Oct 31, 2016
Acha Kukata Tamaa, Mafanikio Yote Yanaanza Hivi…
Kama upo kwenye
safari ya mafanikio jifunze sana kutokuwa na dharau na kile kidogo ulichonacho.
Kama una kitu ambacho ni kidogo iwe pesa au uwezo fulani au kitu chochote
ambacho unaona ni kidogo kithamini sana kitu hicho.
Kitu nilichojifunza
katika safari ya kutafuta mafanikio ni kwamba, mafanikio mara nyingi huweza kuanza
kidogo kidogo sana mithili ya mbegu ya haladari. Kazi ya kukuza au kupapalia
kile kidogo ulichopewa ili kiwe kikubwa sasa hapo ndiyo inakuwa kazi yako.
Kwa mfano, kama ni
pesa huwezi kuanza na kuwa na pesa nyingi mara moja, katika maisha yako unaweza
ukaanza na pesa kidogo tu, lakini hizo pesa kidogo ukazifanya kama mbegu na
kuwekeza huku na huko na baadae kuwa pesa nyingi.
Kama ni gari,
nyumba, mtaji au maarifa fulani vyote hivyo huwa vinaanza kidogo kidogo na baadae
kuwa vitu vikubwa vya kushangaza. Chochote ambacho unacho hata kama ni kidogo
acha kukidharau hata kidogo zaidi kiheshimu.
Mafanikio yote makubwa, yanaanza kama mbegu. |
Tambua Hakuna
mafanikio ambayo yanaanza juu kabisa. Asili ya mafanikio yote makubwa yanaanza
kwa kuanzia chini. Hizo ndizo hatua za mafanikio. Wakati wote mafanikio yapo
kama hatua za mtoto mdogo ni lazima atambae kwanza kabla ya kutembea, na
mafanikio yapo vivyo hivyo.
Kwa hiyo kwa
kulijua hilo chochote ulichonacho hata kama ni kidogo vipi, mshukuru MUNGU
kwa hicho na kisha kifanye kiwe mbegu kwako ya kukusaidia kufanikiwa. Acha kuwa
na dharau na kidogo ulichonacho na kama ukiwa na dharau hutafika popote.
Kama una pesa
kidogo zitunze. Kama unafanya kazi unayolipwa mshara mdogo iheshimu kwanza kazi
hiyo, na halafu ile pesa kidogo unayoipata ifanye kuwa kama mbegu ya kukusaidia
kufanikiwa katika maisha yako kwa kuiwekeza.
Hapo ulipo hata
kidogo acha kuogopa kwa jinsi unavyoteseka na kusota kwa sababu ya kukosa pesa
au maisha magumu, ninachotaka kukwambia huo ni mwazo tu wa mafanikio yako.
Usikate tamaa endelea kupambana, Mungu yupo pamoja nawe.
Hakuna kitu ambacho
hakibadiliki hata maisha yako yanakwenda kubadilika ikiwa hutakubali kushindwa
na ukawa mtu wa kuchukua hatua. Siku zote kumbuka kuthamini kile kidogo
ulichonacho.
Kama unakumbuka katika
maandiko matakatifu wakati wana wa Israel wakiwa wamekosa tumaini na kuamini ni
lazima wafie katika bahari ya shamu, lakini Mungu aliwaokoa kupitia fimbo
aliyokuwa nayo mtumishi wake Mussa.
Hata wewe hapo
ulipo kipo kitu ambacho unacho hutakiwi
kukidharau. Kama Mussa angeizarau fimbo yake na kusema kwamba isingeweza kufanya
kitu basi wana wa Israel wangefia wote katika bahari ya shamu.
Kwa chochote
ulichonacho, chukua hatua. Kiheshimu hicho ulichonacho na kifanyie kazi. Kama unaona
unapata pesa kidogo sana, ziweke pesa hizo, acha kuzitumia hovyo na kusema haziwezi
kunisaidia kitu.
Hivyo, ili kufanikiwa ni
lazima utambue mafanikio yako huwa yanaanza kwa kidogo sana. Jukumu la kuyakuza
na kuyafanya yawe makubwa lipo mikononi mwako. Kama ni mbegu ya mafanikio tayari
unayo, acha kulaumu chochote zaidi, heshimu kidogo ulichonacho na utafanikiwa.
Endelea kujifunza
kupitia dirayamafikio.blogspot.com
Napenda pia
kukaribisha wewe rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na jina
lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
Hakuna gharama na karibu sana.
Tunakutakia kila la
kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Ni wako rafiki
katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.