Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, April 20, 2017

Jinsi Ya Kufanikiwa Katika Ulimwengu Huu Wenye Kelele Nyingi.

No comments :
Tunaishi katika ulimwengu ambao una vitu au mambo mengi yanayotutaka kila siku tuyafatilie tena ikiwezekana kwa ukaribu.
Si ajabu kuamka asubuhi ukakutana na meseji 50 kwenye wasap au ukakutana na habari nyingi ambazo unatakiwa uzijue na kuzifatilia.
Pia si ajabu kabla hujakaa sawa ukatumiwa meseji za kawaida au kupigiwa simu kabisa ambapo kikawaida unatakiwa uzijibu.
Si ajabu tena ukapewa ‘appointment’ na mtu ambayo unatakiwa uitekeleze ‘appointment’ hiyo bila kufanya hivyo unaweza kaanza kujihisi mnyonge.
Ukiangalia kwa siku moja unaweza kuwa na vitu vingi sana vya kufanya ambavyo vyote hivyo vinataka kutumia muda wako.

Kitu cha kujiuliza utafanikisha vipi mambo yote hayo kwa muda ulionao? Jibu ni rahisi tu hapo hutaweza.
Ili uweze kufanikisha karibu kila kitu hapo na kwenda katika hali ya usawa ya kufanikisha ukitakacho, unatakiwa kuweka nguvu ya uzingativu kwa jambo moja tu.
Kuwa na mambo mengi sana na kutaka kuyaacha yote kwa pamoja au kugusa gusa mara umegusa hiki, mara umeacha utajikuta hufanikiwi kwa mambo mengi.
Kitu kubwa unatakiwa kujiwekea ratiba ya vitu vya kufanya. Unapoamka asubuhi tambua kabisa ni mambo gani ambayo utayafanya.
Ukishayajua mambo hayo anza kutekeleza moja baada ya jingiine bila kuyumbishwa mawazo yako popote pale.
Ukishaweka mawazo yako pamoja, usiyumbishwe na kitu mpaka unahakikisha kazi ambayo ulikuwa umejiwekkea imeweza kufika mwisho kabisa.
Huwezi kufanikiwa ikiwa akili zako zitakuwa zinaruka ruka ruka mara huku mara kule, unatakiwa kutulia kufanya kitu kimoja tena kwa utulivu mkubwa.
Hakuna muujiza ambao unaweza ukautumia kuweza kufanikiwa katika dunia hii yenye mambo mengi zaidi tena bila kuweka nguvu zako nyingi za uzingativu pamoja.
Watu wenye mafanikio ndio wanavyofanya na kufanikiwa. Ni watu wa kufatilia jambo moja kwa umakini na utulivu mkubwa mpaka kuona kila kitu kipo sawa.
Hebu anza leo kuweka nguvu zako kwenye jambo lako moja hadi likupe mafanikio, kinyume cha hapo utakuwa unajidanganya sana.
Hivi ndivyo unavyoweza kufanikiwa katika ulimwengu ambao una kelele na mambo mengi sana, kikubwa weka nguvu ya uzingativu.
Chukua hatua katika kufikia mafanikio makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu.


No comments :

Post a Comment