nilizieleza kwamba ni mafanikio ya kiroho na mafanikio ya kimahusiano.

Hivyo nichukue wasaa huu kuweza kukakaribisha tena ili twende sawa, katika kuzijua aina nyingine za mafanikio ambazo ni vyema kuzifahamu siku ya leo, na sio kuzifahamu tu bali kuziishi kwani kufanya hivyo itakusaidia kupigia hatua zaidi za kimaendeleo.

Je unataka kujua ni aina zipi za mafanikio ambazo zilisalia? Usipate tabu twende sawa;

Zifuatazo ndizo aina za Mafanikio ambazo ni vyema kuzifahamu na kuziishi.

3. Mafanikio ya kiafya.

Najua utakuwa unashangaa baada ya kuona aina hii ya mafanikio ambayo unatakiwa kuwa nayo, wala usishangae huo ndio ukweli ni lazima uwe na aina hii ya mafanikio. Ni ukweli ambao upo bayana machoni petu ya kwamba ni vyema kila mmoja wetu awe na afya njema kila wakati.

Kuwa na afya njema ni jambo jema sana kuliko kuwa mgonjwa, najua utakuwa shahidi mzuri hasa pale ambao ukiugua maisha yako huathirika kwa kiasi gani, bila shaka utakuwa umegundua ya kwamba pindi uumwapo mambo mengi sana ambayo yanakuhusu wewe hukwama sana.Ndipo hapo ambapo ninapochukua jukumu la kukumbusha ya kwamba afya na uzima ambao unao leo ni vyema ukautumia katika uzalishaji hasa katika kufanya kazi kwa bidii kwani tambua ya kwamba kuna baadhi ya watu dakika hii wapo kitandani wanaumwa na walitamani kuwa na afya nzuri kama wewe. Hivyo fanya kazi kwa bidii.

Pia mara kadhaa nimekuwa nikikukumbusha ya kwamba ujio wako hapo duniani ni kwa lengo maalum, na pia kuna watu wanategemea ya kwamba utaacha alama hapa duniani. Kwa kulitambua hilo ni jambo la heri sana kuweza kumshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kukuleta katika dunia hii yenye kila aina ya vitu uvitakavyo.

Pia kwa kupitia misingi hiyo ni vyema ukaujali sana mwili wako kwa kufanya mazoezi, kula vizuri na kujiweka utaratibu ambao utasaidia kufanya uchunguzi wa afya yako kila wakati ili kujua kama kama upo sawa, kwa maana afya bora ni msingi imara wa mafanikio yako.

4. Mafanikio ya kifedha.

Hapa ndipo ambapo kila mmoja hutoa macho kupafikia na kusahau ya aina nyingine za mafanikio, na hii ni kwa sababu watu wengi huamini ya kwamba fedha ndio kila kitu, huenda ikawa ni sawa kwa namna fulani lakini sio kwa asilimia mia moja maana kama hautakuwa na afya njema, mahusiano bora ya Mungu na watu wengine huenda usifikie lengo hili la mafanikio ya kifedha, hivyo ni vyema ukawa na aina hizo nyingine za mafanikio kwanza.

Hata hivyo pasipo kuharibu radha ya aina hii ya mafanikio, katika kupata aina hii ya kimafanikio ni kwamba ni lazima uwe na mipango kabambe ambayo itakufanya uweze kutimiza malengo yako.

Kama unafanya biashara ni lazima upange mwanzoni mwa mwaka kwamba katika biashara yako unataka kutengeneza kiasi gani cha fedha? baada ya kupanga ni lazima pia uwe na mikakati madhubuti ambayo itaonesha ni kwa jinsi gani ambavyo unaweza kulifikia lengo lako.

Lakini nikumbushe ya kwamba katika kufikia aina hii ya Mafanikio kuna changamoto na vikwazo vingi sana hivyo huna budi kuweza kuishi katika misingi ambayo utakuwa nidhamu ya pesa, na kuweza kujifunza lile somo ambalo huwashinda wengi la uwekaji akiba.

Kulijua somo hili la uwekaji akiba litakufanya uweze kufikia malengo yako ya kifedha ambayo utakuwa umeyapanga mwanzoni mwa mwaka. Lakini kabla ya kuweka nukta katika pointi hii ni kwamba tengeneza bajeti ambayo itakuongoza, jambo hili ni muhimu sana kwani kutengeneza bajeti kutakufanya uweze kile unachokipata na unachokitumia, na vilevile kutakufanya kujua yapi ni matumizi ya lazima na yasiyo ya lazima.

5. Mafanikio ya kimaendeleo ya mtu binafsi.

Baada ya kuweza kupata aina hizo nyingine za Mafanikio. Aina ya mwisho ambayo Siku ya leo nitaishia kuizungumzia ni maendeleo yako binafsi, baada ya kupata hiyo aina ya nne ya mafanikio, unachotakiwa kukifanya ni kuweza kuongeza ubunifu, juhudi, nguvu katika kutekeleza suala hili la mafanikio yako binafsi.

Maendeleo ya mtu binafsi hutegemeana na mtu mwenyewe ni vitu gani ambayo alikuwa amepanga kuvipata mfano ni nyumba,gari viwanja mifugo na mengineyo mengi, na baada ya kupata vitu hivyo mtu huyo nafsi yake itakuwa imeridhika, japo falsafa ya mafanikio inasema hautakiwa kuridhika na hali uliyonayo ya kimafanikio kwani kufanya hivyo ni chukizo kubwa mbele ya Mungu na pia ni dhambi kubwa sana.

Ni matumiani yangu ya kwamba umajifunza mambo ya msingi ambayo kimsingi yatukusaidia sana endapo utayaishi, pia usiwe mchoyo wa vitu vizuri kama hivi, hivyo nikusihi ya kwamba uweze kumshirikisha mwingine ili naye aweze kujifunza.

Pia napenda kukukaribisha rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na namba yako kwenda 0713 04 80 35 ili uanganishwe.

©Ndimi Afisa mipango Benson Chonya.

No comments :

Post a Comment