Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, October 21, 2016

Usiruhusu Makosa Haya Yawe Sehemu Ya Maisha Yako.

No comments :
Yapo makosa ambayo hutakiwi kuyaruhusu mara kwa mara kutokea katika maisha yako. Ni muhimu kuzingatia hilo kwa sababu maisha tuliyonayo ni mafupi na kila hatua inatakiwa tuifanye kwa uhakika ili tusipoteze muda sana.
Kumbuka hata hivyo wengi wetu kuna wakati tunashindwa kufanikiwa sana kutokana na kuruhusu makosa ya aina fulani yatokee sana katika maisha yetu. Makosa haya ndio yamekuwa yakipelekea mipango mingine kuweza kukwama.
Je, ni makosa gani ambayo hutakiwi kuyaruhusu katika maisha yako mara kwa mara ili uweze kufanikiwa?
1. Usiruhusu  kutawaliwa na watu hasi.
Hata kidogo usiruhusu kuweza kutawaliwa na watu hasi. Usiwape nafasi kubwa ya kuweza kuwasikiliza. Ikiwa utafanya hivyo kuwaruhusu watu hasi, watakuharibia maisha yako sana kwa kukupa ushauri wa kukatisha tamaa na mwisho utaona maisha hayawezekani tena.

Acha kuruhusu woga utawale maisha yako.
2. Usiruhusu woga ukutawale.
Woga ni sumu kubwa sana ya mafanikio yako. Acha kuruhusu woga ukatawale sana. Kwa wale ambao huruhusu woga uwatawale kwa kiasi kikubwa hawafanikiwi. Hiyo hutokea hivyo kwa sababu hata hushindwa kuchukua hatua za kujaribu kufanya jambo jipya kwa sababu ya woga.
3. Usiruhusu kuiga sana.
Inapotokea ukawa unaiga sana kwa kawaida unaua ule ubunifu wako wa ndani. Hivyo kama unaiga kitu uwe na mipaka, lakini lilokubwa kwako unatakiwa kuwa mbunifu sana ili iweze kukusaidia kutengeneza mafanikio makubwa.
4. Usiruhusu kufanya jambo usiloweza.
Kama kuna kitu hukiwezi ni vyema usikifanye. Kukifanya kitu hicho huku ukiwa huwezi au huna hakuna na matokeo chanya hiyo itakuharibia sana sifa na maisha yako. Kila unapotaka kulifanya jambo fulani, hakikisha unalijua vizuri kwa undani ili likupe mafanikio.
Hivyo ni vyema ukatambua kwamba hayo ndiyo makosa ambayo hutakiwi  kutokuyaruhusu sana yatokee ili uweze kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kama itatokea unaruhusu makosa hayo sana maishani mwako, basi utakuwa unajitengenezea mazingira ya kushindwa mwenyewe.
Nikutakie siku njema na ansante sana kwa kutembelea  DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza. Kitu cha kufanya kwako, washirikishe na wengine waweze kupata maarifa haya bora.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,


No comments :

Post a Comment