Nov 7, 2016
Zijue Sifa Hizi Kwa Hakikisho La Mafanikio Yako.
Katika tafiti ambazo zimewahi
kufanyika katika chuo fulani nchini marekani, waligundua ya kwamba kuna tabia za
watu ambazo huwa zinafanana. Tabia hizo ni zile za kimafanikio, lakini zipo
tabia ambazo hazifanani kwa watu hao hao tena. Lakini katika tabia za watu
ambao wamefanikiwa idadi na takwimu wa mfanano huo upo kwa asilimia ndogo
sana.
Na kuwepo kwa asilimia ndogo hizo
zinatengeneza orodha ndogo sana za watu wenye mafanikio. Kama ndivyo hivyo ili
kuongezaka kwa idadi ya watu wenye mafanikio hatuna budi kujifunza kwa watu
ambao wamefanikiwa kwa kuangalia wao wana siri gani ambayo imewafanya waweze
kufanikiwa? Na suala si kujua tu bali kuweza kuyachukua yale mambo mazuri
ambayo wao huyatumia hadi kuwasababisha kuwa katika maisha mazuri.
Unaweza ukajiuliza labda ni kwanini
tujifunze kwa watu ambao wamefanikiwa, ili nasi tuweze kufanikiwa? wala usipate
tabu maana majibu ya maswali yako kuhusiana na watu ambao wamefanikiwa
tutakwenda kuyaangalia, kwa kuangalia sifa walizonazo ambazo zimewafanya
wao weweze kufanikiwa.
Zifuatazo ndizo sifa za watu wenye mafanikio;
a) Watu wenye mafanikio huwa ni watu
wenye kiu na shauku ya mabadiliko hususani katika upande wa mafanikio. Pia huwa
ni watu ambao kimsingi pamoja na mafanikio ambayo wamekwisha yapata huwa hawaridhiki
kwa hali waliyonayo japo tayari wamekwisha fanikiwa, kwani wao huamini ya
kwamba mafanikio hayana ukomo.
b) Hujali sana muda husasani katika
masuala ya ufanyaji wa kazi. Pia aina hii ya watu wenye mafanikio hawako tayari
kupoteza muda katika mambo ambayo hayaleti faida. Lakini kubwa kuliko
yote katika suala la kujali muda wao huamini ya kwamba mafanikio ni leo, huku
wakiendelea nini kifanyike leo na kama watataka kifanyike kesho, huendelea
kujihoji ni kwani kifanyike kesho? Kwa misingi hiyo na wewe mwenzangu
huna budi kujitenenezea utaratibu huo ambao utakusaidia kuweza kuwa bora katika
maisha yako.
c) Watu wenye mafanikio huugozwa kwa
malengo yao ambao wamejiwekea na kuyafuata na si kinyume chake. Msukumo wa
utekelezaji wa malengo ndio ambao umewawezesha kufika katika kilele cha
mafanikio. Hivyo hata wewe ili uweze kufanikiwa ni lazima uweze kuishi
ndani ya melengo yako ambayo umejipangia. kama utaamua kuishi kinyume na
malengo yako mafanikio itakuwa ni ndoto.
d) Wapo tayari kuwapoteza ndugu,
jamaa na marafiki ambao hawana msaada wowote katika mambo ambayo huwa
wanayafanya kila siku. Hufanya hivyo kwa sababu idadi kubwa ya watu
katika ulimwengu huu ni wakatishaji wa tamaa wa mambo ya watu wengine,
lakini idadi ndogo sana ya watu ndio ambao wanaweza kukusaidia katika mambo
yako ya kimafanikio. Hivyo ni vyema ukafanya uchaguzi sahihi kwa kuangalia ni
mtu gani ni sahihi.
Hizo ni baadhi ya sifa chache kati ya
nyingi ambazo watu ambao wamefanikiwa na wamekuwa wakiziishi na
kusabibisha wao kuendelea kufanikiwa. Mpaka kufikia hapo sina la ziada na pia
nikusihi ya kwamba badili maisha yako kwa kuwa na fikra sahihi.
Ndimi: Afisa mipango Benson Chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.