Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Saturday, April 15, 2017

Tafakari Kwa Kujifunza Mambo Haya Yatakayoboresha Maisha Yako Leo.

No comments :
1. Mafanikio makubwa sana utayapata kama unafanya kitu ambacho unakipenda sana toka moyoni. Ikiwa hukipendi kile unachokifanya yaani unakifanya kitu hicho kwa kujilazimisha uwe na uhakika, hutafanikiwa sana.
Hivyo kila wakati pata muda wa kujiuliza je, ni kitu gani ambacho unakipenda? Kisha baada ya hapo kifanye kitu hicho kwa nguvu zote. Kumbuka siku zote mafanikio makubwa yanakuja kwa kufanya kile kitu unachokipenda.
2. Ni rahisi kufanikiwa na kupata karibu kila kitu unachokihitaji katika maisha yako ikiwa utakuwa tayari kuwasidia wengine nao kuweza kufanikiwa. Ndio maana mara nyingi watu wenye mkono wa ‘birika’ si rahisi sana kuweza kuwaona wakifikia viwango vya mafanikio makubwa.
Jiulize kitu gani ulichonacho ambacho unaweza ukakitoa na kikawa msaada mkubwa kwa wengine? Kama kitu hicho unacho hebu kitoe, acha kukaa nacho tu wewe peke yako, washirikishe na wengine ili kiwe baraka kwenu wote.

3. Kama unataka kuwa TAJIRI, kila wakati hakikisha unakuwa na akili ya kijasiriamali na kujitahidi sana kufanya yale kama wanayoyafanya matajiri hata kama umeajiriwai. Ikiwa utakwenda kinyume cha hapo sahau kabisa kuwa TAJIRI maishani mwako.
4. Kitu kibaya katika maisha yako ni kule kujishusha na kujiona ni mdogo kumbe wakati hata hauko hivyo. Wengi wanatabia ya kujishusha sana na kujiona ni kama wadudu kumbe ni wakubwa sana kuliko fikra zao hizo.
Hebu jiulize ni kwa nini unajishusha sana na kujiona hufai? Je, unafikiri kuna kitu ambacho umekikosa hadi ikapelekea ukajiona mnyonge kiasi hicho. Sikiliza hujaumbwa ili uwe mnyonge au uwe mdogo kama unavofikiri, wewe ni mtu tofauti sana.
Amini unaweza ukapata mafanikio mara kumi ya hapo ulipo sasa. Unashangaa, ndio unaweza kufanikiwa zaidi ya mara kumi ya hapo ulipo wala hutakiwi kujiwekea mipako. Kila kitu kinawezekana kwako ukiweka nia na kuamini, itakuwa.
5. Kila wakati jiulize ni kwa namna gani kupitia kile unachokifanya utakwenda kubadilisha maisha ya wengine na kuwafanya wawe watu wa mafanikio. Jitahidi kila siku uwe baraka kwa wengine. Weka juhudi si za kukusaidia wewe tu ila mpaka kuwasadia wengine pia.
Kwa hiyo unapotafuta pesa kumbuka zote sio zako, tenga angalau kidogo ambazo unaweza ukampa yule ambaye hajiwezi. Kama ambavyo nasema mara kwa mara, wakati mwingine mafanikio makubwa yanakuja kupitia utoaji wako. Je, unatoa kiasi gani kuwasaidia wenye uhitaji hapo ndipo mafanikio yako yalipo.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment