google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 27, 2017

Mambo Kumi Ya Kuimarisha Maisha Yako.

No comments :
Maarifa ni msingi mkubwa wa mafanikio kwa jambo lolote lile. Ndio maana kwa kadri jinsi unavyozidi kuwa na maarifa bora na ndivyo maisha yako yanazidi kusimama na kuwa ya mafanikio makubwa.
Hivyo kwa mantiki hiyo ni muhimu sana kujifunza mambo yanayoimarisha maisha yako karibu kila siku. Hebu leo katika makala haya, twende pamoja tujifunze mambo kumi ya msingi yanayoweza kuimarisha maisha yako.
1. Washindi katika mafanikio hawafanyi sana mambo tofauti na unayofanya wewe bali wanafanya mambo hayo kwa UTOFAUTI.
2. Msingi mkubwa wa mafanikio unajengwa na mtazamo wako ulionao. Mtazamo ulionao ndio unaokufanya ufanikiwe au ushindwe katika jambo unalolifanya.
3. Mara nyingi fursa kubwa za mafanikio zinakuwa zipo miguuni petu au katika maeneo yanayotuzunguka. Acha kutumia muda mwingi  sana  kuangalia fursa zilizo mbali na wewe na kusahau pale ulipo.

Hapo ulipo pia kuna fursa, kuwa makini na eneo ulilopo kuangalia fursa zinazokuzunguka kufanikiwa. Unajua, ni rahisi sana kuona fursa zilizo upande mwingine na kusahau fursa ulizonazo karibu yako.
4. Fursa yoyote kubwa ikija kwako kama utaipoteza, sio rahisi fursa hiyo tena kuweza kujitokeza kwako kwa namna nyingine.  Kwa hiyo kama kuna fursa imejitokeza kwako na una uwezo nayo itumie kwa uhakika kukufanikisha.
5. Mtazamo wowote ulionao uwe chanya au hasi, unajengwa na mambo makubwa matatu, Mazingira yanayokuzunguka, uzoefu katika maisha na elimu. Hayo ndiyo mambo matatu yanayojenga mtazamo wako, Hakuna mtazamo unaojengwa nje ya  mambo hayo hapo.
6. Faida za MAWAZO CHANYA katika maisha yako.
      Kuongeza ufanisi na ubora katika kazi.
      Kuongeza faida kwa ukifanyacho.
   Kutatua changamoto nyingi kwa urahisi.
   Kupunguza msongo wa mawazo.
   Kudumisha mahusiano bora na ya wengine.
7. Hasara za MAWAZO HASI katika maisha yako.
   Msongo mkubwa wa mawazo.
   Kupoteza afya.
   Kuwa na hisia nyingi za maumivu.
    Maisha yako kukosa maana.
Pamoja na kwamba unajua hasara za mawazo hasi wengi wetu bado hawabadiliki unajua ni kwa nini? ni kwa sababu ni asili ya binadamu kukataa mabadiliko, hapo unahitaji nguvu nyingi ya kukutoa kwenye hali ya mazoea ili ufanikiwe kujenga mawazo chanya.
8. Hauhitaji elimu kubwa sana ambayo haina uwezo wa kubadilisha maisha yako, elimu bora ambayo unaihitaji au  unatakiwa uipate ni elimu ya kubadilisha maisha yako, elimu ambayo itakunyanyua au kukutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine kimaisha. Mafanikio yako makubwa yanakuja kwa kujipatia elimu inayotoa thamani ya maisha yako na sio vinginevyo.
Kwa hiyo kama kwa namna moja au nyingine umekosa elimu kubwa ya darasani na kufika mahali unajilaumu kwamba ningesoma ningefika mbali sana kimafanikio, unakosea, huu sio wakati wa kusikitika. Jifunze kutafuta elimu yenye thamani itakayobadilisha maisha yako. na habari njema ni kwamba elimu hiyo haipatikani darasani, inatafutwa mtaani kwa watu sahihi.
Ni mzigo mkubwa sana kwako na kwa jamii kwa ujumla kuwa umesoma halafu hauna mafanikio makubwa. Kama iko hivyo kwako, jiongeze kidogo tu, anza kuisaka elimu sahihi, elimu ambayo itakupa thamani sahihi ya maisha yako na kukubadilisha na kuwa mtu wa mafanikio. Maisha ya mafanikio hayaji kwa kusoma saana, bali ni kwa kujifunza vitu sahihi ambavyo vina uwezo wa kubadilisha maisha yako.
9. Kama vile ambavyo miili yetu ina hitaji chakula kizuri kila siku, pia akili zetu zinahitaji maarifa bora kila siku ambayo yataweza kutubadilisha hapa tulipo na kutupeleka eneo zuri zaidi kimafanikio.
10. Njia mojawapo ya wewe kujisikia vizuri ni kufanya vitu ambavyo hutaweza kuhitaji malipo yake kutoka kwa wengine. Unapojisikia vizuri ni rahisi sana kuweza kufanya mambo makubwa na kwa msukumo mkubwa pia ulio ndani yako.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.