google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 12, 2017

Kama Unataka Kutunza Muda Wako Vizuri, Fuata Sheria Hizi Tatu Muhimu.

No comments :
Sina shaka wengi wetu wamekuwa  wakijua umuhimu na faida za kutunza muda vizuri, lakini kwa bahati ni wachache sana wanaofanikiwa kuweza kutunza muda wao vizuri. Wengi hujikuta ni watu wa kupoteza muda sana karibu kila siku.
Kitu cha kujiuliza ni kitu gani ambacho mara nyingi kinapelekea wengi wanapoteza muda wao, ingawa tayari wanajua au wameshaambiwa muda ni kitu cha thamani sana na ukipoteza muda huwezi kuurudisha tena?
Naamini kabisa kitu kinachopelekea wengi kuendelea kupoteza muda wao ni kwa wao wenyewe kutokujua sheria zinazofaa kutumiwa ili kulinda muda wao vizuri. Ni wakati muafaka umefika wa kujua sheria hizo ili ikusaidie kutunza muda wako vizuri.
Hata hivyo, kabla sijakwambia sheria hizo naomba nikwambie hivi mara nyingi watu wanaotunza muda wao vizuri, wanafanya mambo yao kwa uhakika mkubwa sana na kwa ubora wa hali ya juu.
Mpaka hapo unaona suala la kutunza muda ni la lazima sana kwako ili kuweza kufikia mafanikio ya juu. Ni wakati wako sasa wa kwenda pamoja ili tujifunze sheria za muhimu ambazo unaweza ukazitumia zikusaidie kutunza muda wako kwa ufasaha.
1. Weka vipaumbele.
Ili uwe na matumizi mazuri ya muda wako ni lazima uwe na vipaumbele ambavyo utakwenda kuvifanya kwa siku husika. Na vipaumbele hivi haviji kwa bahati mbaya bali vinatokana na majukumu ambayo umejiwekea kufanya kwa siku hiyo.
Kabla hujaanza kufanyia kazi orodha ya kazi ulizojiwekea kwa siku hiyo ni muhimu sana kwako kujua kitu gani cha muhimu na kitu gani sio cha muhimu kwako kukifanya. Sio kila jambo ni la muhimu katika kukufikisha kwenye ndoto zako.
Ili kujua hilo angalia hicho unachokifanya kinakusogeza kwenye ndoto zako au kinakurudisha nyuma na ndoto zako. Hivyo ukashaona hivyo, utajifunza na utaanza utaratibu wa kupangilia ndoto zako kwa ufasaha hadi kufanikiwa.

2. Vunja vunja  muda wako.
Kuna wakati kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu inaweza isikupe matokeo unayoyataka. Kama hiyo iko hivyo, maana yake unahitajika kuvunja vunja muda wako katika sehemu ndogo ili uweze kufanya kitu cha uhakika wakati akili yako ina nguvu.
Wataalamu wengine wa masuala ya muda, wanatuambia kwamba inachukua dakika 90 kwa ubongo wa binadamu kufanya kazi kwa ufasaha. Hiyo ikiwa na maana ukizidisha dakika hizo, hakuna kazi ambayo unaweza ukaifanya kwa ufasaha mkubwa tena.
Hivyo ni jukumu lako kuweza kuangalia ni muda upi ambao ni  rasmi kwako utautenga ili kutekeleza majukumu yako. Kwa mfano, unaweza ukaanza kufanya kazi kwa dakika 25 kisha dakika 5 unapumzika au unaweza ukavunja muda kwa jinsi unavyoweza wewe ili kuleta ufanisi.
Hii ni mbinu inayokusaidia ufanye kazi nyingi bila ya wewe kuweza kuchoka sana na kujikuta karibu umekamilisha kila kitu ambacho ulikuwa unakihitaji kukimalisha kwa muda wako husika.
3. Gawa majukumu kwa watu wengine.
Acha kuwa king'ang'anizi wa kujaribu kufanya kila kitu mwenyewe, jifunze kufuta watu ambao wanaweza kukusaidia majukumu ambayo sio lazima ufanye wewe. Wape watu kazi wakusaidie, hiyo itakuokolea sana muda wako kuliko unavyodhani.
Mbinu hii ya kugawa majukumu kwa watu wengine, ni mbinu mojawapo bora ya kukuokolea muda wao. Watu wenye mafanikio wanatumia mbinu hii kuweza kufanikiwa. Hakikisha unawapa watu wengine majukumu, ama ‘leverage’ ili wakusaidie kufanikiwa.
Endelea kujifunza kupitia mtandao wako bora wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano;  +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.