Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Sunday, January 1, 2017

Salamu Za Mwaka Mpya Kutoka DIRA YA MAFANIKIO.

No comments :
U hali gani mpenzi msomaji wa mtandao huu Wa DIRA YA MAFANIKIO? Ni matumaini yangu makubwa u mzima wa afya tele na unaendelea na kuifanya dunia ifurahi pamoja nawe katika kulisukuma  gurudumu hili la maendeleo. Endelea kufanya hivo kila wakati, kwani kufanya hivyo kutakufanya uweze kutimiza kusudio lako.

Lengo la maandishi haya ni kwamba uongozi mzima wa mtandao huu, inapenda kuchukua fursa hii adhimu kuweza kukupongeza sana kuweza kutembelea mtandao huu kila wakati kuanzia mwaka uliopita mpaka siku hii tulipouanza tena mwaka upya.

Lakini kama hiyo haitoshi najua fika wapo wengi ambao makala mbalimbali ambazo tumekuwa tukiziandika mahali hapa zimekuwa zikibadili maisha ya wengi, kwetu sisi ni jambo la faraja sana. Kwani tunapenda kuona maisha ya kila mmoja wetu katika ulimwengu huu yanabadilika na hatimaye kufikia lengo lake, hatimaye kuishangaza jamii.


Pia hayo yote yasingeweza kutokea bila uwepo wa utukufu wa mwenyezi Mungu ambaye kwa namna moja ama nyingine ameweza kutupa riziki pamoja na pumzi ambayo hatukulipia hata shilingi moja, na mpaka dakika hii tupo hai.

Uwepo wa uhai ndani yetu ni ishara tosha kwamba Mwenyezi Mungu yupo pamoja nasi kila wakati kwani ikumbukwe ya kwamba wapo watu wengi ambao walitamani kuwepo siku hii ya leo lakini hatupo nao tena, hivyo kwa kuwa mimi na wewe bado tupo hai hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kuyafanya yote hayo yaweze kutimia.

Na ikiwa leo ni tarehe 01 mwezi 01 na mwaka bila shaka unaufahamu vyema tunasherehekea sikukuu ya mwaka mpya. Hivyo kwa kulitambua hilo tunatambua mchango wako wa hali na mali kwa kuweza kuwa mtu wetu wa karibu kwa namna moja ama nyingine, hivyo tunapenda kukutakia sikukuu njema ya mwaka mpya na mafanikio makubwa kwako kila wakati.

Kwa niaba ya timu nzima ya DIRA YA MAFANIKIO tunakuahidi msomaji wetu kwamba tutaendelea kuwa na wewe bega kwa bega katika kuhakikisha maisha yako yanafika sehemu na unafanikiwa kwa viwango vya juu sana, ila hilo litawezekana ikiwa utakuwa ni mtu wa kuchukua hatua.

Kabla sijaweka nukta nataka kukumbusha ya kwamba kila wakati, unatakiwa kuweka juhudi na nguvu kwa kila jambo ambalo unalitaka liwe kweli. Lakini kwa mambo mazuri yanayopatikana katika mtandao huu ni vyema ukamshirikisha na mwingine.

Tuwatakie siku njema na  mwaka 2017 uwe wa mafanikio makubwa sana na yenye Baraka.

Imeandikwa na uongozi Wa Dira Ya Mafanikio.


No comments :

Post a Comment