Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, April 24, 2017

Tatizo Kubwa La Kutokutaka Kukosea Wakati Unatafuta Mafanikio Ni Hili Hapa.

No comments :
Hakuna mafanikio ambayo unaweza kuyapata bila kukosea, kama hutakosea na ukaweza kufanikiwa basi wewe naweza kusema ni miongoni mwa watu ambao wana bahati sana. Mafanikio ni matokeo ya kujifunza kutokana na makosa.
Tatizo la watu wengi wanataka kufanikiwa lakini bila kukosea na wanasahau kwamba hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana kwa namna hiyo. Mafanikio yanakuja kwa kukosea na hilo si kosa, pengine kama unavyofikiri.
Unapotaka kufanikiwa bila kukosea, kiuhalisa huwezi kufanikiwa sana kwa sababu, tatizo kubwa la kutokukosea linakufanya ufanye mambo mengi kwa woga na mwisho wa siku kujikuta ukipata mafanikio kidogo sana.
Kwa hiyo ikiwa na maana kwamba kama unataka kufanikiwa, kukosea hakukwepeki, na wala hilo sio suala la kuanza kujutia, ninaposema kukosea si maanishi kukosea kwa makusudi bali naamanisha zile ‘mistake.’
Kama kuna kitu umelenga kukifanya, hebu kifanye kwa moyo wote, acha kuwa na woga. Ikitokea kama umekosea au umefanya makosa kwa bahati mbaya usisimame, endelea kusonga mbele na kutafuta kilicho bora kwako.
Kushindwa kwako kutakufanya ujirekebishe na kuwa na uwezo wa kufanikiwa kwa viwango vya juu sana. Acha kuumizwa na kutokutaka kukosea kwako, kwani kumbuka kila wakati tatizo kubwa la kutokutaka kukosea ni kushindwa kufanikiwa sana.
Unahitaji sana kujifunza kutoka kwenye kukosea kwako kila wakati, fanya maisha yako yawe shule bora ya kuweza kukusaidia kufanikiwa kwa viwango vya juu kabisa, hivyo ndivyo mafanikio makubwa yanavyojengwa.
Makala hii imeandikwa na Imani Ngwangwalu, DIRA YA MAFANIKIO.

No comments :

Post a Comment