Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, April 10, 2017

Mtazamo Chanya Bila Kuwa Na Kitu Hiki Ni Sawa Na Bure.

No comments :
Inasemekana ya kwamba mtazamo chanya ni rasilimali tosha dhidi ya kuuaga umaskini, aidha watalamu wa masuala haya ya elimu ya mafanikio wanazidi kusisitiza ya kwamba ili mtu aweze kufanikiwa anakiwa kuibeba mitazamo  hiyo chanya kila wakati.
Lakini licha ya watu wengi kuibeba mitazamo hiyo chanya wamekuwa wakisahau kitu kimoja, kitu  hicho  ni muhimu sana kwani huenda sambamba na mitazamo hiyo chanya. Na leo nataka nikwambie kitu hicho, kwani kuwa na mtazamo chanya bila ya kuwa na kitu hicho ni sawa na bure.
Kitu chenye ni hiki, mtazamo chanya huenda sambamba na " kuwajibika" watu wengi kama ujuzi  na maarifa wanayo ya kutosha, ila tatizo ni kule kunakowafanya watu hao kuwa mtazamo chanya zaidi ila wamesahau kuwajibika juu ya kitu walichonacho.

Tangu umeanza kujifunza mambo mbalimbali ya mafanikio naamini mpaka sasa kwa sehemu fulani una mtazamo chanya juu ya jambo fulani, ila kinachokosekana kutoka kwako ni kule kunakoitwa kuwajibika juu ya mtazamo huo.
Hivyo mimi naamini kutokufanikiwa kwako kimaisha umeamua mwenyewe, nasema hivi kwa sababu hutaki kuchua hatua kwa ile hali uliyonayo, wengi huamini mafanikio huja kesho, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda hujikuta maisha yao yapo vilevile na hiyo kesho yao isiyokuwa na mipaka.
Kama wewe ni miongoni mwa watu wanaosema nitafanya kesho, nakusihi ya kwamba achana na dhana hiyo kwani mafanikio ya kesho hutengenezwa na leo, pia amini kwamba binadamu huishi siku moja, siku hiyo leo, kesho si rafiki kwako.
Hivyo kwa kile kidogo ulichonacho mathalani mtazamo chanya ulionao ni nguzo sahihi ya mafanikio yako endapo utaamua kuwajibika juu ya jambo hilo unalolifahamu. Kuchukua hatua ni sehemu kubwa ambayo itakutoa hapo ulipo kwenda sehemu nyingine ya mafanikio.
Ni wako Afisa Mipango Benson Chonya.
0757909942

No comments :

Post a Comment