Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Saturday, April 29, 2017

Kitu Chenye Nguvu Kubwa Kuliko Pesa Ni Hiki Hapa.

No comments :
Kwa wengi wetu si rahisi sana kuweza kuamini kwamba kipo kitu chenye thamani kubwa kuliko pesa. wengi huamini sana pesa ni kila kitu, kwamba ukiwa na pesa basi, ndio mambo yote yameishia hapo.
Lakini upo ukweli mwingine ambao pengine huujui. Mbali na thamani ya pesa yenyewe, malengo ni kitu ambacho kinathamani kubwa sana hata kuliko pesa yenyewe ,malengo ninayoyazungumza hapa ni malengo yanayofanyiwa kazi.
Kama una mashaka kidogo na hili, naomba uwangalie watu ambao kuna wakati wanaweza kupata pesa huku wakiwa hawana malengo ni kitu gani kinawatokea. Najua utagundua pesa zao zilipotea.
Unapokuwa una malengo hata upate pesa nyingi sana, si rahisi sana kupotea, tofauti na mtu ambaye anajiendea tu bila kuwa na malengo yoyote. Ni rahisi kuweza kufuata malengo yako na kufanikiwa.

Ipo nguvu kubwa sana kwenye kufuata malengo yako.
Kwa hiyo mpaka hapo unaona kwamba kitu ambacho kinaweza kuwa na thamani kubwa hata kuliko pesa ni malengo yenyewe. Hasa hili linakuja kutokana na nguvu ya malengo katika kupata pesa.
Pesa nyingi hazipo kwenye pesa yenyewe, pesa nyingi zipo kwa wale wanajiwekea malengo na kuamua kuyafuata kila inapoitwa leo. Kama una malengo imara na unayafuta pesa utapata tu.
Kwa vyovyote maisha yako yalivyo, kwa vyovyote na hali yoyote uliyonayo hata iwe mbaya vipi, hauwezi kutoka hapo na kufanikiwa hata upewe pesa nyingi. Pesa hizo utazipoteza usipokuwa na mikakati imara.
Kwa hiyo ili uweze kufanikiwa kipesa zaidi, hebu hakikisha una mipango imara, hakikisha una malengo yaliyo sahihi. Hapo utatengeneza pesa nyingi na kupata mafanikio.
Tunamalize makala hii kwa kusema kwamba, kitu kingine chenye nguvu kuliko hata ya pesa yenyewe ni  yale malengo unayojiwekea. Hicho ndicho kitu chenye nguvu kuliko malengo yenyewe.
Nikutakie siku njema na endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment